Elections 2020 Kuna uwezekano Magufuli hatafanya kampeni Uchaguzi wa 2020

ZULUECO

ZULUECO

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
587
250
tindo nitaendelea kutofautiana na wewe, siyo kwa hoja, ila kwa mtazamo wako chanya na uliojaa chuki dhidi ya Rais Magufuli, Serikali na Chama Tawala.

Hakuna hata mara moja umejadili kwa hoja zaidi ya kebehi na kejeli. Niamini ndiyo kiwango chako cha kushiriki majadiliano?

Isitoshe sijapata kusoma mada yako yoyote yenye kuleta mjadala kuhusu upande wa wanasiasa unaowawikilisha humu JF, ili tikashirikishana kupanua uelewa wa uwezo wa upande huo kuongoza nchi.

Nikirejea kwenye majibu yako:
Wasema kwamba:
1) Ni kama anavyojifanya anakienzi kiswahili, ukweli ni kuwa lugha ya kiingereza inampiga chenga, najiuliza kujua kiingereza ni msingi wa nini?
2) Sio kwamba hataki demokrasia, ukweli ni kuwa haiwezi[/[], je, demokrasia kwako maana yake ni nini na inatekekezwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kebehi za hawa watu hata kama ningekuwa mimi ndo raisi ningeongoza milele ili kuwakomoa tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwengeso

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
6,797
2,000
Nashukuru umerudi, nilijua kwa kile nilichokuambia jana ungerudi, na huu utetezi wako umejikita kwenye kile nilichokuambia jana. Kwangu mtu yoyote asiyeheshimu mifumo ya demokrasia hata afanye zuri gani hawezi kupata sifa toka kwangu. Hata akifanya jambo jema huwezi kuniona namsifia sana sana nitakaa kimya. Ninajua uko biased hivyo sitegemei uone mchango wangu wowote wa maana, hilo sio kosa langu ni juu ya udhaifu wako.

1. Kiingereza ni moja kati ya lugha zetu 2 kuu za Taifa. Yeye ameonyesha hataki kutumia kiingereza bali anakienzi kiswahili. Je kuchomeka maneno ya kiingereza kwenye hotuba zake kuna mantiki gani kama lengo ni kukienzi kiswahili?

2. Demokrasia yetu iko mpaka ndani ya katiba na vyama vya siasa vipo kisheria, inakuwaje azuie kazi halali za vyama vya siasa nchi nzima huku chama chake kikifanya kwa uwazi na kificho?

Suala la uchaguzi, ni dhahiri chaguzi zetu hasa toka awamu yake hii, box la kura haliheshimiwi na yote haya ni kutokana na mitazamo yake dhidi ya demokrasia.
Naamini uliyoyaandika hayawakilishi imani yako ila yanasukumwa na mtazamo wa upande wa pili.

Nikushangae tu wewe unayetukuza lugha ya Kiingereza wakati kuna jitihada za kukuza na kukieneza Kiswahili, lugha ya Taifa. Kwa hilo ni dhahiri una wajibu wa kujitambua, kujiamini na kuchukua hatua stahiki.

Kuhusu demokrasia, amini una tafsiri potofu na ni kwa sababu ya mtazamo wako hasi kuhusu Rais na Serikali.

Demokrasia haipimwi kwa kiwango gani wanasiasa wanapanda majukwaani.

Demokrasia ni utawala wa wengi kupitia wawakilishi waliochaguliwa kwa utaratibu uliokubalika. Kwa nchi yetu uwakilishi unaanzia mtaa/kitongoji hadi Taifa. Na wawakilishi wanawajibika, siyo kupanda majukwaani bali kushiriki vikao vilivyoainishwa kwenye Katiba ya JMT, kusikiliza, kupokea na kuwakilisha yatokanayo kwenye vikao vya juu vya maamuzi.

Uchaguzi hauwezi kuhesabika kutokuwa huru pale tu mshindani anapokosa kuchaguliwa na hatimaye kuilaumu Tume ya Uchaguzi. Na isitoshe mazingira ya kuandaa, kusimamia upigaji kura, kuhesabu na hatimaye matokeo kutangazwa yote huwa huru. Palipo na dosari katika mchakato mzima wa uchaguzi, mahakama ziko wazi kusikiliza malalamiko au madai ya aina hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
28,614

Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu.
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
28,614
2,000
Nimekutekenya kidogo tu lakini ulivyo ' Nyali ' angalia jinsi unavyotokwa na ' Mapovu ' namna hii. Pole sana hadi nakuonea huruma.
[/QUOTE

Kama wewe nilivyokujambisha ukaanza misifa ya kuduwanzi mara sijui mwanaume wa mara, sijui uduwanzi gani.
K
 
Liwalo na Liwe

Liwalo na Liwe

Member
Jul 6, 2012
40
95
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Naitazama Tanzania ya miaka 15 mpaka 20 iliyopita. Nimejifunza na kushuhudia mengi. Tulikuwa na nchi ambayo ilikuwa na matatizo mengi na makubwa, ni ukweli ulio wazi matatizo tuliyo kuwa nayo kila mtu aliyashuhudia. Hiki kinachoitwa demokrasia leo ndo kilikuwa kiboko kilichotumika kumpiga kisawasawa mwananchi was chini. Hiki kiboko ndo kilichotumika kuhifadhi maharamia serikalini, wauza unga, meno ya tembo, ujambazi, ukosefu wa maji has a dar es salaam, mikataba mibovu ya madini, huduma mbovu muhimbili na kukosekana kwa vifaa muhimu, yapo mengi sana yanayoonekana kwa macho. Tulichokikosa nchi hii miaka mingi siyo hicho kinachoitwa demokrasia. Maendeleo kwanza mambo mengine baadae, rais Bora ni mwenye dhamira ya kutenda mema ya nchi yenye kuonekana mambo ya kupewa matumaini yasiyokuwa na utekelezaji yalishapita. Ahadi na Utekelezaji ni msingi wa uaminifu. Uwezo wa jamaa wa kutekeleza ahadi zake unatosha kumpa trust ya majority, wanaopiga porojo waendelee kutafuta visingizio tu, mwenzenu anaendelea kutenda na kuaminiwa. Mtamkuta ikulu asubuhi na mapema, watakao mchagua ni wengi kuliko wasemaji wa maneno yasiyokuwa na utekelezaji. At the end trust is earned when actions meet words
 
samora10

samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,450
2,000
Kwa yoyote mwenye kufuatilia mienendo ya kisiasa na kiserikali atakubaliana na mimi kwamba Magufuli siyo mpenzi kihivyo wa demokrasia. Hili siyo tusi wala lawama, ni mtazamo wangu kuhusu mtazamo wake! Na hata yeye mwenyewe anasemaga mara kwa mara kwamba demokrasia inatuchelewesha!

Siku baada ya siku ameonekana kuegemea upande wa taasisi ya jeshi hadi kufikia kusuggest timu ya taifa itoke Jeshini. Hizi siyo kauli ya kubeza, anaamini kabisa kuwa ndiyo suluhisho la matatizo yetu yote. Huu ni mtazamo wake ambao unajadilika (kama tutaruhusiwa kujadili!)

Katika tafakari yangu namuona pia kama ni mtu ambaye hata madaraka aliyonayo angependa ayapate kwa njia nyingine ukizingatia kama nilivyotangulia kusema, siyo mfuasi mkubwa sana wa mfumo wa demokrasia.

Nakumbuka 2015 siku ya mwisho ya kampeni kule Mwanza, Kikwete alionekana kama anampandisha mori achangamke (tafuta clip wakati Kikwete anampa nafasi ya kuongea). Toka hapo amekuwa na miaka 5 ya kujizatiti kufikia ndoto yake ya kupata madaraka na kuongoza kwa mfumo alio comfortable nao zaidi.

Huwa siyo rahisi kumshinda Raisi aliye madarakani katika uchaguzi (incumbent President) hata awe ameboronga kivipi. Ni kazi ngumu sana hata kwenye nchi zenye demokrasia iliyokomaa. Nikitumia maneno ya kiingereza ambayo sidhani kama naweza kupata tafsiri sahihi naweza kusema 'the election is his to lose'.

Sitashangaa mwakani akiwatuma wengine wakafanye kampeni huku tukaambiwa yeye ana majukumu muhimu zaidi.

Baada ya hapo chacha!
So what is the point here?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzalendo2015

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
5,012
2,000
Sio kwamba hataki demokrasia, ukweli ni kuwa haiwezi. Ni kama anavyojifanya anakienzi kiswahili, ukweli ni kuwa lugha ya kiingereza inampiga chenga kuiongea kwa ufasaha. Hata sasa analitumia jeshi kwakuwa jeshi pia linadhani lina wajibu wa kuhakikisha rais aliyeko madarakani ana haki ya kushinda uchaguzi yeye na chama chake. Hiyo 2020 analitegemea jeshi na vikundi vya kihalifu kuhakikisha anatangazwa mshindi kwani hana uwezo wa kushinda kwa ushawishi.
tindo
Unachosema ni sahihi kabsaa!
Magufuli kwa hakika ame-prove failure kwenye Utawala Bora(Good Governance).
Ushindi wake wa 58% mwaka 2015 ulimtia kiwewe na hata report zilizoonesha kushuka kwa umaarufu wake/kuchukiwa na Watz kulizidi kumwongezea HASIRA na majibu yake tumeyaona kwenye Uchaguzi wa SM!
Hataki kurudia makosa ya 2015 ya kuambulia kura kiduchu hivo kuumbuka mchana kweupe…!
Ninachokiona ni kwamba coming GE~2020 his next move will be similar to what he played kwenye LG Election. Kama mtakumbuka juzi wameajiriwa WANAJESHI WENGI SANA KWENYE SEKTA ZA UMMA ikiwemo Halmashauri za Mikoa na Wilaya…!
Hizo ni strategies za kujiweka sawa! Lakini Watz lazima wajur kuwa Magufuli amekuwa akipendelea sana kuvaa MAVAZI YA KIJESHI na hili si kwa bahati mbaya! He's sending a message to his opponents and Tanzanians as a whole kwamba AKISHINDWA KWA KURA anaweza kulitumia Jeshi kutwaa nchi as a Coup d'e tat!!
 
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
5,009
2,000
Unafikiri atakuwepo ?
 
B

Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
5,266
2,000
Swali fikirishi kwanini ameiambnia dunia kwamba uchaguzi utakuwa huru kipi kimebadirika kwenye tume ya uchaguzi
 
G

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
4,999
2,000
Kwa yoyote mwenye kufuatilia mienendo ya kisiasa na kiserikali atakubaliana na mimi kwamba Magufuli siyo mpenzi kihivyo wa demokrasia. Hili siyo tusi wala lawama, ni mtazamo wangu kuhusu mtazamo wake! Na hata yeye mwenyewe anasemaga mara kwa mara kwamba demokrasia inatuchelewesha!

Siku baada ya siku ameonekana kuegemea upande wa taasisi ya jeshi hadi kufikia kusuggest timu ya taifa itoke Jeshini. Hizi siyo kauli ya kubeza, anaamini kabisa kuwa ndiyo suluhisho la matatizo yetu yote. Huu ni mtazamo wake ambao unajadilika (kama tutaruhusiwa kujadili!)

Katika tafakari yangu namuona pia kama ni mtu ambaye hata madaraka aliyonayo angependa ayapate kwa njia nyingine ukizingatia kama nilivyotangulia kusema, siyo mfuasi mkubwa sana wa mfumo wa demokrasia.

Nakumbuka 2015 siku ya mwisho ya kampeni kule Mwanza, Kikwete alionekana kama anampandisha mori achangamke (tafuta clip wakati Kikwete anampa nafasi ya kuongea). Toka hapo amekuwa na miaka 5 ya kujizatiti kufikia ndoto yake ya kupata madaraka na kuongoza kwa mfumo alio comfortable nao zaidi.

Huwa siyo rahisi kumshinda Raisi aliye madarakani katika uchaguzi (incumbent President) hata awe ameboronga kivipi. Ni kazi ngumu sana hata kwenye nchi zenye demokrasia iliyokomaa. Nikitumia maneno ya kiingereza ambayo sidhani kama naweza kupata tafsiri sahihi naweza kusema 'the election is his to lose'.

Sitashangaa mwakani akiwatuma wengine wakafanye kampeni huku tukaambiwa yeye ana majukumu muhimu zaidi.

Baada ya hapo chacha!
Amefanya kampeni tangu alipoingia madarakani kila siku yuko live kwenye tv hata kwa matukio ya kawaida. Pia.ikumbukww nec ni mali yake binafsi
 
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,700
2,000
Je, haya maneno yanaenda kutimia? Tusubiri tuone.
 
Top Bottom