Kuna watu wanamaisha magumu sana

Kuna watu wanamaisha magumu sana

Ni mwaka fulani nipita apo Dar, nikaamua nipite kwa mshikaji wangu wa kitambo tulisoma wote huko kanda ya ziwa.

Nilimtafuta akanambia yeye yupo kulagwa akanambia hana ela ya usafiri kunifata nilipo nikaona isiwe shida nikamfuata.

Nilipofika asee sikuamini maisha yamemponda sana ile sana nikamuuliza vitu mzee akanambia kama ninavomuona nilimhurumia sana nikampatia 50000 ya kumsaidiasaidia.

Tukaenda adi alipopanga tulipofika akanambia ndio hapa binapoishi asee nje kuchafu choo hakuna, bafu hakuna, maji hakuna, umeme hakuna nikaamua nimuulize unaishije sasa ndugu yangu akasema ni kawaida ameshazoea maisha hayo.

Tukaongozana kuelekea ndani mlango ulikuwa umefungwa tulipokaribia mlangoni kwake akainama akaokota jiwe nikamuuliza vipi tena mbona jiwe tena akacheka akasema hili sio jiwe ni funguo yangu mara akapiga jiwe juu ya kufuri, kufuri likafunguka nilisitajabu sana.

Alipofungua mlango tu ivi asee chumba hakina sakafu nzuri madirisha hakuna nilipowasha kitochi cha simu hakun godoro analala kwenye mkeka tu

Chumba kichafu sana harufu kali sana ya nguo chafu vyombo kama vinamiaka havijaona maji.
nilishindwa kukaa pale nilimpa pesa kidogo nikaenda zangu kulala lodge

Dar anamiaka karibia kumi lakini hata godoro hana
FUNZO,UNAPOPATA MAISHA MAZURI MSHUKURU MUNGU SANA MAANA KUNA WATU WANAISHI KAMA WANYAMA .
Mtoto aliyekulia masaki na Oysterbay na anaishi kwa wazazi wake anaweza kua hii ni hadithi ya vichekesho
 
Endelea ....
Huyo rafiki angu alikuwa akifanyakazi za saidia fundi kubeba zege, kuchimba mitaro, gardening, kubeba mawe na kazi nyingine kibao ila chakushangaza hata nguo zake ni mbovu hanunui nguo mpya ni zilezile tu.

Nilijiuliza shida labda itakuwa kodi lkn nikitathimini anapoishi kodi haivuki 20000 kwa mwezi.
nilihitaji kumuuliza pesa anapeleka wapi lkn nikaingiwa na wazo nikifny hivyo itaonekn km namchunguza ikabidi niache ila nakaamua nitumie njia nyingine.

Kuna siku nilimuomba aje tuonane pahala nikamwambia naomba niazime simu yako kidogo rfk angu maana yangu imezima akanipatia sasa nikaanza kupekuwa asee nilikutana na majina ya ajabu sana mara Aisha utamu , Mshangazi, My Heart, lingine Wife mbeya asee moja kwa moja nikajua pesa anawapa wanawake na kwao hua hatumii pesa kabisa.

Hio siku ilipita siku nyingine majira ya jioni bado nilikuwa nae tunapiga story za hapa na pale mara simu yake ikaanza kuita nikamwambie mpokelee simu akapokea nilisikia sauti ya kike inafoka hata bila salamu et ivi wewe unajitoa akili nimekwambia nitumie pesa kama kweli unataka niwe mkeo nilisikitika sana.
hio sauti ya kike ikaendelea kufoka kama hutumi hio pesa mimi na wewe basi tuachane, jamaa yangu alianza kulia kama mtoto mdogo nilimuonea huruma sana lkn sikua na jinsi issue za mapenzi hua siziingilii.

Lkn nilimshauri kitu arudi om akajipange kama shida ni mwanamke basi aoe nikatoka zangu dar .

Angalizo,Unapoenda sehemu kijitafuta achana kabisa na mambo ya wanawake, Wanawake wanarudisha sana nyuma maendeleo ya kijana anaejitafuta mjini.
Achana na kina asha utamu, mara zuuuh , Kina cutee[emoji16] utaisha hawezi kukushauri chochote yeye ni leta tule akupe kipapa basi, unabeba zege afu ela unaipeleka huko ungemtumia ata maza nyumbani ungebarikiwa
We ni mnafiki, unapata wapi muda wa kuchunguza maisha ya mwanaume mwenzio kiasi hicho!? Basi ungemchunguza na kumshauri mwenyewe au kumsaidia lkn kwa ulichofanya kupost hapa ni kama ulimnafikia tu ili uonekane umefanikiwa na yeye hajapiga hatua. Kwa tabia hii hata wewe huna maisha yoyote ya maana, usingepata huo muda mchafu.
 
Jiji la Dar limechelewesha na kuua ndoto za vijana wengi sana.
Dar es Salaam kusema kweli kama huwezi kujiongeza na kutegemea mshahara na dili hewa lazima ndoto zife tu na kubakia kuwasema watu wa mkoani kuwa wana maisha magumu
Hakuna maisha magumu kama hapa Dar.
Watu wanajikakamua ila asilimia 85 ya Wakazi wa Dar wanakipato cha hand to mout,Saving na Investment ni kwa asilimia chache sana.
Working for paying bills
 
Jiwe TENA UNAWEZA kimbia ukazani ana taka kukuzuru MANA afya ya akili ishakua mtihani
 
Wewe hujakutana na watu wenye maisha magumu , sasa huyo hadi anauwezo wa kupanga ndio unamuona ana maisha magumu?
 
Arudi Kijiji akalime kama unaweza mtafutie kibarua ila usikutupuke. Usimuonee sana mtu huruma katika hali aliyonayo hujui alipotokea jipe muda kujua sababu za kuwa na hali hiyo.
 
Umenikumbusha jambo hapa, kuna jamaa angu mmoja ananikubali sana ila Sina uhakika...kuna kipindi maisha yalikuwa safi sana kwangu ila kwake yalikuwa magumu sana...basi nikawa namuita mara kwa mara anaangalia ninavyopambana...ikawa Kila siku anakuja....kama mwaka mmoja...baadae nikapata shida nikaamua kuhama mkoa....kumbe jamaa anaumia, nimeenda mkoa mwengine kujiangalizia afya miaka kadhaa baadae nikaanza kujitafuta upya ktk mkoa mwengine...naye kwenye mambo yao ya ajira akaajiriwa akapangwa mkoa wa mbele ya huu niliopo...akaanza kazi huko....siku akapata safari ya kikazi mkoa ambapo mm nipo..haloo....moja kwa moja kanitafuta nikamwambia nipo mbali na ulipofikia anasema hata kama gharama kubwa kiasi Gani nataka nikuone tu....nikastuka, anataka aone maisha ninayoishi kama ni yaleyale au?? Nikamuelekeza masaa mawili mwamba huyu....anasema alikosa amani alitamani anione ndugu yake....daa nikawaza kumbe jamaa anaupendo sana na Mimi hivi. Hadi kesho tunawasiliana....😛. Tupendane haloo, mm sikumzania jamaa...ila nikamwambia hata tembo akonde vipi hawezi kuwa kama sisimizi...akawa na Imani akaondoka amefarijikq🤣
 
Mleta mada hana huo wema, angekuwa mwema asingekuja kumuanika rafiki yake humu. Kama kaweza kuandika uzi basi jua mitaani ameshamchafua sana. Waogope ssna watu uliokuwa nao mtaani, uliosoma nao utotoni na uliomaliza nao chuoni.
kuna kaukweli kwenye msg yako
 
Back
Top Bottom