Kuna watu wanamiliki majini bila kificho na kuyatumia kwenye tiba sambamba na visomo vya Quran takatifu. Huu sio ushirikina?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ushirikina sio kutumia uchawi pekee, hata unapomshirikisha Mwenyezi Mungu na majini huo nao ni ushirikina.

Mkasa huu niliweza kuushuhudia live kwa macho yangu 2019, Mgonjwa alipona maradhi yake lakini hadi leo najiuliza ilikuwa sahihi kwa Sheikh / Ustadh kuyatumia majini sambamba na kuitumia Quran takatifu ?

Tumefika nyumbani kwa Shehe na mgonjwa, haya anamwambia akae chini kwenye mkeka, ghafla Ushtadh anapandisha majini, anaanza kucheka kama mtu alierukwa na akili eh heh ehe (kama ni mara yako ya kwanza utaogopa) anaanza kubeua na kucheua, kwa macho legevu mithiri ya kulewa anamtazama mgonjwa kwa makini katika namna ya kumchunguza. Mke wake yupo pembeni wanaangaliana na Ustadh machoni, hujui kinachoendelea kumbe kuna mawasiliano hapo, mke wake ndie anamwambia mgonjwa kwa lugha ya kibinadamu "kasema ufungue kinywa", "kasema usogee karibu usiogope", n.k. Ustadh anamaliza upelelezi, anazinduka akiwa amechoka, jasho linamtoka, anahema kama kakimbizwa umbali mrefu.

Shehe anaanza kuongea na mke wake lugha ambayo nadhani ni ya kikabila ama kiarabu, Shehe anamwambia mgonjwa afungue kinywa amgeukie mke wake, mkewe ghafla ni kama anapitiwa na usingizi akiwa amekaa kumbe nae kashapandisha hapo, anamchunguza mgonjwa kwa dakika 3 hivi, ili kujirudi Ustadh anamwite binti mdogo nadhani ni house girl anakuja kumtikisa anavyojua yeye ndio anazinduka.

baada ya hapo Shehe anaanza kusoma vifungu vya quran kama nusu saa hivi kwa sauti kubwa. Tiba zingine za ziada za mizizi, asali na mabaki ya miti yaliyosagwa ya kuogea mgonjwa anapewa awe anatumia, Shehe anamsisitiza mgonjwa awe anasali kila akiamka na kila akienda kulala, wawili tuliemsindikiza mgonjwa tunapewa jukumu la kuhakikisha anasali na kutumia hizo dawa.

Kwa siku 3 mfululizo mgonjwa tunampeleka mara mbili kusomewa visomo huku akiendelea na dozi.

Mgonjwa anaapona ila bado swali kuu linabaki kwamba kwanini majini hutumika ?
 
Dini yetu inaruhusu kujilinda na kujihami Kwa njia yote ile,self difence hiyo,huo ni ulinzi
Una akili sana...sana...sana...

Sasa nikae mazingira hatarishi dhidi ya familia yangu...nagundua kuwa na jini la ulinzi ni bora.....nisilitafute?!!

Ni nini tofauti ya kutembea na BASTOLA na kuwa na hiyo mijini ?!!!

Watu akili zao sijui zinakuwepo "mk...ni"?!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nina
jirani yangu mmoja Alikuwa Imamu WA MSIKITI (.....) mkubwa MMOJA Jini Dar es salaam.

Aliamua Kuokoka na kupokea Jina la Yesu kristo WA NAZARETH.
Baada ya Kuokoka akaamua kusoma sana BIBLIA na kunielewa kwa marefu na mapana yake.

Akaamua aanzishe KANISA kubwa Sana Jijini Dar es salaam. Anasema Jina la YESU HALIWEZI kuandika kwenye Quran kwasababu jina la Yesu ni ADUI WA Majini na Mapepo na MASHETANI.

Anasema hata alivuliyokuwa muislamu , Balaza la Ulamaa wanajua yote NGUVU ya jina la Yesu ndio maana wanaogopa sana.

MUNGU AMBARIKI SANA MTUMISHI WAKE.
 
Back
Top Bottom