Kuoa si jambo dogo kwa mwanaume

Kuoa si jambo dogo kwa mwanaume

Financial Freedom

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2016
Posts
1,250
Reaction score
2,314
Wasalaam wakuuu,

Aisee huyu mwanamke kanizalia mtoto mzuri tu wa kike ana miezi miwili tu ila nikifikiria ishu ya kuoa napata wasiwasi sana maana moyo wangu haumwamini mwanamke yeyote hata kidogo.Naogopa ndoa 100% maana sipendi kuoa zaidi ya mara moja.

Tuwe wachumba tu hata kwa miaka 7 hata kama tukizaa watoto wengine kwenye uchumba, hela mimi nitakupa ila sio ndoa kwa haraka hivi. Siwezi nisamehe!
 
Acha ubinafsi usijfikirie wewe tu mfikirie mtoto, unafikiri yeye hapendi kuwa na Wazazi wenye ndoa ? Unafikiri mtoto hatopenda kuongelea kuhusu Wazazi wake ? Au wewe hauna Wazazi wenye Ndoa? Kwa maoni yangu kama mtu hawezi kuishi na mtu basi asilete kiumbe Dunia hii, tuache ubinafsi, kama humwamini Mwanamke kiasi cha kumuoa usizae naye pia.
 
Acha ubinafsi usijfikirie wewe tu mfikirie mtoto, unafikiri yeye hapendi kuwa na Wazazi wenye ndoa? Kwa maoni yangu kama mtu hawezi kuishi na mtu basi asilete kiumbe Dunia hii, tuach ubinafsi, kama humwamini Mwanamke kiasi cha kumuoa usizae naye pia.
Mkuu kuzaa na mtu inatokea tu bila kupanga muda mwingine
 
Mkuu kuzaa na mtu inatokea tu bila kupanga muda mwingine

Dunia ya leo unawezaje kupata mtoto bila ya kupanga ? I mean, nyenzo zote hizo, isitoshe inaonekana basi pia labda hata huyo demu hamna mawasiliano mazuri sana kwani kwa kawaida mademu hawawezi kupata mimba kama hawajapanga, namaanisha mademu wa leo, ...
 
Sijui ulipatwa na jambo gani ambalo limekufanya uwemuoga kiasi hicho.

Lakini hilo unalodhani unaliepuka kwa sasa ndio linanafasi kubwa kutokea kuliko ungemuoa, kwa sababu kwa sasa huwezi kumzuia kuwa na mtu mwingine ambaye atakuwatayari kumuoa, kwa kuwa si mke wako na wala hauko tayari kumuoa.

Aliyeolewa atakuwa mke wa mtu, hata kama hatokuwa mwaminifu, na asiyeolewa anaweza kuwa wa yeyote yule.
 
Wadada wakiamua wenyewe kuzaa huwezi kumzuia,mnamaliza tendo mnakubaliana atakunywa P2 hanywi anadai amesahau ndo basi anazaa.Alivyoniambia hivyo alinikata moto napo abortion hataki anasema kwanin atoe? Sio mwanafunzi
 
hapo ulipo ushaoa, huna cheti tu na pete kidoleni.
Under implied Condition umeshaoa
Hahah hapana sijaoa,kuoa naogopa sana mbele ya watu afu siku mambo yameharibika nitawaambia nin watu.

Mimi sio malaika kuachana ni kitu kidogo nitawaambia nin watu
 
Sijui ulipatwa na jambo gani ambalo limekufanya uwemuoga kiasi hicho.

Lakini hilo unalodhani unaliepuka kwa sasa ndio linanafasi kubwa kutokea kuliko ungemuoa, kwa sababu kwa sasa huwezi kumzuia kuwa na mtu mwingine ambaye atakuwatayari kumuoa, kwa kuwa si mke wako na wala hauko tayari kumuoa.

Aliyeolewa atakuwa mke wa mtu, hata kama hatokuwa mwaminifu, na asiyeolewa anaweza kuwa wa yeyote yule.
Ni yale yale tu,wake za watu sio waaminifu hivyo hivyo ambao hawajaolewa nao sio waaminifu
 
Back
Top Bottom