Kuna watu hufa mara mbili

Kifo kwa baati mbaya wengi hawakijui kiundani. Kuna hatua tano za kufikia ukamilifu wa kifo, ukweli usiojulikana na pasipo kujua watu wengi wamekuwa wakizikwa wakiwa hai. kama hatua tano za kifo hazikukamilika matukio kama maiti kuamka na kutembea, kupiga chafya, kutingishika, kutoka jasho sana na mengine mengi hujitokeza na kuna uwezekano mtu mapigo ya moyo yakashuka, hawezi kufumbua macho wala kuongea walakutikisika lakini anasikia kila kitu mnachoongea . Sababu mojawapo inayofanya watu kudhani wamekufa ni woga wa kuangalia maiti, utaalamu au vifaa duni vya kupimia.
Asilimia kubwa ya watu wanaotajwa wamefufuliwa kwa njia yoyote ile (kama maombezi) wengi wao walikuwa hawajafa.
Nikipata muda nitakuja kufafanua hatua tano za kufa, na wanaofufuka wanafufukaje
Karibu sana tupate kuelimishana.. Hope utakuja the soonest

Jr
 
Kuna siku nipo nje mchana na washikaji tunalamba kirikuu nipo nimemshika mbwa wangu ametulia. Akapita mshikaji anafanya kazi mochwari huwezi amini yule mbwa alimbwekea sanaa mshikaji yaani ikawa vurugu mechi, jamaa akacheka na kusema atakuwa ameninusa harufu ya kifo

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Lazaro wa biblia ashakaa kaburini siku nne na Yesu akamfufua, na jee ulisoma juu ya Ile skeleton aliyofufua nabii Elisha?
 
Umeshafungua Uzi kueleza hili mkuu?
Kifo kwa baati mbaya wengi hawakijui kiundani. Kuna hatua tano za kufikia ukamilifu wa kifo, ukweli usiojulikana na pasipo kujua watu wengi wamekuwa wakizikwa wakiwa hai. kama hatua tano za kifo hazikukamilika matukio kama maiti kuamka na kutembea, kupiga chafya, kutingishika, kutoka jasho sana na mengine mengi hujitokeza na kuna uwezekano mtu mapigo ya moyo yakashuka, hawezi kufumbua macho wala kuongea walakutikisika lakini anasikia kila kitu mnachoongea . Sababu mojawapo inayofanya watu kudhani wamekufa ni woga wa kuangalia maiti, utaalamu au vifaa duni vya kupimia.
Asilimia kubwa ya watu wanaotajwa wamefufuliwa kwa njia yoyote ile (kama maombezi) wengi wao walikuwa hawajafa.
Nikipata muda nitakuja kufafanua hatua tano za kufa, na wanaofufuka wanafufukaje
 
.
downloadfile-6.jpeg
 
Mwaka 1999 tukiwa nchi fulani hapo bara Asia tukaitwa kuhudumu mahali, kazi yetu ilikuwa ni kumvisha vizuri marehemu tayari kwa heshima za mwisho aliyekufa kwa kupigwa risasi na majambazi na kuporwa pesa nyingi

Jamaa alikuwa maarufu na mwenye pesa hivyo ukumbi ulikuwa umefurika watu wanasubiri kuaga, tukaingia chumba maalum kwa huduma maalum ya kumuandaa jamaa! Dah kumcheki tu tukaona huyu sie kafa na hasira na maumivu hivyo uso na mwili vilikuwa vimekakamaa na alikuwa kama kajikunja

Tukajaribu kutumia mbinu zote tujuazo ili akae vema tumvalishe lakini ikashindikana tukaona anatuletea ujinga tukamletea ukauzu tukampa live kwamba hatujui hatumjui na tunafanya haya kwa ajili yake na watu wake hatulipwi chochote hivyo akiendelea kukomaa tutamvunjavunja viungo nguo ziingie!!! Mbona alilainika na tukamvisha fasta
😳😳😳
 
Kipindi kile ukimwi unaua sana. Kuna njemba iliRIP wananchi wakapanga kuzika jioni. Wakati wa ibada ya kikatoliki padre akaimwagia maiti yale maji wanasema ya baraka.... kulaaleki maiti ikapiga chafya.... Nakumbuka Padre aliyekuwa anawapa watu faraja ndio aliongoza zile mbio za marathoni... Sijawahi ona riadha ya namna ile maana hata kilema alisahau magongo akaunga msafara wa marathoni...

Maiti inatisha acheni masihara. Sijui kwanini zinamheshimu mshana jr
😂😂😂😂😂😂
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom