Kuna ulazima dhana ya "Human Evolution" ifutwe shule ya msingi hadi form six

Kuna ulazima dhana ya "Human Evolution" ifutwe shule ya msingi hadi form six

Yaani MM unasema binadamu alitokana na nyani?
Unasema hivyo kwa lengo LA kupotosha watu au hata wewe mwenyewe huelewi maana ya evolution?
Mkuu unasema evolution ni imani? Hebu niambie ni imani ipi inayo exist kwa evidences na inayoruhusu kukosolewa?

Kwa mtazamo wako, masalia ya watu wa kale yaliyopatikana Africa kama vile fuvu la Olduvai yalitokea wapi?

Tatizo moja la hizo dini zenu ni kuwafanya watwana wa fikra.Kama ingekuwa ni Zimbabwe ndio wameikataa evolution sijui kama ungeanzisha huu uzi. Lakini kwa kuwa waturuki wameshafikiria kuikataa evolution, wewe unaona mawazo yao ni sawa.

Mimi nadhani ni wakati wa kuacha kudanganya watoto kuwa Mungu ndiye aliyetuumba.

Nadharia ya creationism imejaa uongo mtupu.Mfano ni inaposema mwanamke alitoka kwenye ubavu wa mwanamke ilihali ukweli ni kwamba mwanaume ndiye aliyetoka kwenye uke wa mwanamke.
 
Nilipoona tu unasema wanadamu walitokana na nyani nimeishia hapohapo kusoma. Wewe ni miongoni mwa wale ambao hamkuelewa mnasoma nini shuleni au mwalimu wako aliye kufundisha evolution alikua kiazi. Kwakua elimu haina mwisho unaweza kupata mwanga kidogo hata kwa kusoma wikipedia jaribu kusoma tena ukiwa na open mind. Weka hisia zako na maoni yako pembeni ukitaka kuujua ukweli na ku enjoy science, vinginevyo umevamia vitu vilivyo uzidi ubongo wako uwezo
 
Suala jingling gumu ambako linaonyesha kipindi cha Adams na Hawa, walikuwepo watu wengine ni pale Kaini anapofukuzwa mbele za uso wa Bwana, alienda katika nchi ya mbali na kuoa mke na kuzaa watoto. Baadhi ya wataalamu wa dini wanadai kuwa, kwenye Biblia wanawake walikuwa hawahesabiki, hivyo hao ni uzao wa Adam. Tulijibu hili pia.
 
Hata mi nimesikia mipango ya Uturuki. Mimi ni nakuunga mkono moja kwa moja ushauri wako kuwa tuyafundishe masuala haya kwenye watu wenye uwezo wa kuchambua mambo hasa kuanza A-Level.
Mimi ni mkristo, hata hivyo kwa mtazamo wangu theory ya evolution ni bora zaidi kuliko ile ya uumbaji (creation). Ukiikataa theory ya evolution, kataa pia kutoweka kwa dinosaurs, kubali kuwa mapiramidi ya Misri yalijengwa na waarabu.
Sasa swali, kama ukifuatilia mtiririko wa uzao wa mwanadamu tangu Adamu hadi Yesu Kristo ni miaka 2000 na tangu Yesu Kristo ni miaka 2017 na jumla ni miaka 4017. Je unakubali kuwa mwanadamu wa kwanza aliishi miaka 4000 iliyopita pekee? Wale Red Indians walifikaje Amerika ndani ya muda huo mfupi wakaenea kote? Wahindi weusi (Dravidian na Pre-Dravidian) nchini India na Sri Lanka walitoka wapi? Wale Aborigines wa Australia na Visiwa vya Pacific walitokea wapi?
Umesahau tangu Adam hadi Gharika.
Kumbuka kabla ya Nuhu kuzaliwa alikuwa ameshawahi kuwepo Methusela mwenye miaka zaidi ya 990
kumbuka pia huyu ni mtukuu wa adam ambae adamu mwenyewe aliishi miaka zaidi ya 900.
Kwa kufuata geneology ya kipindi kile utakuta umeruka takribani miaka mingine 2000
 
Hbrn za asubuhi. ULIYEETA HII HABARI NAKUPONGEZA MNO!
Me naona wangufuta kbsaaa hii story eti binadamu alianza kama nyani!....ndo imefanya wazungu kutudharau hadi leo na kutuona waafrika kama bdo tunafanana na nyani...na pia, imetufanya waafrika kutokujua our real identity! Kwamba chanzo chetu ni wapi,....sasa hawa jamaa wadhungu wanasema tulitokana na nyani, na kwa vile waafrika tusivopenda kufanya research zaaidi, tumeishia hapo!....
Tena inaonekana wazungu wengine wanajifunza katika series ya evolution alipitia kuwa mwafrika alafu mwafrika akaevolve kuwa mzungu.
Anti-Patrick_Ewing_Evolution_Image.jpg
 
Hivi kweli sisi wote tulitokea kwenye zao wa Nuhu ndo tukasambaa dunia nzima ndani ya kipindi kifupi cha miaka 3000 pekee? Hivi utofauti huu mkubwa ungwezekana ndani ya muda mfupi kiasi hicho?
Yale mafuvu yanayogunduliwa yenye umri mkubwa yanayodaiwa ni wanadamu, ni ya wanyama gani sasa?
Inawezekana hatujakubaliana kiini cha ugaidi wetu lakini kwa mwanahistoria mzuri anakubali kuwa, wanadamu hat ukubwa Hivi tulivyo na ndiyo maana wanaeleza kuwa kadri muda unavyokwenda wanadamu watazidi kuwa wazuri sana kutokana na teknolojia kubwa katika uzalishaji wa vyakula vyenye afya kwa binadamu, mimba na wanyama.
 
Umesahau tangu Adam hadi Gharika.
Kumbuka kabla ya Nuhu kuzaliwa alikuwa ameshawahi kuwepo Methusela mwenye miaka zaidi ya 990
kumbuka pia huyu ni mtukuu wa adam ambae adamu mwenyewe aliishi miaka zaidi ya 900.
Kwa kufuata geneology ya kipindi kile utakuta umeruka takribani miaka mingine 2000
Vita update vya dini, vinaeleza watu wote walikufa isipokuwa familia yake. Sasa na wewe unakubali Kirahisi rahisi hivyo kuwa hao jamaa uzao wao ndio ulikuja Afrika wakageuka kuwa mbilikimo, wanegro, bushmen na wabantu, kweli?
 
Nilipoona tu unasema wanadamu walitokana na nyani nimeishia hapohapo kusoma. Wewe ni miongoni mwa wale ambao hamkuelewa mnasoma nini shuleni au mwalimu wako aliye kufundisha evolution alikua kiazi. Kwakua elimu haina mwisho unaweza kupata mwanga kidogo hata kwa kusoma wikipedia jaribu kusoma tena ukiwa na open mind. Weka hisia zako na maoni yako pembeni ukitaka kuujua ukweli na ku enjoy science, vinginevyo umevamia vitu vilivyo uzidi ubongo wako uwezo
nyani nimetumia lugha rahisi ili kila mtu aelewe na avutiwe kufuatilia na wewe ujione unapakukosoa...
Nakalipithecus
Au ningeandika Mwanadamu alitokana na Samaki na sio hivyo nyani ndio ungewahi kuandika zaidi.

Kikubwa jibu hoja uelewa wa mleta hoja sioni kama unafursa kabisa, maana akiwa aelewi yeye wewe wengine watakuelewa...
 
Suala jingling gumu ambako linaonyesha kipindi cha Adams na Hawa, walikuwepo watu wengine ni pale Kaini anapofukuzwa mbele za uso wa Bwana, alienda katika nchi ya mbali na kuoa mke na kuzaa watoto. Baadhi ya wataalamu wa dini wanadai kuwa, kwenye Biblia wanawake walikuwa hawahesabiki, hivyo hao ni uzao wa Adam. Tulijibu hili pia.
ni kweli, adam na hawa hawakuzaa watoto wawili tu japo haijaandikwa.
zaeni mkaongezeke na kuijaza nchi na siku kaini anazaliwa zinaonekana zimeandikwa kwa ufupi tu. Hata ukiangalia uzao wa wale watu wa kitabu cha mwanzo wanawake hawatajwi.
Mfano henoko akamzaa Methusela. Hapo mama karukwa kwa sababu wale walikuwa mwili mmoja ukimtaja baba na mama humo humo tayari yumo.

maoni lakini
 
Binafsi mimi hiyo evolution of man theory nilisha idelete tangu siku nilivyomaliza mtihani wa form four.
 
Vita update vya dini, vinaeleza watu wote walikufa isipokuwa familia yake. Sasa na wewe unakubali Kirahisi rahisi hivyo kuwa hao jamaa uzao wao ndio ulikuja Afrika wakageuka kuwa mbilikimo, wanegro, bushmen na wabantu, kweli?
Lisilowezekana kwa Mwanadamu kwa Mungu linawezekana.
Walikwa wanane wakaijaza nchi na dunia kwa ujumla.
Mabadiliko yasikutishe maana Mwili unamatrillions ya genes ambazo zinaweza kubadilisha physiology ya kiumbe.
Ila Kiumbe hakiwi kingine bali kinakuwa bora zaidi kwa mazingira yake.
 
Mada hii hua inaniumiza sana kichwa maana hua najiuliza kama ni Kweli mbona tuna mapori mengi sana huku kwetu na hatuja wahi sikia au kuona kuna mtoto alie kuwa nyani au sokwe kaokotwa? Acha nikae kimyaa.
 
Ndiyo ifutwe sababu inampa wakati mgumu mtoto kushindwana kuelewa huku akibaki na maswali Mengi, nadhani iwekwe Elimu ya juu ambapo mwanafunzi anakuwa na uelewa mpana wa kupambanua hoja : mwana theory mmoja akasema "don't teach all my theories to innocent children"
 
Mada hii hua inaniumiza sana kichwa maana hua najiuliza kama ni Kweli mbona tuna mapori mengi sana huku kwetu na hatuja wahi sikia au kuona kuna mtoto alie kuwa nyani au sokwe kaokotwa? Acha nikae kimyaa.
Jibu utaambiwa ilichukua miaka millioni nyingi sana kubadilikakidogo kidogo.
unawezaje Kutegemea ushahidi wa miaka Mamillioni wakati Hata ushahidi wa miaka maelfu tu haupo.
Timing is the heart of these teachings
 
Hii HUMAN EVOLUTION badala ua kufutwa ni muhimu sana ifundishwe kwa vitendo namna hii
Kwa hiyo hiyo evolution imefika mwisho au bado inaendelea?
Sokwe wa sasa vipi, wanaendelea kubadilika au zoezi limesitishwa!
Hii evolution ni kwa viumbe wote au ni kwa binadamu tu?
 
Evolution.jpg

8676_Human_Evolution.jpg


Japo wanasayansi wachache wanabisha, lakini ni Ukweli usiofichika kwamba Elimu Dhana ya Uibukaji Ina utata mwingi kuliko Ukweli...
Pia ina Maswali mengi yaliyo wazi kuliko majibu...
Kila mtu anapofundishwa shule ya msingi na sekondari, Hushtuka anaposikia kwa Lugha Nyepesi kuwa Mwanadamu alitokana na Nyani/Sokwe/au mnyama wa jamii hiyo.
Tena hii ni kurahisisha tu watoto na vijana wangechanganyikiwa kabisa kama wangeanzia kuambia Huyo sokwe alipotokea.
594dbceac46188ed678b4616.jpg

Huyu mzee anaitwa Darwin Mndiye muenezaji mkuu na anachukuliwa kama ni Muasisi wa mthana hii ya uibukaji...

DUNIANI kuna kitu kinaitwa INDOCTRINATION
Hii ni hali ya Kufundisha na kulazimisha kitu kwa njia ya Imani bila kuacha mwanya wa kuhoji na kujiridhisha kisayansi.
Hii hutumika sana na sisi watu wa Imani katika kukukubali vitu kama uwepo wa Miujiza,Uweza wa Mungu, na Masomo mbali mbali ya kidini.

Zoezi hili hufanana 100% na kinachofanyika mashuleni kuwaaminisha watoto na Vijana mwanadamu Kaibuka tena bila nyama za kushiba ambazo kwa uwezo wake kiakili hangeweza kufahamu.
Kufundisha Huku hakuna tofauti na Kumfundisha Mtoto Shuleni kuwa Mwanadamu aliumbwa na Mungu bila kuwa na maelezo ya kushiba.

NINI KIFANYIKA NA WEWE KARIBU KWA MAWAZO YAKO....
Kwa kutambua hilo ingekuwa ni vizuri kama
1:Kama kufutwa ikishindikana basi Nadharia zote mbili MTU KAIBUKA KUTOKA KWA SOKWE na MTU KAUMBWA NA MUNGU zifundishwe kwa uzito sawa ila kama mawazo mawili kinzani.

2:Yote mawili yatolewe kabisa na yaanze kufundishwa mtu akiwa tayari amejitambua na uwezo mkubwa wa kuhoji na kujifunza.

DONDOO ZA ZIADA
Kwa kutambua utata uliojificha katika Dhana hii, Kuanzia mwaka 2019 nchini uturuki dhana hii inafutwa rasmi katika vitabu vya historia na Baiolijia. Mwanafunzi atajifunza haya akiwa Chuo na uwezo mkubwa wa kuhoji na kutafakari vitu tata ya kisayansi na uvumbuzi.
Mkuu asante sana kwa kuleta mada hii.Theory ya evolution sio sayansi.Watu wengine wanaiita poor science,evolution is not only poor science,but not science at all!True science proves the Bible to be true,it does not disprove the Bible.

Biblia inasema wazi kwamba Mungu ndiye aliye muumba mwanadamu.The theory of evolution is an attempt by Satan to lure away people from believing in the true God.Watu ni lazima wajue kwamba Darwin was a satanist.

Ni vema watu wakajiuliza swali moja la msingi,jee bado Sokwe wanabadilika kuwa watu?Kama jibu ni hapana, the answer is obvious,the theory of evolution is obsolete na haipaswi kufundishwa mashuleni kabisa.Isifundishwe mashuleni kwa kuwa hata mtu mkubwa anaweza kuwa indocrinated.Uongo ukirudiwa mara kwa mara,envually unaonekana kuwa kweli!To me Uturuki wako correct and rational.Sisi pia tunapaswa kufanya kama Uturuki,unless we are satanists
 
Kati ya theory za hovyo na potofu...
 
Back
Top Bottom