Kuna watu wanamaisha magumu sana

Kuna watu wanamaisha magumu sana

Ni mwaka fulani nipita apo Dar, nikaamua nipite kwa mshikaji wangu wa kitambo tulisoma wote huko kanda ya ziwa.

Nilimtafuta akanambia yeye yupo kulagwa akanambia hana ela ya usafiri kunifata nilipo nikaona isiwe shida nikamfuata.

Nilipofika asee sikuamini maisha yamemponda sana ile sana nikamuuliza vitu mzee akanambia kama ninavomuona nilimhurumia sana nikampatia 50000 ya kumsaidiasaidia.

Tukaenda adi alipopanga tulipofika akanambia ndio hapa binapoishi asee nje kuchafu choo hakuna, bafu hakuna, maji hakuna, umeme hakuna nikaamua nimuulize unaishije sasa ndugu yangu akasema ni kawaida ameshazoea maisha hayo.

Tukaongozana kuelekea ndani mlango ulikuwa umefungwa tulipokaribia mlangoni kwake akainama akaokota jiwe nikamuuliza vipi tena mbona jiwe tena akacheka akasema hili sio jiwe ni funguo yangu mara akapiga jiwe juu ya kufuri, kufuri likafunguka nilisitajabu sana.

Alipofungua mlango tu ivi asee chumba hakina sakafu nzuri madirisha hakuna nilipowasha kitochi cha simu hakun godoro analala kwenye mkeka tu

Chumba kichafu sana harufu kali sana ya nguo chafu vyombo kama vinamiaka havijaona maji.
nilishindwa kukaa pale nilimpa pesa kidogo nikaenda zangu kulala lodge

Dar anamiaka karibia kumi lakini hata godoro hana
FUNZO,UNAPOPATA MAISHA MAZURI MSHUKURU MUNGU SANA MAANA KUNA WATU WANAISHI KAMA WANYAMA .
Kuna watu bado wana amini kuwa ni lazima uishi dar kumbe wanapoteza muda tu
 
We ni mnafiki, unapata wapi muda wa kuchunguza maisha ya mwanaume mwenzio kiasi hicho!? Basi ungemchunguza na kumshauri mwenyewe au kumsaidia lkn kwa ulichofanya kupost hapa ni kama ulimnafikia tu ili uonekane umefanikiwa na yeye hajapiga hatua. Kwa tabia hii hata wewe huna maisha yoyote ya maana, usingepata huo muda mchafu.
Msenge huyo
Hio stori yote ni upupu kautunga.....
 
Ukitembelea Dar uswazi unaweza ukalia.

Watu wana maisha magumu sana. Mazingira wanayoishi yanatia kinyaa.

Maeneo ya Tandika, Vingunguti, Manzese n.k oyaa watu wanaishi dampo 🤮🤮🤮

Mitaro ya maji machafu ya vyooni inapita mbele ya nyumba, muda wote kubichi kunatoa harufu na watoto wanacheza humohumo

Mabomba ya DAWASA yanavuja na yamepita kwenye mitaro ya maji ya mavi

Ukiwa na kinyaa sehemu kubwa ya Dar sio mahali pa kuishi ni jalala
 
Back
Top Bottom