Kuna ulazima wa Tanzania kuwa na Shirika la Ndege?

franktemu123

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
1,400
1,451
Wadau nimekuwa nikijiuliza kwani ni lazima kama Taifa tuwe na Shirika la ndege ? maana kwa sasa hatuna NGUVU KAZI ya KUTOSHA katika SEKTA husika vinginevyo tutashuhudia ajali, delay, cancellation zitakuwa za kumwaga. Ni bora tuwekeze kwenye GESI tuwe na tuna-EXPORT huko Abroad kuliko kung'ang'ania Ndege
 
ni kweli ndugu frank ni bora tukajikita kwenye utalii na gesi hayo mengine tuwaachie wengine wakina EMIRATES, TURKISH, maana wao ndo wenye ni nidhamu ya biashara na WELEDI katika wafanyayo
 
Tunalazimisha matokeo yake tuna ndege moja ya mkopo Lakin wafanyakaz 300

Kufanya makosa haimaanishi kuwa hatuwezi...

Kutokujifunza katika makosa ndio kitu kinachotugharimu...

Kwa nchi kama yetu inayotegemea sekta ya utalii kama moja ya vyanzo vya bajeti ya serikali tunapaswa kuwa na shirika thabiti la ndege...
 
watanzania wengi wanadhani kuanzisha shirika la ndege ni kama kuanzisha mabasi ya UDA. Kimsingi naona bado hatujaamua kuwa serious kwenye biashara ya ndege watu wamekaa kusubiria PER DIEMS na ALLOWANCES tu na si katika ubunifu, tizama hii (www.atcl.co.tz) kisha angalia www.fastjet.com ndo utaelewa ninamaanisha nini
 
Kufanya makosa haimaanishi kuwa hatuwezi...

Kutokujifunza katika makosa ndio kitu kinachotugharimu...

Kwa nchi kama yetu inayotegemea sekta ya utalii kama moja ya vyanzo vya bajeti ya serikali tunapaswa kuwa na shirika thabiti la ndege...

Kuendeshaa biashara ya ndege sio lelemama,inahitaji nidhamu ya hali ya juu ya pesa,kwa sasa hatuna nidhamu hiyo hivyo hatuwez
 
Kuendeshaa biashara ya ndege sio lelemama,inahitaji nidhamu ya hali ya juu ya pesa,kwa sasa hatuna nidhamu hiyo hivyo hatuwez

Sio kwamba Tanzania haijawahi kuwa na hiyo nidhamu hapo awali hivyo hicho si kikwazo mkuu...

Tulikuwa na shirika imara kwa muda mrefu tu kabla halijaporomoka na kuporomoka huko kuliambatana na kupotea kwa viwanda na mashirika mengine pia...

Kwa sasa serikali yetu imelala kila mahali labda tuingoje hadi hapo itakapozinduka tena...
 
nimewahi kuona Waganga wa Kienyeji toka TZ maeneo ya Johannesburg, Durban na Lusaka, Harare, Nairobi na Mombasa kwa nini tusianzishe vyuo vya kufunza Waganga wa Kienyeji halafu tuwa-export mpaka Ulaya na huko USA?
 
Duuh we andreakalima ndo kusema unataka tuanze kupeleka waganga wetu wa kienyeji huko ughaibuni sio? jamani JF full raha. Nionavyo sisi kumiliki shirika la ndege bado sana
 
kuanzishwa kwa University of Dodoma kutabadilisha kabisa hali ya uchumi wa Tanzania japo serikali inabidi ifanye jitihada za makusudi katika kuwatumia wataalamu wanaozalishwa hapo kwa kuwapa nafasi za kazi na kutengeneza mazuri ya mitaji kwa hao Graduates. Maana naamini hao vijana wakitoka hapo watakuwa wameiva haswa tayari kuingia kuzalisha ajira kwa vijana wenzao na wale wachache wataoajiriwa
 
Hili shirika lipo ili mradi watu wachote hela. Biashara ya ndege ni ngumu sana na inaweletea hasara hata kampuni ambazo ziko serious na hazina matatizo kama yetu.
 
Wabunge wanakomalia viwanja vya ndege vijengwe kwenye majimbo yao....kama kondoa kiwanja cha nini..dada yetu Mh.Mhita.Msosi tunapiga mmoja tu kwa siku..hiyo nauli ya ma bus ni kazi sembuse ya ndege...kilimo anga ilikufa siku nyingi na ndege yake imeoza pale ARK AIRPORT kama nzige au ndege kolekole wakija tutakodi kutoka kenya au Addis.
 
Wadau nimekuwa nikijiuliza kwani ni lazima kama Taifa tuwe na Shirika la ndege ? maana kwa sasa hatuna NGUVU KAZI ya KUTOSHA katika SEKTA husika vinginevyo tutashuhudia ajali, delay, cancellation zitakuwa za kumwaga. Ni bora tuwekeze kwenye GESI tuwe na tuna-EXPORT huko Abroad kuliko kung'ang'ania Ndege
serikali inunue share katika mashirika yaliyopi yaani fastjet na Precisionair (inunue shares za KQ) nguvu kazi zipo tayari kule
 
nionavyo Tanzania hatuna haja ya kuwa na ndege bora tubaki na UDA yetu ndio tunayowaweza kwa ufanisi
 
Ndege tujifunze kwa hawa ndugu zety wa Kenya. Kila mwaka wanapata hasara. Tanzania kamwe tusijiingize kwenye hii biashara.
Fastjet watatuua kama alivyokufa Precision
Kina emirates, etihad, turkish, qatar, eygpt, fly dubai, oman air hao watatuuuua mara mia
 
Kusema ukweli kama Utalii ukipewa nguvu na watu wakajua umuhimu wake unaweza kuchangia bajeti kubwa kuliko sekta nyingine yoyote kutokana na vyanzo vya kitalii tulivyonavyo ukilinganisha na nchi nyingine Duniani.Tabu ipi?hakuna ambaye hatambui uhusiano wa biashara ya ndege na utalii ni kama mume na mke.Leo hii kwa mwaka moja watalii wanaoingia Tanzania ni chini ya milioni moja ukilinganisha na nchi zingine ambazo vyanzo vya kitalii ni vichache.Kutokana na vyanzo vyetu kwa mwaka inapaswa kuingia watalii wasiopungua milioni 5.Wazee walinena huwezi kujua future wakati haujui past ilikuwaje

Hatupendi kujifunza kutokana na makosa

Biashara ya ndege ni biashara yenye risk kubwa sana na hasa ukizingatia ndege ndiyo injini kuu kwenye hii biashara lakini kwa kipindi kirefu kumekuwa na matatizo mengi katika uendeshaji wa hili shirika.

MATATIZO:
1)Huwezi kuendesha shirika la ndege na kuleta faida nzuri kama ni part ya siasa.Siasa siku zote lazima iwe peke yake na biashara iwe peke yake japo vyote vinaweza kuwa ndugu lazima sumu kubwa kwenye biashara ni kumuachia ndugu aiongoze biashara siku za usoni hautajua mchawi wako ni nani
2)Uendeshaji wa shirika la ndege ni mithili ya timu ya mpira.Timu ya mpira si jina bali ni wachezaji huwezi kusema unaanzisha timu wakati hujui nani atacheza.Hiyo haiwezi kuwa timu na hata upatikanaji wa wachezaji lazima uwaandae.Huwezi ukaendesha shirika la ndege ambalo litaleta faida mathubuti kama hujawekeza kwenye watu.Leo hii tunasomesha mainjinia wa ndege South Africa ambao kila mmoja gharama yake ni dola laki moja je tutasemesha wangapi ili tupte watu wa kutosha.Tangu mwanzo kama shirika llilipaswa kuisukuma serikali kujenga chuo kikuu cha masuala ya Aviation and Aerospace engineer ambacho kingeandaa wataalam mathubuthi katika fani mbalimbali ikiwemo Airline management and organization of airline enterproses watalaam hawa wamekosekana na ndiyo maana matokeo yake tumeyaona
3)Shirika kama shirika lazima liundwe na timu ya watalaam waliobobea katika masuala ya uendeshaji wa mashirika ya ndege watu kama CEO wana play role kubwa sana tatizo kubwa kumekuwa hakuna njia mbadala wa kuwapata hawa watu.Ukiangalia kwenye matangazo ya kazi za serikali utakuta CEO lazima uwe umefanya kazi miaka 10 kitu kimoja hatutatumbia kuwa na uzoefu mkbwa katika eneo Fulani haimaanishi wewe ni innovative.Mashirika ya ndege ni sensitive sana hapa hatuongelei mashirika ya kilimo.Tunaongelea mashirika yenye assets ambazo risk yake kubwa sana mfano ajali

SULUHISHO
Nchi kama nchi inahitaji sana kuwa na shirika la ndege kwani ni chanzo kizuri cha mapato na ajira.Mashirika kama haya ni rahisi kutoa ajira zaidi ya 10000 mfano mdogo Ethiopian airline imetoa ajira za kudumu 17000 na bado inaongeza idadi kwa siku za usoni

Hakuna kinachoshindikana chini ya jua

1) Lazima upatikane uongozi wenye kujua nini unafanya na nini unataka kuachive.Mfano kwa CEO asipatikane eti kwa kuwa amefanya Air Tanzania kwa miaka ishirini hayo ni makosa.CEO apatikane kwa international biding itangazwe nafasi pote duniani ili kupata mtu mwenye greatest archivement kwenye uendeshaji wa ndege potelea mbali watume CV watu 10000 lakini achaguliwe mmoja tu.Na huyu mtu afanye kazi kwa mkataba wa miaka miwili akishindwa kufikia malengo basi anaachi kiti.Mimi sioni tabu kama leo tukimlipa hata dola za kimarekani laki mbili CEo anayeweza kuingiza faida ya dola milioni 500 kwa mwaka.Mfano mdogo tuangalie club kubwa za mpira wa miguu duniani kocha haijali kuingia mkataba na kocha wa milioni 20 dolla ili elete ushindi akishindwa straight away anaachia kiti kuwapa watu wenye uwezo

Tukishindwa kumpata CEO kwa njia hii basi tuangalie airline gani imefanya vizuri zaidi duniani tumface CEO wao tumpe dau zaidi ili aje kufanya wonders and this is what we call business hakuna undugu na sio jambo geni wakati Bill Gate alipoanzisha Cascade investment wapi alipata fund manager ambaye alimuingizia faida kubwa zaidi?alimchukua kutoka kwenye kampuni nyingine na kumuongeza dau kwa upande mwingine ndivyo thamani ya ahira inavyotakiwa kuwa
2.Shirika letu linapaswakuwa na vision plan kwa mfano malengo ya miaka 10,malengo yamiaka 20.Hili litachochea kazi ya watu kuhakikishia wanafikia malengo mfano malengo ya miaka mitano kutua kwenye viwanja vyote Africa na siyo tu kutua bali kuwa na kiwango cha faida ambacho shirika litapigana kufa na kupona ili lifikie kiwango

3.Ili kulifufua shirika tunaweza kuanza na ndege zenye daraja moja tu pili lazime watumie ndege zenye umbo jembaba kwa kizungu (short-haul flights which complements the range of narrow-body)Kwa nini hizi ni bora kwa mashirika yetu gharama za uendeshaji wake ziko chini ukilinganisha na ndege zenye maumbo mapana kwa mfano kwa kuanzia shirika letu linaweza hata kuanza na ndege kumi aina ya Sukhoi Superjet 100 capacity yake ni abiria 100 kwa sasa bei ya ndege moja ni dola za kimarekani milioni 35 sifa za hizi ndege ni unafuu wa gharama katika uendeshaji
4 Shirika lazima liachane na tabia ya kukodi ndege kukodi ndege moja ya airbus kama linavyofanya kwa sasa gharama zake ni milioni nne dola za kimarekani hakuna umuhimu lijikusanye hata kwa mikopo lipate ndege zake
5)Faida za kununua ndege kwa uwingi(bulk procurement) kuna discount kubwa inatolewa na isitoshe ndege mpya pia ni nafuu zaidi kuziendesha hazina matatizo ya kiufundi pia kuna efficient interm of fuel,training,maintanance pili shirika kama lilinunua ndege hizi kwa discount linaweza kuzitumia kwa muda wa miaka 10 then likaziuza kwa bei kubwa hapo tunazidi kuongelea faida

6)Pia kuna gharama kubwa za kuendesha airline kupitia traditional hubs kama JK international airport kuna gharama nyingi kama handling nk shirika linaweza kuopt secondary hub (airport ndogo) mfano ndege inakwenda Rwanda sio lazima tutumie Kigali international airport inaweza kutumia airport ndogo karibu na Kigali kwa kawaida hizi zinaitwa secondary hub gharama zake za aircraft handling zipo chini sana ukilinganisha na viwanja vikubwa na pia ziingie mfumo unaitwa offload turnaround(yani ndege inafika inashusha na kugeuza)itaounguza gharama nyingi sana za kupack pale mpaka asubuhi

7)Mashirika mengi sana ya ndege yalikufa kutokana na gharama kubwa za mafuta ya ndege.Shirika lazima liwe na mikakati ya muda mrefu sana wa kibiashara.Moja lazima liwe na storage yake yenyewe yenye capacity kubwa sana mfano kipindi hiki wakati mafuta yameshuka sana duniani lazima inunue mafuta kwa wiki inadvance hata kwa miaka miwili kwa kufanya hivyo itaokoa pesa nyingi sana kwenye mafuta kwa kipndi chote hicho

7)Gharama zingine zinaweza kupunguza kwa kuanzisha database nzuri ambayo itaondoa ulazima wa kuwa na agent kila kitu kifanywe online bila ya kuwa na agenti au ofisi za ziada na gharama za majengo,kuwa na system ya wafanyakazi wenye kazi mbalimbali mfano hawa cabin crew wanaweza pia kucheki tiketi pale getini pamoja na kusafisha ndani ya ili kupunguza watu

Hayo ni machache tu ila yapo mambo mengi sana yanayoweza kulisimamisha shirika letu kidedea
 
Shirika la ndege si lele mama. Unahitahi kutoa siasa nje ya operations za kila siku. Kwa viongozi mchwa wetu, shirika litakufa kesho yake
 
sioni ulazima wa kuwa na shirika la ndege kwa sasa ukizingatia majirani zetu RWANDA, KENYA, ETHIOPIA na SOUTH AFRICA wanatuhudumia vyema tu ni bora tujikite kwenye KUCHAKATA GESI na pengine UMBEA maana labda tunayoweza
 
Back
Top Bottom