Kuna watu hatuna bahati

Kuna watu hatuna bahati

Ni-PM tujadiliane kwa kina tatizo lako. Kama hutajali.
 
Sikiliza kijana.

Kwanza hiyo "sperm vimeo" inabidi ueleze ni "sperm count" au "motility" yenye matatizo? Yote hayo yanatibika kwa aina moja nyingine.

Halafu siku hizi kuna hospitali zina specialize matatizo ya uzazi kama si Tanzania hata nje ya Tanzania, utaalam uko mbali sana siku hizi, wale amabao miaka 10 nyuma walikuwa hawana njia ya kutibika kupata watoto sasa hivi wengi wao wanatibika.

Kama functionality ya sperm zako hairidhishi kuweza kumpa ujauzito mwanamke "naturally" basi kuna njia nyingi mbadala.

Hebu funguka tukupe ushauri sahihi na usikate tamaa ni mtihani wa maisha tu. Mbona wengi wenye kisukari wanazaa, ondoa hofu kuna njia mbadala nyingi tu.

asante sana,nahisi matumaini yapo hapa ni kujitahidi kutunza afya yangu isiharibike zaidi
 
pole sana mkuu ila usivunjike moyo mapema hivyo muombe tu mungu ni muweza wa kila kitu
 
Pole. Nina IDDM ya muda mrefu kuliko wewe, na nashindwa kuelewa DM yako imewezaje ku-fast track kiasi hicho hadi kufikia ugumba kwa kipindi cha less than 8 years. Either way, jibu maswali ya Bi. FaizaFoxy kwanza. Msaada is just around, if you spell correctly what is happening with you
 
Last edited by a moderator:
Daaah nakushukuru Mungu na nasema tena Ahsante.


Ndugu usikate tamaa, maisha ni matamu kama utaikubali hiyo hali na kuamua kukabiliana nayo, mtegemee sana Mungu hakuna linaloshindikana kwake, kama tatizo ni kuzaa mbona dogo sana hilo, alifufua wafu seuse hilo!! Kuna wenye mazito zaidi yako so ukikaa kuwatafakari utajikuta unamwambia 'Mungu ahsante'
Fuata masharti ya madaktari huku ukimtegemea sana Mungu.
 
Salaam wadau?
Mimi ni mdau wa jukwaa la siasa ila nimefungua id mpya ili nije nifunguke kitu kinachonsumbua nafsi yangu na kukosa raha ya kuishi

mimi bwana mdogo wa 23 yearz,nipo chuo diploma,nilipokua na miaka 17 niligundulika na type 2 diabetes(kisukari)nikapewa dawa na nikaambiwa nijiepushe na vitu vya sukari na kufanya mapenzi,nilijitahidi kufanya hivo ila sikudumu kutokana na ujana tena nilijisahau na kuendelea na maisha,sasa mwaka jana nilianza kuumwa umwa, baada ya kupima niligundulika kua ugonjwa wangu umeniathiri vibaya viungo vya uzazi kwaiyo sitoweza kuzaa,sperm zangu ni vimeo..dah niliumia sana na sana,yaani maisha yangu magumu alafu bado napata majanga kama haya.

Japo sasa afya yangu ipo vzuri ila matatizo haya yamenifanya nikate tamaa ya maisha,Nimekua sina raha ya maisha,nipo mpweke naona giza maishani mwangu,chuoni nimeporomoka kiuwezo,nayakimbia mahusiano kwa kuogopa insecurity zangu kwa sababu naona mwanamke atankubali akijua mimi mgumba.


Sikiliza Bw. mdogo. Hapa duniani kila mmoja ana janga lake, usione watu wanatembea kwa kuringa na furaha barabarani... mioyoni mwao wana machungu yao.

Kwanza kabisa ikubali hiyo hali uliyonayo. Wewe kuwa mgonjwa, na kutokuwa na mtoto au matatizo yote uliyonayo yasikufanye usifurahie kuishi kwa raha katika dunia hii kadri utakavyojaliwa na Mungu. Jikubali kuishi hivyo .... hutakaa hapa milele. Furahia kipindi kifupi ulichonacho. Sio kweli kwamba huna bahati, usikate tamaa hata siku moja.

Ishi jinsi unavyotakiwa kuishi...... nimechoka kuandika mie..... Maisha mema
 
Hajasema ana shida ya motto bali mtoto

Dah jamani, na maana ni tofauti kabisa, umenishtua nikasema isije mlengwa akadhani ni huo motto, ila nimerudia nimekuta amejibu kwa kunisahihisha. Asante lakini.
 
Pole mkuu bora uwe masikini lakini uwe na mtoto very sad
 
Maisha ni zaidi ya ndoa na watoto, kuna watu ndani ya ndoa hawana hamu nazo.
Ukinyimwa upande huu unapewa upande mwingine
 
Pole. Nina IDDM ya muda mrefu kuliko wewe, na nashindwa kuelewa DM yako imewezaje ku-fast track kiasi hicho hadi kufikia ugumba kwa kipindi cha less than 8 years. Either way, jibu maswali ya Bi. FaizaFoxy kwanza. Msaada is just around, if you spell correctly what is happening with you

mkuu pole,mi ya kwangu ya kurithi na hvo unavosema imekua haraka ndo hata daktari ameshangaa inshort mimi bado nahangaika nipate daktari ambaye atakayeweza kujua whats behind it
 
Last edited by a moderator:
al-baajun

mungu aliye kuumba wewe hashindwi kukuponya...kikubwa ni imani tu.
 
Last edited by a moderator:
Daaah nakushukuru Mungu na nasema tena Ahsante.


Ndugu usikate tamaa, maisha ni matamu kama utaikubali hiyo hali na kuamua kukabiliana nayo, mtegemee sana Mungu hakuna linaloshindikana kwake, kama tatizo ni kuzaa mbona dogo sana hilo, alifufua wafu seuse hilo!! Kuna wenye mazito zaidi yako so ukikaa kuwatafakari utajikuta unamwambia 'Mungu ahsante'
Fuata masharti ya madaktari huku ukimtegemea sana Mungu.

namshukuru mungu pia,kweli nikifkria wenye matatizo zaidi yangu naona nina afadhali mungu akubariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom