Kuna vituo vingapi vya "Fire" vya Serikali Dar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna vituo vingapi vya "Fire" vya Serikali Dar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 4, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa vile serikali ya CCM imeamua mtindo wa kubinafsisha huduma muhimu tumeona hivi karibuni wakibinafsisha shughuli za usalama kwa Majembe Auction Mart na kwa muda mrefu wamebinafsisha hata shughuli za uokoaji na kupambana na moto. Hili limekuja baada ya kubinafsisha shughuli za ulinzi wa Polisi kwa kuruhusu uwepo wa vikampuni binafsi vya polisi (private police companies).

  Tumeona upungufu wa mkakati huu kwenye majanga yanayoendelea ya mvua ya Krismasi (kama nilivyodokeza, tukiwa mtandao wa kwanza kuripoti juu ya mvua hiyo masaa 12 kabla ya vyombo vya habari vya Tanzania havijarukia).

  Tumeonesha kwenye suala la hospitali ya Temeke na sasa najiuliza kwenye kupambana na majanga ya moto, je serikali ya CCM itaendelea mpaka lini kubinafsisha usalama wa maisha ya watu wetu? Mpaka wapi kuungue ndio tutajua kuwa huwezi kuwa na jiji la kisasa bila ya huduma ya kisasa ya kupambana na mojawapo ya majanga ya kawaida kabisa kutokea yaani moto?

  - Ilipoungua Ikulu hatukujifunza?
  - Ilipoungua Benki Kuu hatukujifunza
  - Ilipoungua Nasaco hatukujifunza
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  MKJJ,

  Umeacha kuorodhesha jengo la kitegauchumi cha Bima!

  Nadhani umeng'amua kuwa nia ya msingi ya kubinafsisha huduma zote za muhimu namna hiyo, ni kujinufaisha binafsi kwa wachache wenye dhamana za idara na wizara husika. Taifa zima linaangamizwa kutokana na kiu ya fedha chafu za kikundi fulani cha manyang'au wachache.

  Hizo fedha wanazopata wala hazitawatosha. lakini kitakachowakumba mwishoni ni AIBU!
  Wanatembelea nchi za wengine kushangaa, lakini hakuna wanalojifunza!
  AIBU yao milele!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  PJ, ni kweli.. mimi naiita "template" ya mafisadi yaani kuharibu cha umma ili walete cha binafsi. Tatizo ni kuwa wanafanya hivi hata kwenye mambo muhimu sana kwa taifa na ya usalama wa taifa. KUanzia Tanesco, Posta na Simu, Ulinzi na Usalama na sasa tusipoangalia hata uchaguzi utabinafsishwa ili waendelee kuchaguliwa wao.
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nadhani viko viwili vya jiji. Kimoja kiko faya na kingine Temeke. Kuna vikosi vya zimamoto uwanja wa ndege na bandari.

  Amandla......
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hapa hoja sio VITUO VINGAPI VYA FIRE!.....hoja ni kwanin hivi vituo haviko active?....

  imewahi tokea mikocheni hapo LIMOZIN inawaka moto ajabu,lilikuja gari la faya pale kwa mwendo mkali kweli kweli...!kufika pale HALINA MAJI!.......

  WTF
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  na hivi vituo vina magari mangapi kila kimoja; vile vya Bandari na Uwanja wa Ndege sivihesabu kwani vinatakiwa viwe standby kwenye maeneo yao hiyo naamini ni kinyume hata cha taratibu kuondoa magari yao kwenye kupigana na moto uraiani.. Kwa hiyo kama tukizungumzia vya kiraia vipo viwili.

  Sijui vina magari mangapi.. nitatafuta majibu ya haya.. na kwenye jiji la watu karibu milioni tatu ni mahitaji gani yaliyopo?maana usije kuta nyumba ya Gavana ingeweza kununua magari kadhaa ya kupambana na moto siku moto ukisha nyumba hiyo!
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Geoff hii hoja nilishaisikia mara nyingi tu mara magari yamekuja na hayana maji au maji hayatoshi hivi huwa ni kweli? Hivi dereva wa gari hilo anapolitoa spid toka kituoni kwenda eneo la tukio haangalii kama kuna maji au la? anakwenda kufanya nini sasa eneo la tukio amekuwa mwandishi wa habari ambaye hata yeye ana afadhali maana hukumbuka kamera yake au kalamu yake ya uandishi.

  Mimi siamini kama serikali inashindwa kutatua tatizo hili nali tu ule utayari haupo. Kama tunaweza kuruhusu ujenzi wa nyumba za mabilioni, kesi za EPA e.tc. serikali inashindwa kweli kuturubuni kwa kiini macho cha fire??
   
 8. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #8
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Geoff,

  I wanted to say the same thing....

  Mwanakijiji, hata magari yawepo, na maji hamna itasaidia vipi?
  ...hapo hatujaongeza umeme kwa mgao bro. Water pressure operates
  on electricity na utaona bomba zinamimina maji kana kwamba mtu
  anamaliza kukojoa vile. Gaademm!

  Mwenzio nishashuhudia fire wakija kuzima moto kisha wanaanza
  kuomba watu mabeseni ya maji eti gari lao halina maji.

  Umesema hapo juu Ikulu, benki Kuu na Nasaco ziliungua na
  hatujajifunza nd'o iwe Magomeni mapipa kwa walalahoi?

  Tutafika kweli?

  P.S. Magari ya Fire ya Private yanamilikiwa na nani? Is it by design that they exist?
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kaangalieni nyumba wananzo jenga mawaziri na wakubwa wengine wa CCM kama hata zina mitungi ya gesi ya kuzimia moto hapo ndo mtajua kweli wanajali
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Jan 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Hata kama Dar ina watu milioni kadhaa (who knows idadi kamili) kwa nini iwe Dar tu? Lindi na Mafia kuna vituo vingapi vya zimamoto na EMS? Au huko hakuna watu wanaoweza kuungua na moto?
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  The question was supposed to be, "kwanini vituo vya zimamoto havina zana", Dar ukiangalia kile cha fire ni kama magofu cha temeke ni kama kaburi.

  Ukiangalia hata mji wetu unavyopangwa hakuna hata njia ya hayo magari kupita, wakati mwingine unakuta limekaa pale halina hata maji, au likienda sehemu ya tukio linakuwa halina hata maji(excuse ni kuwa si kila moto unahitaji kuzimwa kwa maji)

  By the way who cares kama nyumba yako ikiungua! Kama no body in the government seem to care about you when you get sick or when you have nothing on the table, ambayo kila siku yanaonekana. What about moto ambao hatujui lini utatokea?
   
 12. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kizazi hiki kimeoza.kizazi cha bongo flava.
  Ajabu kuna watu walikuwepo na wapo tangu enzi za uhuru kwenye nafasi kubwa kiuongozi,sasa huo uozo unatoka wapi?
  Wakifa vigogo,unasikia kigogo anasema tumeondokewa na mtu mhimu kwa mustakabali wa Taifa,tutakosa ushauri wake nk.Je wanataka kutuambia kuwa Ushauri wao ndio umetufikisha hapa?
  Je wewe uliye na dhamana sasa mchango wako kwa ustawi wa Taifa hili ni upi?
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Duuuh!
  Hii ni kali Dodoma Kimmoja na Mwanza Kimmoja, A town Kimmoja, Kwingine nilikopita siju, Ukiangalia hata mazingira yao ya kazi jamani aibu tupu kumechakaaaa.

  Kadri tunavyosonga mbele nimekuja kugundua kuna mashirika mengine yanakufa kabisa na hayafufuliwi na kwaibuka mashirika ya ajabu ajabu tena ya watu binafsi,mashirika yaliyokufa na sijui kama yana uhai wakufufuliwa tena eg Nyaza,Shireku, nakadhari wengine mtamalizia, Hapo nashindwa kuelewa Serikali inajipa marks vipi kuwa inasonga mbele au haiwezi mambo mengine? na kwanini isifanye vichache kwanza kwa kadri ya uwezo wao na wawe wanasonga mbele kuliko kujilimbikizia project nyingi bila mafanikio?
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hapa mnakosea. tatizo ni kuwa swali la Mzee Mwanakijiji halitoshelezi. Kinachotakiwa kuulizwa ni kuna infrastucture ya aina gani ya kupambana na moto katika jiji la Dar es Salaam? Gari la zimamoto hata siku moja halitakiwi kutegemea maji iliyoyabeba peke yake kupigana na moto. Panatakiwa kuwa na fire hydrants sehemu nyingi ili gari liweze kufyonza maji hapo. Kwenye majengo makubwa panatakiwa na njia ya maji iliyokuwa dedicated kwa ajili ya kuweza kufyonzwa panapotokea janga la moto. Zimamoto wanapokuja kwenye tukio wanatakiwa kuunganisha mipira yao hapo, yale ya kwenye gari ni ya hatua za mwanzo tu. Tulikuwa na system ya fire hydrants katika sehemu ya jiji letu na hata katika majengo lakini kama kawaida yetu tuliona ni anasa na hatukuzihudumia mpaka sasa hivi zimebakia historia. Tujiulize kuna vifaa vingapi vya kupigana na moto katika kumbi zetu za starehe, nyingi ambazo zimeezekwa na makuti? Zaidi ya hapo, ni wangapi wanajua kuvitumia ? Na jee sehemu za milango ya tahadhari ziko wazi na zinaweza kutumika? Mara nyingi milango hii utakuta imewekewe grili kwa nje ili kuzuia vibaka! Ngazi ngapi za tahadhari ziko wazi katika majengo yetu? Ni mara ngapi wafanyakazi na wanafunzi katika maofisi, mashule, hospitali wamepewa faya drill ili kuhakikisha kuwa wanajua nini cha kufanya panapotokea moto? Vituo ni nyongeza tu, ni sehemu ya infrastructure na tamaduni nzima ya kupambana na moto. Matatizo yetu ni makubwa kuliko uhaba wa vituo na vitendea kazi!

  Amandla..........
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Idara "Fire" ipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani (or whatever you may call it) na kama ilivyo kawaida hii wizara uwa haina takwimu! Nenda Police, Nenda Uhamiaji mambo ni yale yale! Hili swali hata ukimuuliza Katibu Mkuu wa Wizara hajui magari ya "fire" yapo mangapi na kati ya hayo yapi yanafanya kazi!

  Kama ulivyobandika hapo juu, Genge la watu wachache wenye uchu linaharibu mali za umma ili liweze kufaidi. Utendaji duni wa idara "fire" linaanzia mbali, na kama unakumbuka kuna mtuhumiwa wa EPA alipewa tenda ya kunua magari ya "fire" kwa baadhi ya halmashauri (mojawapo ni Songea), magari yalifika lakini hayajawahi kufanya kazi tangia wakati huo! Of course yeye binafsi out of that tenda and other dubious dealings aliweza ku-airlift VOGUE!

  Anyways Happy New Year all Jf Members.
   
 16. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kujua ya kuwa sisi watanzania tuna fikra fupi basi nenda maeneo ya makumbusho ya taifa pale karibu na hoteli ya Royal Palm, utaona mabaki ya Fire Hydrants njiani . Hizi fire hydrant ambazo ni kwa ajili ya kujaza magari ya zimamoto zilijengwa na mkoloni miaka ya hamsini au arobaini huko. Kwa hiyo kwa maana nyingine, mzungu aliona umuhimu wa kuwa na fire hydrant katika mitaa yake katika kipindi hicho .


  Ni jambo la kusikitisha lakini hii ndio nchi yetu , priority zetu tumeweka kwenye bongo flavor, mashindano ya umiss na Ndombolo ya solo.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jan 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  On the same infrastructure tip...vipi zile sehemu ambako watu wamejenga kiholela holela? Maana kuna sehemu kama pale Tabata, Ubungo, au hata mitaa ya Tangi bovu ambako hakuna njia hata gari na hata baiskeli na pikipiki hazifiki. Kuna nyumba na sehemu za starehe (baa na migahawa) zinazofikika kwa miguu tu. Huko kukitokea moto itakuwaje?
   
 18. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Wanaenda na maji, lakini ile pump ya maji inamaliza tenki zima ndani ya dakika 2-3, kunatakiwa kuwe na fire hydrants kama wadua wengine walivyosema.
  Lakini ndo hivyo hata maji ya nyumbani taabu, fire hydrants usiulize kabisaa!!
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mapenzi ya Mungu. Binadamu hawezi kuzuia!

  Amandla......
  .
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unafikiria vizuri kwani sasa unajua tatizo letu ni kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria... Kama Dar jiji kubwa zaidi na lenye watu wengi zaidi lina vituo viwili tu rasmi huko mikoani kila mkoa si una kituo kimoja tu na wengine hakuna kabisa? Nakumbuka Tanga kilikuwepo kimoja sijui kama kimeongezwa!
   
Loading...