Kuna vivutio gani mkoa wa Mara?

Mzee hakuna mazuri yoyote huko maana naona umeelezea vyote in a negative way
 
Sasa unaingia mkoa wa Mara! Jamaa ni wakorofi wa asili ngumi visu nje nje! Wana wivu hatare! Usiwazoee mno wapee distance! Ukitoka let's say ukiwa bar jitahidi kukwepa makundi! So and so forth.
 
Wakuu nitoe shukrani kwa michango yenu. Nimesharipoti mkoa wa Mara, na sasa nina wiki tangu nifike hapa Tarime.

Kiukweli yote mliyonipa tahadhari nimeyazingatia kwa umakini. Mengi nimeweza kuyafaham kwa hii wiki moja niliyokaa hapa na mengi zaidi nitayajua kwa kadri siku zitakavyoenda panapo majaaliwa.

Wakazi wa huku ni wakarimu ila ni wenye hofu sana na wageni (sijajua ni kwanini). Lodge nyingi nilizokaa nimekua nikihojiwa maswali kuhusu uraia na napotokea nahisi kwavile mimi ni shombe shombe ( jambo ambalo sikulizoea)

Kuhusu sehem za kula bata aisee huku ni kama hakuna. Bado wako nyuma sana. Hakuna pisi kali kabisa. Hapa nikiri tu ukizoea kukaa dar unaweza usione mwanamke wa kutongoza huku. Pisi zilizopo ni zile sura personal tu na zinaongea kibabe [emoji23], halafu unakuta vijana wanababaika nazo hatari. Nimeshangaa sana.

All in all sina budi kupambana na hali yangu ndani ya huu mwaka mzima mpaka project yangu itakapoisha hatimae nirudi ktk mji niliouzoea. Nitangulize shukrani za dhati sana [emoji120]
 
Bora kutembea na mke wa mtu lakini sio binti wa mtu,utatahiriwa kwa mara ya pili
 
Serengeti national park japo wengi wanadhani ipo arusha
 
Kuna mchongo nimedaka wa NGO boss, nahisi nitakua kule miaka miwili hivi.

Umeshawahi kuishi Tarime mkuu?

Sent from simu ya kuazima
Tarime ndiyo wilaya pekee ktk mkoa wa Mara iliyochangamka! Watu wa Tarime ni wachapa kazi na wafanya biashara wazuri sana. Pia ni wachangamfu na wakarimu sana. Kuna fursa za madini hasa dhahabu. Ardhi yake ina rutuba sana hivyo kilimo kinakubali sana. Changamana nao vizuri hutojutia. Hakikisha unakuwa mtu wa haki, acha dhuluma na ghiriba. Hakikisha unajiweka pembeni na wake za watu vinginevyo ubabe wa Wakurya utauona.
 
Ziwa Victoria na visiwa vyake vingi vingi tu
 
Unaweza kuacha wazi gari ama nyumba ikiwa na fedha na watu wasishughulike navyo vyote,hii ni kawaida sana, kosa wasikie kuwa una mawe ya dhahabu ndani! Ni very risky kwa maisha yako ndugu. Kuwa na jiwe la dhahabu ni kama kuwa na nyara ya serikali! Roho mkononi!
 
Duh kama ndio wilaya iliyochangamka inakua hivi. Sipati picha huko palikopoa pakoje [emoji23][emoji23][emoji23]. Yes fursa zipo nyingi, unaweza buni kitu kipya huku ukapiga ela ndefu sana nimeona hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…