Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,686
- 46,373
Kuna watu wengi mtandaoni hasa Wakristo na kutoka chama cha CHADEMA hupendelea sana kunukuu maandiko ya kidini kwa maana ya Biblia katika kuwasilisha hoja na hisia zao kuhusu matukio mbalimbali yanayohusiana na harakati za kisiasa zinazoendelea nchini kila siku.
Kuna huwa kipi kinaongezeka katika harakati za kisiasa kwa kutumia maandiko ya kidini yanayowalenga watawala na watu wenye dola.Watawala wengine wanaoandikiwa na kulengwa na hizo nukuu iwe ni kutoka kwenye Biblia au Quran hawaamini hata hivyo vitabu au kimojawapo na wanavichukulia ni vitabu kama vilivyo vingine vyovyote vilivyopo duniani.
Ifike hatua upeo wa kisiasa uwe juu kufahamu dini ina mchango mdogo sana na finyu katika kubadili kwa njia chanya hali za kisiasa katika nchi yoyote, zaidi sana huchangia utengano badala ya utangamano. Ushahidi wa kihistoria unathibitisha hilo.