kwa jamii kubwa ni fedheha na wewe unahisi hivyo ndo maana umekuja kuuliza. Kama mnapendana (kupendana tu haitoshi) na mnaendana vya kutosha kuoana, mtoto ni mojawapo ya swala muhimu la kujadili kabla hamjaingia kwenye ndoa. Kufunga ndoa na mwenzi mwenye mtoto kunaweza kusiwe na shida endapo kutakuwa na mipaka ya mahusiano kati ya mwenzi na mzazi mwenzie. Ni lazima mkubaliane protokali toka mwanzo na mwenzi mwenye mtoto ahakikishe anazingatia.
Umesema baba mwenye mtoto hajihusishi kabisa na huyu mtoto. Kama hajihusishi huwa ni rahisi, lakini utashangaa akiskia mzazi mwenzie ana mchumba anajitokeza na kuanza kuleta fujo za hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kujaribu kumsihi mama mtoto amrudie yeye, na mama mtoto akikataa basi atatishia kumtaka mwanae. Hapa linakuwa ni jukumu la mama mtoto kuonyesha msimamo na kumuwekea mipaka huyu mwanaume. Huyo mwanamke akionyesha kuyumba hapa basi itakula kwako.
Sasa hili linalofuata halihusiani na ubaya au wema wa kuoa mwanamke mwenye mtoto. Linahusu huo uamuzi wako wa kuoa. Ni nini hasa kinachokufanya utuambie lengo lako ni huu mwaka usiishe uoe? Ni masharti ya mganga au? Kijana hakuna umri sahihi au mbovu wa kuoa. Kuna wakati sahihi au mbovu wa kuoa. Huyo msichana unayetaka kumuoa kabla huu mwaka haujaisha unamfahamu kiasi gani zaidi ya ule upendo wa sekondari? Ni lini mmekuwa marafiki kiasi cha kuona sasa huu urafiki wetu umeiva kiasi cha kuashiria kuingia hatua nyingine? Binti huenda anaharakisha umuoe kwa kuwa anaujua unyanyapaa wa hii jamii. Anahisi akikukosa wewe uliyeonyesha nia anajua atasubiri sana kuolewa na mtu mwingine. Wewe je una haraka gani? Kwamba utamkosa huyu?
Halafu ndo kwanza umeanza kazi, uko mwaka wa kwanza chuo..................in short slow down bro. Iwe unataka kumuoa huyu au unataka tu mwaka usiishe hujaoa, slow down. Bado miezi mitano mwaka uishe. Ni michache sana kufanya maamuzi na maandalizi. NI MTAZAMO TU