Kunyweni kahawa ina faida lukuki

Kunyweni kahawa ina faida lukuki

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,297
pic+kahawa.jpg

Dar es Salaam. Dhana potofu kuwa unywaji kahawa unaleta shinikizo la damu umesababisha kinywaji hicho kutumika kwa asilimia 10 tu nchini.

Akizungumza leo Jumapili, Julai 9 katika Banda la Bodi ya Kahawa Tanzania lililopo katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya 41 (Sabasaba), Ofisa Uhamasishaji wa bodi hiyo, Frank Mlay amesema dhana hiyo imesababisha zao hilo likose thamani hapa nchini.

Badala yake, Mlay amesema kinywaji cha zao hilo kina faida nyingi za kiafya ikiwa ni pamoja na kuzuia saratani, ugonjwa wa kutetemeka (Parkinson Disease) na maumivu ya ngozi.

Amesema asilimia 90 ya kahawa inasafirishwa nje ya nchi na asilimia 10 pekee ndiyo inayotumika hapa nchini.

Meneja masoko na ubora wa bodi hiyo, Rogalus Meela amesema kama Watanzania wataitumia kahawa ipasavyo wataiongezea mnyororo wa thamani ambapo akija mnunuzi kutoka nje atalazimika kuinunua kwa bei ya juu.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa hisani ya joseverest

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wazungu wanakunywa kahawa strong sana na hawaweki sukari lakini hawana presha , wala ugonjwa wowote ule. Kunyweni kahawa acheni kudanganywa tena inatibu kibofu cha mkojo kwa wale wenye matatizo hayo.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Uko sahihi

Chief Economist
 
Coffee containing caffeine can cause insomnia, nervousness and restlessness, stomach upset, nausea and vomiting, increased heart and breathing rate, and other side effects. Consuming large amounts of coffee might also cause headache, anxiety, agitation, ringing in the ears, and irregular heartbeats.
 
Kwani haina cafein hiyo kahawa?sasa ifanye kama maji uone utamu wake

Sent from my SM-G900F using JamiiForums mobile app
hata maji ukinywa mengi yanamadhara
 
Wazungu wanakunywa kahawa strong sana na hawaweki sukari lakini hawana presha , wala ugonjwa wowote ule. Kunyweni kahawa acheni kudanganywa tena inatibu kibofu cha mkojo kwa wale wenye matatizo hayo.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
Tuacheni ujinga jamani, kahawa ina madhara mengi kuliko faida. Kahawa,Pombe,Sigara,Maziwa ya Ng'ombe just to mention but a few.
 
Sitakunywa kahawa hapa dunian labda mbinguni...
Madhara yake ni makubwa sana..mwenyewe ni shahidi

Sent from my SM-G925F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom