Kuna wana maombi humu?

Kuna wana maombi humu?

picasso

New Member
Joined
Nov 13, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Jamani nimetoka kazini nipo hoi, nilikuwa busy sana leo. Sikupata hata nukta ya kupumzika. Nimefika home wife kaniudhi sana. Yaani nina hasira mpaka nimeshindwa kulala. Usingizi wote umeondoka. Sasa nimegundua mwenzangu anapenda ugomvi sana, nimefika mahali nimechoka sana naona siku si nyingi ntafanya kitu cha kuishangaza dunia. Naomba mniombee ili niwe na moyo wa uvumilivu, niepukane na mwovu shetani. Kila siku narudi home nimechoka lakini sipati hata nafasi ya kupumzika, nakuta maudhi ya ajabu.
 
Tupo ndio.
Lkn na ww inabidi utumie kinywa chako kumkemea shetan sio kuombewa tu.

Btw mambo gani hayo yanayokuudhi maanaake somtym ukute yanahitaji ushauri tu sio kila kitu maombi
 
wana maombi? humu MMU? sijui labda wapo!!!!
nimekumbuka mwallu kam this wei uongoze maombi
 
Last edited by a moderator:
Kaka maombi si unga wa ngano useme waweza kuutumia utakavyo. We only pray with focus. Shida yako wewe sio maombi ni kaushauri tuu. Wewe kwa nini umwone huyu mkeo kuwa ni tatizo? Utalijuaje tatizo kama weye sio tatizo? Jieleze upewe ushauri. Ati utafanya kitu dunia ishangae, mwe mwe mweee Tumefikia huko! Lahaulla ! Nakuambia hata sasa imeshakushangaa. Utafanya nini kipya? Poa tu mpende mkeo wala hatakuudhi unaudhika kwa sababu ya kale kabinti paleee.
Bora ni huyo anayekuudhi
 
Shemeji hajaweka chumvi kwenye chakula?? au hajapeleka maji bafuni?? au watoto wanazogoa sana??

Utafanya kitu duni ishangaee?? kuna jela mkuu, ni mbaya kuliko unavyoifikria kule wanakunyonya ulimi tu, mpaka upuye..
 
Khaa! Kwaiyo mkeo ni VUVUZELA!!!
Pole!
Kuwa mvumilivu!
 
Jamani nimetoka kazini nipo hoi, nilikuwa busy sana leo. Sikupata hata nukta ya kupumzika. Nimefika home wife kaniudhi sana. Yaani nina hasira mpaka nimeshindwa kulala. Usingizi wote umeondoka. Sasa nimegundua mwenzangu anapenda ugomvi sana, nimefika mahali nimechoka sana naona siku si nyingi ntafanya kitu cha kuishangaza dunia. Naomba mniombee ili niwe na moyo wa uvumilivu, niepukane na mwovu shetani. Kila siku narudi home nimechoka lakini sipati hata nafasi ya kupumzika, nakuta maudhi ya ajabu.
Ngojea nimtafute dada mmoja kaokoka akuombee,pole sana kaka!
 
Sasa Kaka, Dunia Imeingia Katika Enzi Ambayo Matatizo Husolvika Kwa Maneno, Vita Kubwa Ambayo Ingemalizwa Kwa Drone Na Makombora Watu Wanamaliza Mezani Kwa Juice Ya Mango, Kwakuwa Una Mwamini Mungu Hebu Fanya Mazoea Ya Kuombea Tatizo Hili. Na Akikutibua Tumia Njia Ya Ukimya, Enzi Mpya Ya Kutibu Matatizo Ya Ndoa! Akikutibua Chumbani Nenda Sebuleni Na Uweke Fikra Zako Jamii Forum, Tutakutuliza. Maisha Huambukiza Unajua? Hii Ndio Sababu Wanandoa Wa Muda Mrefu Huwaga Na Tabia Zinazo Fanana, Tenda Mema Daima. Kama Kunakitu Hajafanya, Fanya! Ata Addopt Na Maisha Yatakuwa Vyema! Tunakuombea, Na Pokea Amani, Tatizo Hili Halipo Tena Kwa Imani, Hebu Tusubiri Kupokea!
 
Inawezekana uchovu wako umebadilisha mfumo wa maisha ambao mkeo anashindwa kuupokea,labda huko nyuma mlikua mnakaa mezani na kujadiliana kuhusu familia ila sasa umepata uchovu na umekuwa mwamuzi wa kila kitu...mkeo ameshindwa kulipokea hilo..
Kabla ya kufikiria ubaya na tatizo la mwenzako jaribu kujichunguza undani wako..
 
Ndoa ndoano. yereuwiiii. kuna watu wanakera ukirudi home hupati proper mapokez lazima upokelewe na vijimaneno maneno irrelevant. no kiss no passion basi kero tupu!!!!!!
 
Pole sana mkuu hilo ni tatizo kubwa. Umesema mkeo anapenda ugomvi basi itabidi utafute muda muafaka mkae mzungumze ili aelewe wewe hupendelei hayo makitu ya kugombana. Ni kweli wako watu wanapenda sana ugomvi na imekua hobi kwao. Kubadili mtazamo wa mtu wa aina hii inatakiwa yeye mwenyewe kwanza ajitambue na atambue kuwa ugomvi sio dili.

Umeomba jambo jema maombi , tunakuombea lkn hiyo nia yako ya kufanya kitu dunia ishangae acha kabisa mawazo hayo kwani hakuna jipya chini ya jua sana sana wewe ndio utakua looser. Amini kwamba Mungu anaweza na yuko karibu nawe kuliko unavyofikiri na anakuwazia mema daima. Mungu anakupenda jinsi ulivyo na yuko tayari kubadili hali hali hapo nyumbani kwako.Naomba amani ya Kristo ipitayo akili zote ifurike kwa wingi moyoni mwako .
 
Utatuzi wa matatizo ya ndoa umo ndani ya wanandoa wenyewe. Nyote wawili mnahitaji maombi. Mungu akuongozeni mpate kumshinda shetani anayetaka kuharibu nyumba yenu.
Kaa na mkeo na muelezane yanayowakera. Nina hakika mkeo ana sababu zake zinazomfanya atende au aseme hayo unayoita maudhi. Pengine naye atasema chanzo ni wewe! Fanyeni maombi pamoja, amani itapatikana. Sisi tutafanya maombi lakini uwezo wa kurudisha na kudumisha amani nyumbani mwenu umo ndani yenu (wewe na mkeo). Amani ya Kristo itawale!
 
Yes
Tupo Demba tuliompokea Yesu, shaka ondoa

haaa haaa poa lakini huyu jamaa hahitaji maombi wala nini anahitaji kujitahmini na kuangalia wapi alipojikwaa ili aondoe kisiki na kusonga mbele, tatizo hapa tuna story ya upande mmoja, uwe na mwanaume muadilifu tu, mwenyekutambua wajibu wake halafu uwe na kelele tu sidhani labda awe na upungufu wa akili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom