Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,614
Jamani nimetoka kazini nipo hoi, nilikuwa busy sana leo. Sikupata hata nukta ya kupumzika. Nimefika home wife kaniudhi sana. Yaani nina hasira mpaka nimeshindwa kulala. Usingizi wote umeondoka. Sasa nimegundua mwenzangu anapenda ugomvi sana, nimefika mahali nimechoka sana naona siku si nyingi ntafanya kitu cha kuishangaza dunia. Naomba mniombee ili niwe na moyo wa uvumilivu, niepukane na mwovu shetani. Kila siku narudi home nimechoka lakini sipati hata nafasi ya kupumzika, nakuta maudhi ya ajabu.
Kwa hatua ulofikia na kutambua kuwa unahitaji kuombewa - ni hatua nzuri ambayo wewe mwenyewe unaweza kupiga magoti chumbani ukiwa peke yako na kutafakari nini chanzo; baada ya hapo mwombe Mungu aweze kukuondolea matatizo hayo. Kuwa serious wakati wa kuomba hakika maombi yako yatajibiwa. POLE SANA RAFIKI.