Kunuka mdomo kunavyopunguza ladha ya mapenzi

Kunuka mdomo kunavyopunguza ladha ya mapenzi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,087
Japo ni ugonjwa na unatibika lakini huleta karaha mno kwa wapenzi na hii husababisha watu kutojiamini,

Kuna mahusiano yamevunjika kutokana na hili jambo ,mpenzi anataka akuchum lakini akikukaribia tu anakutana na harufu kali anajikuta anakwepesha mdomo na hamu yote inaisha inakera kwakweli.

Kama una tatizo hili ni vema ukawahi tiba maana hata kwa watu wengine utakosa raha na amani utataka kuongea kitu lakini ukikumbuka mdomo wako ghafla unasita lakini vilevile wengine wakikuona tu unataka kuongea wanageuza nyuso zao na wengine kuziba pua.

Unabaki mkiwa na mpweke inaumiza sana.
 
Sio kwenye mapenzi tu hata mkiwa kwenye kikao kuna watu wakiongea tu mnatamni mtoke nje, chumba chote kinaenea harufu mbaya.
 
Japo ni ugonjwa na unatibika lakini huleta karaha mno kwa wapenzi na hii husababisha watu kutojiamini
Kuna mahusiano yamevunjika kutokana na hili jambo ,mpenzi anataka akuchum lakini akikukaribia tu anakutana na harufu kali anajikuta anakwepesha mdomo na hamu yote inaisha inakera kwakweli
Kama una tatizo hili ni vema ukawahi tiba maana hata kwa watu wengine utakosa raha na amani utataka kuongea kitu lakini ukikumbuka mdomo wako ghafla unasita lakini vilevile wengine wakikuona tu unataka kuongea wanageuza nyuso zao na wengine kuziba pua
Unabaki mkiwa na mpweke inaumiza sana

Pole kwa kumpata mwenye hali hiyo..............
 
Kuna wengine wanapiga mswaki vizuri tu na meno yao mazurii, meupee yaani yanatunzwa vizuri sana!! Ila ole wako afungue huo mdomo utaomba pooo...!!!

Ni ugonjwa, sometimes unatokea kwenye mapafu au hata koo!! Ni kukimbiliakwa wataalam basi
 
sasa jaman lazima mjue kuwa watu wa namna hii wanahitaji msaada wetu na si kuwasema pembeni!
Mi niko na mpenzi ila hapo mwanzo alitema vibaya.....sio kwamba wanapenda ila wengi wanakuwa hawajijui kama wanaharufu mbaya ya mdomo, ni sawa na mtu aliyeko chooni huwa anahisi choo hakinuk.........kinachotakiwa ni kuwa wazi kwake na kumpa mbinu za kulitokomeza hilo tatizo!
 
vizuri majigo ila kuna watu wengine wamejitakia unakuta demu katoka kimanzichana bondeni katembea kapanda daladala kashuka kituoni katembea mpaka geto kwako akifika tu unajifanya kuzama chumvini ...!!?
 
amini husiamini wengi wetu tuna hili tatizo bila kujijua na bado tunawateta wenzetu......hebu jaribu njia hii ili kujua mdomo wako ni salama, lamba kwa ulimi upande wa pili wa kiganja chako(upande mweusi unaokuwa na vinyweleo) alafu nusa hiyo sehemu uone kama hapanuki, kama pananuka ujue nawe umo!!!
 
vizuri majigo ila kuna watu wengine wamejitakia unakuta demu katoka kimanzichana bondeni katembea kapanda daladala kashuka kituoni katembea mpaka geto kwako akifika tu unajifanya kuzama chumvini ...!!?

hahahahah ila uzamiaji kiholela nao unachangia vijana wengi wa sasa kuwa na fangasi ya mdomo!
 
hahahahah ila uzamiaji kiholela nao unachangia vijana wengi wa sasa kuwa na fangasi ya mdomo!

Mambo ya kuiga na pia ubahili wa kununua colgate au kuwa mvivu wa kupiga mswaki vizuri. Hiyo ya kuzama chumvini nina mfano live kabisa jamaa alihangaika miezi 5 anasaka tiba ,mdogo ulikuwa unatema kama choo cha city kisa chumvini
 
mswaki wanapiga , tena mara tatu kwa siku ila wengi hatujui mbinu za upigaji mswaki....wengi tunasugua meno na si kinywa!!

Ni kweli kabisa pia kutumia dawa na miswaki feki
 
Back
Top Bottom