Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Kwa yoyote mwenye kufuatilia mienendo ya kisiasa na kiserikali atakubaliana na mimi kwamba Magufuli siyo mpenzi kihivyo wa demokrasia. Hili siyo tusi wala lawama, ni mtazamo wangu kuhusu mtazamo wake! Na hata yeye mwenyewe anasemaga mara kwa mara kwamba demokrasia inatuchelewesha!
Siku baada ya siku ameonekana kuegemea upande wa taasisi ya jeshi hadi kufikia kusuggest timu ya taifa itoke Jeshini. Hizi siyo kauli ya kubeza, anaamini kabisa kuwa ndiyo suluhisho la matatizo yetu yote. Huu ni mtazamo wake ambao unajadilika (kama tutaruhusiwa kujadili!)
Katika tafakari yangu namuona pia kama ni mtu ambaye hata madaraka aliyonayo angependa ayapate kwa njia nyingine ukizingatia kama nilivyotangulia kusema, siyo mfuasi mkubwa sana wa mfumo wa demokrasia.
Nakumbuka 2015 siku ya mwisho ya kampeni kule Mwanza, Kikwete alionekana kama anampandisha mori achangamke (tafuta clip wakati Kikwete anampa nafasi ya kuongea). Toka hapo amekuwa na miaka 5 ya kujizatiti kufikia ndoto yake ya kupata madaraka na kuongoza kwa mfumo alio comfortable nao zaidi.
Huwa siyo rahisi kumshinda Raisi aliye madarakani katika uchaguzi (incumbent President) hata awe ameboronga kivipi. Ni kazi ngumu sana hata kwenye nchi zenye demokrasia iliyokomaa. Nikitumia maneno ya kiingereza ambayo sidhani kama naweza kupata tafsiri sahihi naweza kusema 'the election is his to lose'.
Sitashangaa mwakani akiwatuma wengine wakafanye kampeni huku tukaambiwa yeye ana majukumu muhimu zaidi.
Baada ya hapo chacha!