Elections 2020 Kuna uwezekano Magufuli hatafanya kampeni Uchaguzi wa 2020

Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,700
2,000
Kwa yoyote mwenye kufuatilia mienendo ya kisiasa na kiserikali atakubaliana na mimi kwamba Magufuli siyo mpenzi kihivyo wa demokrasia. Hili siyo tusi wala lawama, ni mtazamo wangu kuhusu mtazamo wake! Na hata yeye mwenyewe anasemaga mara kwa mara kwamba demokrasia inatuchelewesha!

Siku baada ya siku ameonekana kuegemea upande wa taasisi ya jeshi hadi kufikia kusuggest timu ya taifa itoke Jeshini. Hizi siyo kauli ya kubeza, anaamini kabisa kuwa ndiyo suluhisho la matatizo yetu yote. Huu ni mtazamo wake ambao unajadilika (kama tutaruhusiwa kujadili!)

Katika tafakari yangu namuona pia kama ni mtu ambaye hata madaraka aliyonayo angependa ayapate kwa njia nyingine ukizingatia kama nilivyotangulia kusema, siyo mfuasi mkubwa sana wa mfumo wa demokrasia.

Nakumbuka 2015 siku ya mwisho ya kampeni kule Mwanza, Kikwete alionekana kama anampandisha mori achangamke (tafuta clip wakati Kikwete anampa nafasi ya kuongea). Toka hapo amekuwa na miaka 5 ya kujizatiti kufikia ndoto yake ya kupata madaraka na kuongoza kwa mfumo alio comfortable nao zaidi.

Huwa siyo rahisi kumshinda Raisi aliye madarakani katika uchaguzi (incumbent President) hata awe ameboronga kivipi. Ni kazi ngumu sana hata kwenye nchi zenye demokrasia iliyokomaa. Nikitumia maneno ya kiingereza ambayo sidhani kama naweza kupata tafsiri sahihi naweza kusema 'the election is his to lose'.

Sitashangaa mwakani akiwatuma wengine wakafanye kampeni huku tukaambiwa yeye ana majukumu muhimu zaidi.

Baada ya hapo chacha!
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
28,613
2,000
Sio kwamba hataki demokrasia, ukweli ni kuwa haiwezi. Ni kama anavyojifanya anakienzi kiswahili, ukweli ni kuwa lugha ya kiingereza inampiga chenga kuiongea kwa ufasaha. Hata sasa analitumia jeshi kwakuwa jeshi pia linadhani lina wajibu wa kuhakikisha rais aliyeko madarakani ana haki ya kushinda uchaguzi yeye na chama chake. Hiyo 2020 analitegemea jeshi na vikundi vya kihalifu kuhakikisha anatangazwa mshindi kwani hana uwezo wa kushinda kwa ushawishi.
 
Carlos The Jackal

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
15,209
2,000
Fuatilia nchi zote ambazo viongozi wake, wamewapa uhuru na nafasi kubwa Jeshi. Hata jeshi kushikilia nafasi nyet nyeti za kimfumo.

Hii maana yake nin?? Huwa wanawapa Chambo wanajeshi hawa, ili wale washibe bila kuangalia chambo iki kimepikwa nann.

Matokeo yake nn? Wanajeshi wakishakuja baadae kugundua kua Chambo walichokula kina uwalakini. Nakwamba ikitokea Madaraka yakataliwa na kiongozi mwingine basi wao na maisha yao kwaujumla yatakua rehani.

HUISHIA KUKUBALIANA KUA. KWA FAIDA YAO. NAMAISHA YAO NA UCHUMI WAO. NI MARA MIA WAENDELEE KUMSAPOT KIONGOZI ALIWALISHA CHAMBO ILI UWEPO WAKE MADARAKAN UWEZE KUWAHAKIKISHIA ULINZI.

zitazamen nchi zote ambazo Jeshi lina nafasi mf, Venezuela.

"In Good times ,Friends know you BUT in Sorrow, you know them "
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
18,380
2,000
Tume yako
Police wako
Usalama wa nchi ni wako
Wakurungezi watangaza matokeo ni wako
Mwendesha mashitaka yoyote yale ni wako
Msajili wa vyama ni wako

Kampeni za nini hata ningekuwa mimi? na bila kuwa na plan B kwa hawa vyama mbadala hakuna diwani watapata achilia mbali mbunge.

Narudia tena bila mikakati mahsusi ya ushindi basi tunarudi chama kimoja. Yaani tutaaibika dunia nzima nchi ambayo badala ya kusonga mbele yenyewe inarudia ile mifumo ya nyuma, utashangaa tunafika hadi kwenye ujima, maana tunakwenda kisengelenyuma kwa speed kali.
 
FORTALEZA

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
4,420
2,000
Acha ujuha wewe! Fatilia kuhusu Rais George H.W. Bush (Bush Mkubwa) mbna alikuwa Rais wa muhula mmoja!

Shida ipo huku Dunia ya tatu, baada ya Mungu anayefata ni Rais.
 
mikedean

mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,331
2,000
Kwa mfani hapa Mbeya atakuja kutueleza nini?Tokea tumempa jambajamba siku za kampeni mpaka leo anaiotea ndoto ya kutisha pale Magogoni jumba jeupe.
Maluweluwe ya vijana na wamama wa Mbeya yanamjia kila siku sasa hapo si mahali pake.Asije tu huku maana yale ya 2015 itakuwa x5.Halafu atakae lose ni ccm na serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
J

jimama26

JF-Expert Member
Jul 30, 2013
1,416
2,000
Na bora asifanye maana tayari tuna Rais wa mioyo yetu. Anamalizia matibabu sasa hivi.
 
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,454
2,000
Kwa jinsi nilivyomsikia akiwapiga bit TRA leo nakubaliana nawe, yaani hajui kwanini mapato yanashuka na hajijui kabisa kama yeye mkuda na maamuzi yake hayataki mjadala yeye anajifungia na kuamua.

Ila madaraka kiukweli ameyapenda mno na hakuna dalili atakubali hayakose.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwengeso

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
6,797
2,000
Sio kwamba hataki demokrasia, ukweli ni kuwa haiwezi. Ni kama anavyojifanya anakienzi kiswahili, ukweli ni kuwa lugha ya kiingereza inampiga chenga kuiongea kwa ufasaha. Hata sasa analitumia jeshi kwakuwa jeshi pia linadhani lina wajibu wa kuhakikisha rais aliyeko madarakani ana haki ya kushinda uchaguzi yeye na chama chake. Hiyo 2020 analitegemea jeshi na vikundi vya kihalifu kuhakikisha anatangazwa mshindi kwani hana uwezo wa kushinda kwa ushawishi.
tindo nitaendelea kutofautiana na wewe, siyo kwa hoja, ila kwa mtazamo wako chanya na uliojaa chuki dhidi ya Rais Magufuli, Serikali na Chama Tawala.

Hakuna hata mara moja umejadili kwa hoja zaidi ya kebehi na kejeli. Niamini ndiyo kiwango chako cha kushiriki majadiliano?

Isitoshe sijapata kusoma mada yako yoyote yenye kuleta mjadala kuhusu upande wa wanasiasa unaowawikilisha humu JF, ili tikashirikishana kupanua uelewa wa uwezo wa upande huo kuongoza nchi.

Nikirejea kwenye majibu yako:
Wasema kwamba:
1) Ni kama anavyojifanya anakienzi kiswahili, ukweli ni kuwa lugha ya kiingereza inampiga chenga, najiuliza kujua kiingereza ni msingi wa nini?
2) Sio kwamba hataki demokrasia, ukweli ni kuwa haiwezi[/[], je, demokrasia kwako maana yake ni nini na inatekekezwaje?

Nashukuru umerudi, nilijua kwa kile nilichokuambia jana ungerudi, na huu utetezi wako umejikita kwenye kile nilichokuambia jana. Kwangu mtu yoyote asiyeheshimu mifumo ya demokrasia hata afanye zuri gani hawezi kupata sifa toka kwangu. Hata akifanya jambo jema huwezi kuniona namsifia sana sana nitakaa kimya. Ninajua uko biased hivyo sitegemei uone mchango wangu wowote wa maana, hilo sio kosa langu ni juu ya udhaifu wako.

1. Kiingereza ni moja kati ya lugha zetu 2 kuu za Taifa. Yeye ameonyesha hataki kutumia kiingereza bali anakienzi kiswahili. Je kuchomeka maneno ya kiingereza kwenye hotuba zake kuna mantiki gani kama lengo ni kukienzi kiswahili?

2. Demokrasia yetu iko mpaka ndani ya katiba na vyama vya siasa vipo kisheria, inakuwaje azuie kazi halali za vyama vya siasa nchi nzima huku chama chake kikifanya kwa uwazi na kificho?

Suala la uchaguzi, ni dhahiri chaguzi zetu hasa toka awamu yake hii, box la kura haliheshimiwi na yote haya ni kutokana na mitazamo yake dhidi ya demokrasia.
 
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,700
2,000
Acha ujuha wewe! Fatilia kuhusu Rais George H.W. Bush (Bush Mkubwa) mbna alikuwa Rais wa muhula mmoja!

Shida ipo huku Dunia ya tatu, baada ya Mungu anayefata ni Rais.
Sijasema haiwezekani au haijawahi kutokea, nimesema ni kazi ngumu sana.

Bush alikuwa ni mtu mzito sana, ukiniuliza mimi nitakwambia alipewa Urais aivushe Marekani katika kipindi sensitive sana hasa kilichokuwa kinaendelea Urusi.

Kwa kuishupalia point hiyo nadhani mada yangu haujaielewa.
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,770
2,000
Sio kwamba hataki demokrasia, ukweli ni kuwa haiwezi. Ni kama anavyojifanya anakienzi kiswahili, ukweli ni kuwa lugha ya kiingereza inampiga chenga kuiongea kwa ufasaha. Hata sasa analitumia jeshi kwakuwa jeshi pia linadhani lina wajibu wa kuhakikisha rais aliyeko madarakani ana haki ya kushinda uchaguzi yeye na chama chake. Hiyo 2020 analitegemea jeshi na vikundi vya kihalifu kuhakikisha anatangazwa mshindi kwani hana uwezo wa kushinda kwa ushawishi.
Sema usemavyo, mdhihaki unavyojua na mchukie uwezavyo ila Kikatiba na Kimamlaka Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huyo ndiye Rais wako wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama nchini. Nimemaliza.
 
I

Isa khamisi

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
431
500
Kwa yoyote mwenye kufuatilia mienendo ya kisiasa na kiserikali atakubaliana na mimi kwamba Magufuli siyo mpenzi kihivyo wa demokrasia. Hili siyo tusi wala lawama, ni mtazamo wangu kuhusu mtazamo wake! Na hata yeye mwenyewe anasemaga mara kwa mara kwamba demokrasia inatuchelewesha!

Siku baada ya siku ameonekana kuegemea upande wa taasisi ya jeshi hadi kufikia kusuggest timu ya taifa itoke Jeshini. Hizi siyo kauli ya kubeza, anaamini kabisa kuwa ndiyo suluhisho la matatizo yetu yote. Huu ni mtazamo wake ambao unajadilika (kama tutaruhusiwa kujadili!)

Katika tafakari yangu namuona pia kama ni mtu ambaye hata madaraka aliyonayo angependa ayapate kwa njia nyingine ukizingatia kama nilivyotangulia kusema, siyo mfuasi mkubwa sana wa mfumo wa demokrasia.

Nakumbuka 2015 siku ya mwisho ya kampeni kule Mwanza, Kikwete alionekana kama anampandisha mori achangamke (tafuta clip wakati Kikwete anampa nafasi ya kuongea). Toka hapo amekuwa na miaka 5 ya kujizatiti kufikia ndoto yake ya kupata madaraka na kuongoza kwa mfumo alio comfortable nao zaidi.

Huwa siyo rahisi kumshinda Raisi aliye madarakani katika uchaguzi (incumbent President) hata awe ameboronga kivipi. Ni kazi ngumu sana hata kwenye nchi zenye demokrasia iliyokomaa. Nikitumia maneno ya kiingereza ambayo sidhani kama naweza kupata tafsiri sahihi naweza kusema 'the election is his to lose'.

Sitashangaa mwakani akiwatuma wengine wakafanye kampeni huku tukaambiwa yeye ana majukumu muhimu zaidi.

Baada ya hapo chacha!
afanye kampeni za nini wakati Ana control vyombo vyote vya utawala,kisheria,time ya uchaguzi,bunge tusidanganyane 2020 hakuna uchaguzi ni uchaguzi na maauwaji kwa wataokataa kusarenda.
 
Kaziutumishi

Kaziutumishi

JF-Expert Member
Aug 17, 2018
325
500
Nashukuru umerudi, nilijua kwa kile nilichokuambia jana ungerudi, na huu utetezi wako umejikita kwenye kile nilichokuambia jana. Kwangu mtu yoyote asiyeheshimu mifumo ya demokrasia hata afanye zuri gani hawezi kupata sifa toka kwangu. Hata akifanya jambo jema huwezi kuniona namsifia sana sana nitakaa kimya. Ninajua uko biased hivyo sitegemei uone mchango wangu wowote wa maana, hilo sio kosa langu ni juu ya udhaifu wako.

1. Kiingereza ni moja kati ya lugha zetu 2 kuu za Taifa. Yeye ameonyesha hataki kutumia kiingereza bali anakienzi kiswahili. Je kuchomeka maneno ya kiingereza kwenye hotuba zake kuna mantiki gani kama lengo ni kukienzi kiswahili?

2. Demokrasia yetu iko mpaka ndani ya katiba na vyama vya siasa vipo kisheria, inakuwaje azuie kazi halali za vyama vya siasa nchi nzima huku chama chake kikifanya kwa uwazi na kificho?

Suala la uchaguzi, ni dhahiri chaguzi zetu hasa toka awamu yake hii, box la kura haliheshimiwi na yote haya ni kutokana na mitazamo yake dhidi ya demokrasia.
Mkuu una moyo mkubwa, maswali yenyewe tu yanaonesha yamekaa kijinga jinga, imagine huyo puga anayeuliza yukoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaziutumishi

Kaziutumishi

JF-Expert Member
Aug 17, 2018
325
500
Sema usemavyo, mdhihaki unavyojua na mchukie uwezavyo ila Kikatiba na Kimamlaka Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huyo ndiye Rais wako wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama nchini. Nimemaliza.
Sawa mwambie ben saanane yuko wapi na PhD yake feki bado anaitumia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom