MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,752
- 5,497
Japo wanasayansi wachache wanabisha, lakini ni Ukweli usiofichika kwamba Elimu Dhana ya Uibukaji Ina utata mwingi kuliko Ukweli...
Pia ina Maswali mengi yaliyo wazi kuliko majibu...
Kila mtu anapofundishwa shule ya msingi na sekondari, Hushtuka anaposikia kwa Lugha Nyepesi kuwa Mwanadamu alitokana na Nyani/Sokwe/au mnyama wa jamii hiyo.
Tena hii ni kurahisisha tu watoto na vijana wangechanganyikiwa kabisa kama wangeanzia kuambia Huyo sokwe alipotokea.
Huyu mzee anaitwa Darwin ndiye muenezaji mkuu na anachukuliwa kama ni Muasisi wa mthana hii ya uibukaji...
DUNIANI kuna kitu kinaitwa INDOCTRINATION
Hii ni hali ya Kufundisha na kulazimisha kitu kwa njia ya Imani bila kuacha mwanya wa kuhoji na kujiridhisha kisayansi.
Hii hutumika sana na sisi watu wa Imani katika kukukubali vitu kama uwepo wa Miujiza,Uweza wa Mungu, na Masomo mbali mbali ya kidini.
Zoezi hili hufanana 100% na kinachofanyika mashuleni kuwaaminisha watoto na Vijana mwanadamu Kaibuka tena bila nyama za kushiba ambazo kwa uwezo wake kiakili hangeweza kufahamu.
Kufundisha Huku hakuna tofauti na Kumfundisha Mtoto Shuleni kuwa Mwanadamu aliumbwa na Mungu bila kuwa na maelezo ya kushiba.
NINI KIFANYIKA NA WEWE KARIBU KWA MAWAZO YAKO....
Kwa kutambua hilo ingekuwa ni vizuri kama
1:Kama kufutwa ikishindikana basi Nadharia zote mbili MTU KAIBUKA KUTOKA KWA SOKWE na MTU KAUMBWA NA MUNGU zifundishwe kwa uzito sawa ila kama mawazo mawili kinzani.
2:Yote mawili yatolewe kabisa na yaanze kufundishwa mtu akiwa tayari amejitambua na uwezo mkubwa wa kuhoji na kujifunza.
DONDOO ZA ZIADA
Kwa kutambua utata uliojificha katika Dhana hii, Kuanzia mwaka 2019 nchini uturuki dhana hii inafutwa rasmi katika vitabu vya historia na Baiolijia. Mwanafunzi atajifunza haya akiwa Chuo na uwezo mkubwa wa kuhoji na kutafakari vitu tata ya kisayansi na uvumbuzi.