Kuna uwezekano Hayati Magufuli alikopa ili kulipa Mishahara? Dkt. Mpango afafanue Mikopo ya Trilioni 29 kwa miaka 5 ilifanya nini

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kwa mujibu wa Takwimu zinazotolewa Sasa na makada, Mawaziri waliopita na watu tofauti Magufuli ndio Raisi aliyekopa fedha nyingi kuliko Rais yoyote Tanzania ingawa kaongoza muda mfupi. Je, fedha zake alifanyia Nini? Takwimu hazidanganyi.

Inasemekana alikopa trilion 29 kwa fedha hizo zilitosha kujenga reli Dar to Kigoma pamoja na bwawa la Mwalimu Nyerere, kununua ndege na chenchi zingebaki tukagawana.

Sababu reli ingegarimu tilion 16, bwawa la nyerere tilion 6. Ukarabati shule kongwe bilion 100 Lakini mpaka Sasa miradi hiyo haijafika kokotee. Je, fedha ziliilipigwa? Au zilienda wapi. Tupate uhalisia.

Mama juzi kachukua Trilion Moja tu. Lakini kila Mtanzania Anaweza kuona kwa macho pale alipo madarasa, shule mpya na zahanati na vituo vya Afya kila kona.

Hapa hatumsimangi Ila tuwe wakweli. Ukisema stendi ya Mbezi na ya dodoma. Takwimu hazidanganyi. Stendi ya mbezi imegharimu bilion 50 tu. Tilion 1 ingejenga stendi Kama hizo 20 tanZania nzima. Sasa t.. 29 alifanyia Nini? Soko la Dodoma na stendi gharama yake NI billion 35 tu. Yani Tillion 1 NI soko na stendi Kama ya dodoma 30.

Na soko na stendi ya Mwanza mradi aliusitisha kabisa mama ndio kaanza nao. Jamani tilion sio mchezo 29 alipeleka wapi? Dalaja la wami NI b 66tu na kaliachs bado. Tilion NI bilion 1000. Faraja la busisi NI billion 600. Hilo ndio nusu tilion. Kifupi ukichukua madaraja. Yote, masoko na stendi alipojenga na kufikia bado haifiki tilion 1. Hizo 28 zilifanya Nini.

Kikwete miaka 10 tilion 20. Kaunganisha kilometa 10,000 za Rami ambazo gharama yake NI Tillion 9 hivi. Yani unaona.
Yeye hajajenga hata km 1000tu za Rami. Sasa hizo tilion 29 tulipigwa?

Mnakjibu mje na takwimu halisi sio ushabiki. Usiwe tulipewa mikopo ya kichina. Unachukua billion 100 unaandikiwa billion 10000.
 
Tumia akili kidogo basi.

Hivi wewe huoni madaraja aliyoyajenga Magufuli? Stendi mpya mikoa karibu yote na wilaya zake huzioni? Ukianzia na ya mbezi Dar?

Huoni miladi ya maji kila kaya? Huoni maji yalovutwa kutoka ziwa Victoria kwenda Tabora Nzega ,Shinyanga,Singida maji kila kaya inabomba?

Mimi mwenyewe ni shahidi maji hayo yamepita kijijini kwetu na kwenye ardhi yetu na sisi tumevuta maji na umeme pia.

Ukuta wa Mererani hata huo huuoni?Sasa ulitaka hizo pesa zitumike huko mijini peke yake?

Zahanati na vituo vya afya kila kata na kijiji nazo pia huzioni? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Ungesema Kwa upande wa Watumishi hasa waalimu kwenye nyongeza za mishahara na madaraja aliyapa kisogo pamoja na Demokrasia ya kweli.Ni hayo tu .

Kwenye kuleta maendeleo Magufuli hana mpinzani kuanzia serikali ya pili hadi ya sasa hana wa kumlinganisha naye.

Magufuli alituheshimisha.
Dunia ilisimama.Dunia ilitambua uwepo wa Serikali ya Tanzania .
 
Kwa mujibu wa Takwimu zinazotolewa Sasa na makada, Mawaziri waliopita na watu tofauti Magufuli ndio Raisi aliyekopa fedha nyingi kuliko Raisi yoyote Tanzania ingawa kaongoza muda mfupi. Je fedha zake alifanyia Nini...

Hoja hii ifungamanishwe na madai ya katiba mpya.

Kufanyike total audit kwa mapato na matumizi yote katika awamu ya tano.

Pesa zote zifahamike zilikwenda wapi na hatua stahiki kuchukuliwa.
 
Tunaendeshwa kipumbafu,kama mwenda alikopa vibaya wasaidizi wake wooote wajieleze!! Kuanzia makamu wake,waziri mkuu wake,waziri wake wafedha,spika alokuwepk nk. nk.

Hatuwezi kudanganywa kama wajinga kwamba tunajenga kwa pesazetu huku kwakificho serikali inakopa vibaya mmmno!!

Aloomba msamaha aombe ili asinyang'anywe ugali lakini sisi tunadai uwazi kuhusu nchi ikopavyo.
Hatuna mbunge wakupigia kelele hili wananchi tupige kelele wenyewe.
 
Ujenzi Chatto, makao makuu Dom, ununuzi ndege cash' elimu bila ada, ujenzi meli, rada, fly over, mambo mengi ila kama Urais maana yake kukopa na kujenga unavyojisikia, ni tatizo!
 
Back
Top Bottom