Kuoa si jambo dogo, unatakiwa uwe umejiandaa

Kuoa si jambo dogo, unatakiwa uwe umejiandaa

Mna kaz sana watu wa mikoan, sie wala hatuna hizo habari. baba mkwe yupo kinondon, kwa wazee wangu Temeke. sie wenyewe tuko sinza. kutambulishana hata elf 20 haifiki. USIJE MJINI!!
 
Mna kaz sana watu wa mikoan, sie wala hatuna hizo habari. baba mkwe yupo kinondon, kwa wazee wangu Temeke. sie wenyewe tuko sinza. kutambulishana hata elf 20 haifiki. USIJE MJINI!!
Hahahaha kumbe na ww ni mwanaume wa dar
 
This is a one stupidity thread ambayo haiwapi courage vijana kufunga ndoa. Hakuna ukweli wowote in crap.

Hivi muowaji upo Sinza na muolewaji yupo mwenge kwa mfano kuna gharama zipi hapo? Tusiwatishe wadogo zetu kwa thread za hivi hazina maana ni total nonsense matokeo yake vijana wanaogopa kuoa wakati ni jambo la kawaida sana.
 
1. Kujitambulisha Ukweni. Hapo Utatakiwa Uende Kijijini Alikozaliwa Mkeo Mtarajiwa Ukajitambulishe Huko. Kama Mfano Mkeo Anatokea Mwanza, Na Mnaishi Dar, Andaa Nauli Ya Watu Wawili, Malazi Kwa Siku Mbili, Na Utagharamia Shuhuli Hiyo Ya Utambulisho. We Tenga 500,000. Hapo Tuna Assume Mkeo Atajitegemea. Otherwise 800,000 Itakutoka.

2. Kumtambulisha Mkeo Kwenu. Kama Nyie Nyumbani Ni Arusha, Utatakiwa Umpeleke Huko Ngarenanyuki. Sio Umlete Hapo Tabata Mlipopanga. Hapo Sio Kwenu! Andaa Nauli Yako Na Atakaekusindikiza, Nauli Ya Binti Na Mwenzie, Na Gharama Za Vinywaji Na Chakula Siku Hiyo. Utahitaji Kama 700,000

3. Kifuatacho Itv Ni Kuwaalika Wakwe Zako Nyumbani. Uwatoe Watu Kama Nane Mwanza, Uwalete Arusha. Wale, Walale, Wajisaidie, Kwa Gharama Zako. We Acha Ubishi, Tenga 800,000 Tu.

4. Kwani We Wazazi Wako Wanajua Unakooa? Sasa Je? Wasafirishe Kwenda Mwanza! Watu Watano. Utahitaji Kuwa Na 500,000. Beba Pia Atm Card Yako, Kuna Imejensi.

5. Mahari Ndio Topic Inayofuata Sasa. Ukiwa Mjanja, Unganishia Kwenye Hiyo Safari Hapo Juu Uue Ndege Wawili. Pamoja Na Hayo, Itabidi Ubebe 2,000,000.

6. Sasa Kijana Unaweza Kumvisha Mchumba Wako Pete. Nunua Ya Kawaida Kabisa Ya Dhahabu. 350,000. Tukio Lenyewe La Kumvisha Pete Unaweza Ita Marafiki Wawili Watatu Ukatumia 200,000. Au Fanya Sherehe Kabisa. Mi Simo

7. Oke, Sasa Unaweza Kuitisha Vikao Vya Harusi. Tengeneza Kadi Za Mwaliko Wa Kamati Kwa 200,000, Kikao Cha Kwanza Gharama Zote Ni Juu Yako. Andaa 500,000. Swali La Kwanza Kwenye Kikao: “We Una Shing Ngapi?” Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 Ya Sms Na Simu Kukumbushia Michango. (Shukuru Mungu Kuna Cheka Time)

9. Wakati Vikao Vinaendelea, Utatuma 200,000 Kwa M-Pesa Ili Mambo Ya Kimila Yaendelee Kule Nyumbani. We Unaelewa

10. “Darling, Sasa Mi Kwenye Kitchen Party Ntavaa Nini?” 300,000!

11. “Darling, Kuna Mahali Nimeona Gauni Zuri La Send…” 400,000!

12. “Baby, Rafiki Yangu Alinunua Gauni La Harusi China Yani Lilimpende…..” 700,000!

13. Wakati Huo Wewe Mwenyewe Hujajua Utavaa Nini, Hujanunua Pete Za Harusi, Hujamvalisha Best Man Na Mkewe. Tuseme Unahitaji Kama 1,500,000 Maana Utalia Lia Sana. Kumbuka, Gharama Hizi Huchangiwi Na Kamati. Wala Hutarudishiwa.

14. Siku Ya Send Off Lazma Uende Mwanza. Utaenda Mwenyewe? Ndugu Wawili Watatu Na Mshenga 600,000. Kwenye Send Off Utatakiwa Kutoa Sijui Blanketi La Bibi, Vitenge Vya Mashangazi, Na Vikorokoro Kibao. Nunua Hivyo Vitu 300,000 Uende Navyo Ili Kupunguza Gharama. Beba 200,000 Za Wale Mashangazi Watakaoibuka Ghafla!

15. Mshonee Baba Mkwe Suti 100,000 Mama Mkwe Yeye Atavaa Gauni La 50,000.

16. Fotokopi Hiyo Hapo Juu (Namba 15) Kwa Wazazi Wako. 150,000

17. Watu Watakaopenda Kuvaa Sare Wajitegemee! Mimi Sina Hela! Ila Utavishonea Nguo Vile Vitoto Kwa 80,000.

18. Siku Mbili Kabla Ya Harusi, Utaanza Kupokea Wageni. Unatakiwa Uwatafutie Malazi Na Chakula. Kwa Ujumla Utahitaji Kama 500,000

19. Jioni Watoe Auti Mashemeji Zako Ambao Hawajawahi Kufika Dar Ukawanunulie Bia Ili Wakuone Wa Maana. 200,000

20. Siku Ya Harusi Bibi Harusi Na Mwenzie Na Watoto Na Ma Maids Watatakiwa Wakapambwe Saluni. 200,000

21. We Na Mwenzio Mtaenda Kunyoa Hapo Kwa Nanii. Ndevu Na Nywele Na Black Kibishi 40,000

22. Siku Ya Harusi Beba Sadaka 10,000. Wakati Huo Umeshamtuma Kijana Akakulipie Hoteli Mtakayofikia Baada Ya Harusi. Kamati Haitoi Hela Hiyo, So Utalipa Malazi Ya Siku Mbili 200,000

23. Kama Mtaenda Honeymoon Sehemu Yoyote Nzuri Nzuri Nje Ya Mji, Si Chini Ya 800,000 Kwa Angalau Siku 5.

24. Wakati Uko Huko Honeymoon, Huna Hata Kumi, Mwanakamati Mmoja Ambae Hakuchanga Anakupigia Simu “ Sasa Tunavunja Lini Kamati?” Pesa Yote Iliyochangwa Ilitumika Kwenye Harusi, Sasa Gharama Za Kuvunja Kamati Ni Za Nani?? 500,000!

25. Sasa Mnaanza Maisha Ya Unyumba. 14,180,000 Poorer.
siwezi kusahau siku mke anakaribia kujifungua alafu mama mkwe na baba mkwe wamekomaa wanataka kuja kukaa nyumbani na hapo nilikuwa nimepanga chumba kimoja self maeneo ya kinondoni mkwajuni,na wife naye alikuwa amekomaa anataka wazazi wake waje kuweka bicon pale geto,kweli mwisho wa ubishoo ni majukumu daaaaah
 
Hahaha. Hilarious stuff. Hivi ulimwengu huu, bado kuna waliozaliwa vijijini?
Yeah, tupo wengi sana. Mjini tumekuja kutafuta maisha na ndio kumekuwa nyumbani. Lakini kila wakati huwa tunaenda home kuwajulia wazee hali. Tumefanya sherehe zetu viijini ili kutunza heshima za wazee wetu na hatuwezi kuwasahau japo kweli tunaishi mijini.

Na sio kweli kuwa kwa vile watu wanaishi mbali, gharama za mahari na sherehe zinakuwa kubwa kiasi hicho. Ameongeza chumvi nyingi.
 
Kuna ukweli..

Ila mimi na mke matarajiwa wangu tunataka tufanye process hizo bila kuomba mchango kutoka kwa watu.
Usipowaomba mchango pia hawaji watasema umewadharau, ukitaka kuwaweza waswahili waite waombe mchango then wewe cover mahitaji yote muhimu, Ukumbi, Mc na music, picha na video, chakula halafu wao waambie wachangie bajeti ya vinywaji tu. Hapo mtaelewana lakini usipowaita ukatowa kadi tu watakuja wale walafi watu potential na prominent figures huwa hawaendi kwenye harusi kama hujawaomba mchango.

Take it from me nimeishi na waswahili nawajuwa vizuri, hata kama nikifanya dissertation yangu kwenye tabia za waswahili napasua mbaya.
 
Yeah, tupo wengi sana. Mjini tumekuja kutafuta maisha na ndio kumekuwa nyumbani. Lakini kila wakati huwa tunaenda home kuwajulia wazee hali. Tumefanya sherehe zetu viijini ili kutunza heshima za wazee wetu na hatuwezi kuwasahau japo kweli tunaishi mijini.

Na sio kweli kuwa kwa vile watu wanaishi mbali, gharama za mahari na sherehe zinakuwa kubwa kiasi hicho. Ameongeza chumvi nyingi.

Ameongeza chumvi sana, si uongo. Mi nilidhani Tanzania ya leo, ina vijiji vichache sana. Kiukweli nikikutana na mtu under 30 anaongelea kuzaliwa kijijini, nashangaa flani hivi.
 
Ameongeza chumvi sana, si uongo. Mi nilidhani Tanzania ya leo, ina vijiji vichache sana. Kiukweli nikikutana na mtu under 30 anaongelea kuzaliwa kijijini, nashangaa flani hivi.
Acha utani bwana. Kwanza TZ ina vijiji vingi mno, refer shule za kata, nyingi zipo vijijini na vijana wengi sasa wanajiunga na shule hizo.
Paulo, kwani hujawahi kwenda vijijini? Japo kweli there's a huge shift of population from rural to urban regions, lakini bado waliozaliwa bush ni wengi mno.
 
Usipowaomba mchango pia hawaji watasema umewadharau, ukitaka kuwaweza waswahili waite waombe mchango then wewe cover mahitaji yote muhimu, Ukumbi, Mc na music, picha na video, chakula halafu wao waambie wachangie bajeti ya vinywaji tu. Hapo mtaelewana lakini usipowaita ukatowa kadi tu watakuja wale walafi watu potential na prominent figures huwa hawaendi kwenye harusi kama hujawaomba mchango.

Take it from me nimeishi na waswahili nawajuwa vizuri, hata kama nikifanya dissertation yangu kwenye tabia za waswahili napasua mbaya.
Kuna ndugu yangu alipotaka kuoa aliwafuata marafiki zake (ni wakubwa sana kwake kwa umri) akawaambia anaoa na anaandaa kadi ili awape na hatahitaji mchango. Wakamwambia aache ujinga lazima wachange!!

Na ninavyowajua wale rafiki zake wasingekanyaga kwenye harusi kama angekaidi
 
Ameongeza chumvi sana, si uongo. Mi nilidhani Tanzania ya leo, ina vijiji vichache sana. Kiukweli nikikutana na mtu under 30 anaongelea kuzaliwa kijijini, nashangaa flani hivi.
Mkuu inaonyesha huishi tanzania. Bado Nchi hii ina vijiji vingi sana, na kuna idadi kubwa ya Watu huko kuliko wanaoshi mjini.

Kwa mfano ukitoka nje ya Dar kama kilometa 30from city centre kuelekea upande wowote utakutana na Vijiji
 
Back
Top Bottom