Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema chama hicho hivi sasa kinakumbana na viongozi wasaliti wasiojua wajibu wao wa kulikomboa Taifa.
Akihutubia kongamano la wadau na viongozi wa Kanda ya Kaskazini kiongozi huyo amesema sababu kubwa ya usaliti huo ni uroho wa madaraka kwa baadhi ya watu.
Mwenyekiti huyo anayeongoza chama kikuu cha upinzani nchini amesema kwa sasa chama hicho hakitavumilia viongozi wasaliti na badala yake watakuwa wanaelezana ukweli na kuchukua hatua stahiki kila inapobidi.
Kauli hii ya Mbowe itakuwa msumari wa moto kwa baadhi ya viongozi wanafiki na wanaotumika kutaka kuvuruga chama hicho.
Mbowe ni kiongozi ambaye anaungwa mkono na idadi kubwa ya wafuasi wa CHADEMA kote nchini kutokana na kazi kubwa anayofanya kuimarisha chama hicho kiasi ambacho Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akiwahutubia watendaji wa CCM hapo jana amehofia chama chake kuondolewa madarakani kupitia sanduku la kura mwaka 2015.
Source:ITV Habari