Kuoa binti mwenye mtoto

Kuoa binti mwenye mtoto

Habari wana jukwaa naomba mnishauri,

Nilitokea kumpenda sana binti mmoja wakati niko A level nilikuwa nasoma nae darasa moja ila michepuo tofauti mimi nilikuwa PCB na yeye alikuwa CBG Kibaya zaidi sikuwahi kumtamkia kuwa nampenda nilikuwa naumia moyoni tu.

Baada ya matokeo kutoka(2010) alipata failure na mimi nilipata div iii yenye Principal pass moja nikaenda kusoma diploma ya mifugo(LITI, 2010-2012).

Wakati nikiwa chuoni bado moyo wangu ulikuwa unamfikiria sana huyu binti, mnamo mwezi 11/2011 nilitafuta namba yake kutoka kwa mmoja ya classmate wangu.

Ndipo nilipojipiga kifua na kumweleza hisia zangu kwake na kudai kuwa mbona muda wote huo sijawahi kumwambia nikamweleza kwa nini. Kuanzia hapo ikawa tunawasiliana hadi nilivyorudi chuoni mwezi wa 5/2012.

Nikampigia simu tuonane na kweli alikuja (frankly speaking i did with her) Bila kusahau nilishawahi kumuuliza kama ashawahi kuwa na mtu akanambia ndio lakini wameachana mda mrefu hakuniambia zaidi ya hivyo.

So moja ktk siku nilimwita aje cafe tupate juice alikuja na mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kuelekea miwili nilimuuliza ni wanani akadai ni ndugu yake yuko Zanzibar hatimae niligundua kuwa ni wake(shorten to save time).

Nilivo muuliza kwa nini alinificha akadai angenikimbiza mapema kama angeniambia (a lot ommited to save time) kimsingi binti ananipenda ajabu na nilishamuahidi kumuoa nikipata kazi na sasa nimeajiriwa na wizara ya mifugo na pia ni mwanafunzi wa veterinary Medicine year 1.

Kwa sasa binti anataka nimuoe kwani nimeshapata kazi lakini nagwaya kuwa ni sawa kwa umri wangu kuanza na binti mwenye mtoto? Zingatia binti nampenda sana kwani alivyo huwezi amini kuwa ana mtoto na yeye pia ananipenda.

Ushauri tafadhali kwani lengo langu mwaka huu usiishe nioe kama kuna mtu atataka maelezo zaidi ili anishauri barabara nitampatia.

Lazima akugande unazani kupata mume wakati una mtoto jambo dogo hao masingle tu wasio na watoto nanga inapaa, anyway kama unampenda huyo mtoto isiwe sababu ya wewe kushindwa kuwa nae wazungu wanaema true love conquer it all
 
Daa kijana mdogo ndo unaanza maisha uoe mama mwenye mtoto!!!!!!!!!!!!!!!!! Mhh mie siwezi labda kama na mie ningekuwa nishazaa kwanza....kuna maswali ya kujiuliza kabla ya kuamua:
1. Huyo aliyempa mimba asimuoe?
2. Je umejiaandaaje kulea mtoto wa mwanaume mwenzio maana usiangalie tuu eti unampenda sana huyo binti,, Je na mtoto wake unampenda kweli na uko tayari kumlea kama mwanao wa damu?
3. Je umejiandaaje kukabiliana na vikwazo kutoka kwa ndugu na marafiki kuhusiana na uamuzi wako maana ni watu wachache wenye uamuzi kama wako?

Baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha lakini hebu tafakari kwa kina kabla ya kufanya uamuzi ili usije kutenda dhambi ya ubaguzi kwa mtoto huyo.
 
Asprin atakuambia mahawala hawaachani, swala la kurudiana au kukumbushia mtoto sio sababu. Tena kama alimkataa akiwa mjamzito, inajenga chuki zaidi ya upendo. Hofu yako ndio hasara yako, toa mawazo negative na mtaishi happily after.

Halafu naona huyu hajampenda vya kutosha ndio maana anauliza mawazo ya watu. Live your life, ili usitafute wa kumlaumu pala yanapokushinda.
Kaunga, Hilo la kuoa mtu aliyezaa nawaachia wanaume wengine. Maisha ya ndoa yana stress nyingi, sitaki kuongeza hii ya kujitakia. I've seen it through my relatives. Najua wapo wanaojiheshim lakini sio rahisi kujua, wengine wanaachana huku wakipendana...
 
Last edited by a moderator:
Kuoa binti mwenye mtoto sio dhambi......mnapendana mmekubaliana kuwa na taarifa sahihi kutoka kwa mama kuhusu mtoto
Ila akumbuke mtoto akikua lazima amdunde baba wa kufikia. Akiwa mdogo hakuna shida, shida zinaanza anapoanza kujitegemea hasa akiwa wa kiume
 
mtoto sio sababu yakukufanya usikíe lengo lako.
 
Sioni tatizo kama mnapendana mtoto si ishu. Jamii imezoea mfumo dume ndio maana unapata taabu kuamua. kuna mama vichanga wengi tu sema viliishia kusikojulikana sasa usidanganywe na muonekano wa mtu kama watu wangechunguzwa kungepatikana na idadi kadhaa ya wakaka na wadada wasiokolifai kuitwa hawana watoto. Wengine hawana kwa sababu siku hiyo haikua siku ya hatari na wengine hawana kwasababu walicholopoa.

thnx kwa kutetea sie tuliozaa na tukaolewa mi natoa mfano wangu mwenyewe firs born wangu na babake hatuko pamoja kila mtu kivyake na namheshimu sana mme wangu mana kwa ujasiri wake ameweza kunikubali na akanioa na tuna amani tu suala si kurudiana na mwenzi wako unaeza oa asiye na mtoto akakubambikia pia by the way mbona wanaume mnazaa na mnaoa wasio na watoto acheni ubinfsi au hapa jf hv hamna watu waliozaliwa half siblings humu?au ndo mbwembwe tu!
 
afu wanaume mnakomaa na point ya ma ex kurudiana au ndo zenu hzo?
 
Kaunga, Hilo la kuoa mtu aliyezaa nawaachia wanaume wengine. Maisha ya ndoa yana stress nyingi, sitaki kuongeza hii ya kujitakia. I've seen it through my relatives. Najua wapo wanaojiheshim lakini sio rahisi kujua, wengine wanaachana huku wakipendana...

Unauhakika gani kama yule ulie/utakae oa na hana mtoto kama kaachana na x-wake kikweli kweli! Suala la kuonjeshana na ma-x, ni tabia ya mtu, haijalishi kama alikuwa na mtoto au la wakati wa kuolewa.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi huwa naamini
1. mwanamke aliyepelekwa leba na mwanamme kamwe hamsahau huyo mwanaume no matter wat happens esp mimba ya kwanza
2. Mtoto ni kiunganishi baina ya wazazi. Always watakuwa na mawasiliano no matter wat happens.
3. Huwa naamini kujifungua its a live or die thing. its either mwanamke afe mtoto abaki au mtoto afe mwanamke abaki au wafe wote au wabaki wote. So mwanamke kuamua kumzalia mwanaume mtoto huwa ni upendo wa ajabu kiasi cha kuamua kurisk maisha yake kwa yule mwanaume.

Ni hayo tu. Akili za kuambiwa changanya na zako
 
yaani mngejua...! msingesema yote hayo!
 
Kama mnapendana hakuna tatizo kijana we oa tu, cos ishu ya kid itakuwa ni mwendelezo tu pia nkishaingia kene ndoa mtapata wengine.
 
yaani mngejua...! msingesema yote hayo!

Nawashangaa sana.Mwanamke mwenye akili timamu awezi kutembea na mtu alomzalisha na kumuacha maana hicho kitendo ni cha kinyanyasaji hasa kwa mwanaume mwenye uwezo wa kulea mtoto.

Pia jiulize kama issue ni mimba wangapi wanaolewa na walishatoa za kutosha?

Mwisho kabisa jiulize kwa maisha ya sasa mabinti wana hamia kwa wanaume ata miaka miwili bila ndoa na baadae wanazinguana anakuja kuolewa na kijana mwingine na habari zinakua chin ya kapet japokua binti anakua hana mtoto na x.sasa we ukimpata huyo je utasemaje?
 
Habari wana jukwaa naomba mnishauri,

Nilitokea kumpenda sana binti mmoja wakati niko A level nilikuwa nasoma nae darasa moja ila michepuo tofauti mimi nilikuwa PCB na yeye alikuwa CBG Kibaya zaidi sikuwahi kumtamkia kuwa nampenda nilikuwa naumia moyoni tu.

Baada ya matokeo kutoka(2010) alipata failure na mimi nilipata div iii yenye Principal pass moja nikaenda kusoma diploma ya mifugo(LITI, 2010-2012).

Wakati nikiwa chuoni bado moyo wangu ulikuwa unamfikiria sana huyu binti, mnamo mwezi 11/2011 nilitafuta namba yake kutoka kwa mmoja ya classmate wangu.

Ndipo nilipojipiga kifua na kumweleza hisia zangu kwake na kudai kuwa mbona muda wote huo sijawahi kumwambia nikamweleza kwa nini. Kuanzia hapo ikawa tunawasiliana hadi nilivyorudi chuoni mwezi wa 5/2012.

Nikampigia simu tuonane na kweli alikuja (frankly speaking i did with her) Bila kusahau nilishawahi kumuuliza kama ashawahi kuwa na mtu akanambia ndio lakini wameachana mda mrefu hakuniambia zaidi ya hivyo.

So moja ktk siku nilimwita aje cafe tupate juice alikuja na mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kuelekea miwili nilimuuliza ni wanani akadai ni ndugu yake yuko Zanzibar hatimae niligundua kuwa ni wake(shorten to save time).

Nilivo muuliza kwa nini alinificha akadai angenikimbiza mapema kama angeniambia (a lot ommited to save time) kimsingi binti ananipenda ajabu na nilishamuahidi kumuoa nikipata kazi na sasa nimeajiriwa na wizara ya mifugo na pia ni mwanafunzi wa veterinary Medicine year 1.

Kwa sasa binti anataka nimuoe kwani nimeshapata kazi lakini nagwaya kuwa ni sawa kwa umri wangu kuanza na binti mwenye mtoto? Zingatia binti nampenda sana kwani alivyo huwezi amini kuwa ana mtoto na yeye pia ananipenda.

Ushauri tafadhali kwani lengo langu mwaka huu usiishe nioe kama kuna mtu atataka maelezo zaidi ili anishauri barabara nitampatia.

daah mkuu historia yako kimasomo inafanana sana na ya kwangu, anyway kaka kama ana sifa za kua mke wewe muoe tu, huyo mtoto hawezi kuwa kikwazo. go for your heart
 
Nawashangaa sana.Mwanamke mwenye akili timamu awezi kutembea na mtu alomzalisha na kumuacha maana hicho kitendo ni cha kinyanyasaji hasa kwa mwanaume mwenye uwezo wa kulea mtoto.

Pia jiulize kama issue ni mimba wangapi wanaolewa na walishatoa za kutosha?

Mwisho kabisa jiulize kwa maisha ya sasa mabinti wana hamia kwa wanaume ata miaka miwili bila ndoa na baadae wanazinguana anakuja kuolewa na kijana mwingine na habari zinakua chin ya kapet japokua binti anakua hana mtoto na x.sasa we ukimpata huyo je utasemaje?

umeonaah eeh!thnx in advance kwa hoja nzito mpaka nimelia!
 
hata mie nimeoa mke ambaye nilikuta tayali ameshazaa na maisha yanaenda poa tu so go for her
 
ungekuwa unampenda hata angekuwa na mjukuu ungemuoa tu. upendo wako unaleta mashaka!
 
Back
Top Bottom