TAI DUME
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 10,745
- 29,219
1. Kama mpenzi wangu kila ijumaa anakuja kwangu na anasipendi nae mpaka jumapili usiku, nioe ili iweje?
2. Kama kila nguo zangu zikichafuka au nyumba ikihitaji usafi sikosi mwanamke wa kunisaidie, nioe ili iweje?
3. Kama mwanamke niliyempa mimba yuko tayari kuzaa, nioe ili iweje?
4. Kama kila nikihitaji tendo la ngono (sio tendo la ndoa) nalipata kwa wakati, nioe ili iweje?
5. Kama kila nikihitaji ushauri au kuliwazwa na mwanamke napata, nioe ili iweje?
Bado nipo nipo sana
2. Kama kila nguo zangu zikichafuka au nyumba ikihitaji usafi sikosi mwanamke wa kunisaidie, nioe ili iweje?
3. Kama mwanamke niliyempa mimba yuko tayari kuzaa, nioe ili iweje?
4. Kama kila nikihitaji tendo la ngono (sio tendo la ndoa) nalipata kwa wakati, nioe ili iweje?
5. Kama kila nikihitaji ushauri au kuliwazwa na mwanamke napata, nioe ili iweje?
Bado nipo nipo sana
Mkuu kawoli ndoa ni taasisi ambayo ni muhimu sana katika jamii na bila kwayo mambo mengi yangeyumba kwenye kiwango cha jamii kwa ujumla wake ikiwemo kuiongezea mzigo serikali. Kwa nini mtu anaoa inategemea na mtazamo, kuwa wengine anaoa kwa sababu za imani yake, kuna watu wanaoa kwa ajili tu jamii iko hivyo na kadhalika, ntajaribu kukupa sababu za jumla ambazo nahisi zitakuwa zinagusa wengi bila kujali mitazamo binafsi.
Dhamira(commitment)
Tofauti na kimada, kwenye ndoa watu wanakuwa wameungana kupitia mchakato bila mategemeo ya kuachana japo huwa yanajitokeza kwa baadhi. Ni rahisi kupanga maisha yenu ya mbeleni ikiwemo kujiendeleza kiuchumi na mke tofauti na kimada ambae mkataba wenu unaweza kuwa wa siku pekee na kesho yuko na mwingine, utamtafuta tena ukiwa na haja nae.
Mshirika wako uzeeni
Kadri umri unavyoenda ndivyo utaona umuhimu wa mshirika wako wako wa maisha, watu wengi ikiwemo vimada wako hawapendelei maisha ya kuruka miaka yote hivyo kadri siku zinavyosonga utaona wanavyopungua kutokana na kuwa na majukumu katika ndoa zao au maisha yao(hata kama ndoa haijapita).
Watoto
Japo umesema kuna mtu yuko tayari kukuzalia mtoto lakini sidhani kama utaweza kumlea kwa staili ya weekend na atakuwa mtoto mwenye malezi ya mzazi mmoja na kwa aina ya maisha yako uliyoyachagua sidhani kama utakuwa wewe, anaweza kulelewa na mama kimada ambao tunawajua staili yao ya maisha, tena usipoangalia utakuwa unashindishwa ustawi wa jamii kudaiwa fedha za mtoto, atakuwa kitega uchumi kwa mama(kimada) kuendeshea maisha yake. Maisha, malezi na tabia ya mtoto itavyokua malizia mwenyewe.
Tendo salama
Ukilinganisha maisha ya vimada na maisha ya ndoa, bado kwenye ndoa ngono ni salama zaidi na hatuwezi kuhukumu kwa baadhi ya matukio hasi yaliyopo kwenye baadhi ya ndoa kwa watu kusaliti ndoa zao. Maisha ya vimada yamejengwa juu ya dhana ya usaliti hivyo mtandao wa kusambaza magonjwa ya zinaa kwao kawaida na ngumu kutokea uaminifu baina yenu.
Faida ya kiuchumi
Wewe unakaa kwako na kimada anakaa kwake na kila mtu ana maisha yake, kila mtu anaingia gharama ambazo mngekua pamoja labda mngeweza kushea au kuziepuka. Kodi ya nyumba, gharama za take away, kuendesha uhusiano wa kimada ambao ni tofauti kidogo na mke na gharama nyingi nyinginezo. Inawezekana sana ukawa unaendesha gharama za maisha yako na kimada wako kitu ambacho ni tofauti sana ingekua mke.
Heshima na kukubalika kwenye jamii
Kadri umri unavyokatika watu wataanza kukushangaa kwanini huoi na kujituliza kwenye ndoa badala yake unaendesha maisha ya uvimada, kama una wazazi naamini utawasononesha, rika la watu wako mtaani linaweza likawa tofauti na ulilopaswa kuwepo. Maisha yenye furaha na upendo, kuwepo mtu wa kukusikiliza kila siku tofauti na kimada wa weekend, kuwepo mtu wa kutatua nae matatizo kwa hali na mali(scenario chache za watu kukimbia haziwezi kujumuisha vinginevyo) na mengineyo mengi.