Miaka ya zamani kuna kunguru mmoja alipata ajali akavunjika mbawa akalegea na hata ukimsogelea akawa ajitahidi kukimbia lakini ashindwa kuruka.
Wasamaria wema wakamchukua hadi nyumbani kwao na wakampa huduma ya kwanza kisha wakampatia vyakula tofautitofauti.
Baadae yule kunguru akapona lile jeraha la mbavuni na akaanza kurukaruka nje kwenye kiwambaza.
Siku moja akaruka akapotea na asirudi lakini baadae siku kama mbili hivi akarudi mlangoni na akawa akipiga kelele kwaaakwaa na msamaria mwema akatoka na kumkuta pale nje.
Lakini yule kunguru kumbe alikuja tu kusalimia na kuonyesha atambua yale mazuri alofanyiwa na tangia pale hiyo ikawa ni utaratibu wake yule kunguru na hadi leo lazima atue kidogo nje ya nyumba ya aliemuokoa.