Salaam wadau?
Mimi ni mdau wa jukwaa la siasa ila nimefungua id mpya ili nije nifunguke kitu kinachonsumbua nafsi yangu na kukosa raha ya kuishi
mimi bwana mdogo wa 23 yearz,nipo chuo diploma,nilipokua na miaka 17 niligundulika na type 2 diabetes(kisukari)nikapewa dawa na nikaambiwa nijiepushe na vitu vya sukari na kufanya mapenzi,nilijitahidi kufanya hivo ila sikudumu kutokana na ujana tena nilijisahau na kuendelea na maisha,sasa mwaka jana nilianza kuumwa umwa, baada ya kupima niligundulika kua ugonjwa wangu umeniathiri vibaya viungo vya uzazi kwaiyo sitoweza kuzaa,sperm zangu ni vimeo..dah niliumia sana na sana,yaani maisha yangu magumu alafu bado napata majanga kama haya.
Japo sasa afya yangu ipo vzuri ila matatizo haya yamenifanya nikate tamaa ya maisha,Nimekua sina raha ya maisha,nipo mpweke naona giza maishani mwangu,chuoni nimeporomoka kiuwezo,nayakimbia mahusiano kwa kuogopa insecurity zangu kwa sababu naona mwanamke atankubali akijua mimi mgumba.
Sikiliza Bw. mdogo. Hapa duniani kila mmoja ana janga lake, usione watu wanatembea kwa kuringa na furaha barabarani... mioyoni mwao wana machungu yao.
Kwanza kabisa ikubali hiyo hali uliyonayo. Wewe kuwa mgonjwa, na kutokuwa na mtoto au matatizo yote uliyonayo yasikufanye usifurahie kuishi kwa raha katika dunia hii kadri utakavyojaliwa na Mungu. Jikubali kuishi hivyo .... hutakaa hapa milele. Furahia kipindi kifupi ulichonacho. Sio kweli kwamba huna bahati, usikate tamaa hata siku moja.
Ishi jinsi unavyotakiwa kuishi...... nimechoka kuandika mie..... Maisha mema