Kuna ulazima dhana ya "Human Evolution" ifutwe shule ya msingi hadi form six

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,750
2,000
Evolution.jpg

8676_Human_Evolution.jpg

Japo wanasayansi wachache wanabisha, lakini ni Ukweli usiofichika kwamba Elimu Dhana ya Uibukaji Ina utata mwingi kuliko Ukweli...
Pia ina Maswali mengi yaliyo wazi kuliko majibu...
Kila mtu anapofundishwa shule ya msingi na sekondari, Hushtuka anaposikia kwa Lugha Nyepesi kuwa Mwanadamu alitokana na Nyani/Sokwe/au mnyama wa jamii hiyo.
Tena hii ni kurahisisha tu watoto na vijana wangechanganyikiwa kabisa kama wangeanzia kuambia Huyo sokwe alipotokea.
594dbceac46188ed678b4616.jpg

Huyu mzee anaitwa Darwin ndiye muenezaji mkuu na anachukuliwa kama ni Muasisi wa mthana hii ya uibukaji...

DUNIANI kuna kitu kinaitwa INDOCTRINATION
Hii ni hali ya Kufundisha na kulazimisha kitu kwa njia ya Imani bila kuacha mwanya wa kuhoji na kujiridhisha kisayansi.
Hii hutumika sana na sisi watu wa Imani katika kukukubali vitu kama uwepo wa Miujiza,Uweza wa Mungu, na Masomo mbali mbali ya kidini.

Zoezi hili hufanana 100% na kinachofanyika mashuleni kuwaaminisha watoto na Vijana mwanadamu Kaibuka tena bila nyama za kushiba ambazo kwa uwezo wake kiakili hangeweza kufahamu.
Kufundisha Huku hakuna tofauti na Kumfundisha Mtoto Shuleni kuwa Mwanadamu aliumbwa na Mungu bila kuwa na maelezo ya kushiba.

NINI KIFANYIKA NA WEWE KARIBU KWA MAWAZO YAKO....
Kwa kutambua hilo ingekuwa ni vizuri kama
1:Kama kufutwa ikishindikana basi Nadharia zote mbili MTU KAIBUKA KUTOKA KWA SOKWE na MTU KAUMBWA NA MUNGU zifundishwe kwa uzito sawa ila kama mawazo mawili kinzani.

2:Yote mawili yatolewe kabisa na yaanze kufundishwa mtu akiwa tayari amejitambua na uwezo mkubwa wa kuhoji na kujifunza.

DONDOO ZA ZIADA
Kwa kutambua utata uliojificha katika Dhana hii, Kuanzia mwaka 2019 nchini uturuki dhana hii inafutwa rasmi katika vitabu vya historia na Baiolijia. Mwanafunzi atajifunza haya akiwa Chuo na uwezo mkubwa wa kuhoji na kutafakari vitu tata ya kisayansi na uvumbuzi.
 
Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,994
2,000
Hell nuh, kuna concepts tatu za genesis ya uhai, moja ni kwamba uhai uliambukizwa from other extraterrestrial beings from space, another concept is through evolution another one is through Miungu. Through miungu inafundishwa makanisani na misikitini, through evolution inafundishwa mashulei iyo ingine labda ujichunguzie mwenyewe, now the one through evolution is complex, kuna wanaofupisha na kusema tumetokea kwa manyani kama pctr yako ila ukija kisomi zaidi na kiufupi is that life came from small inanimate matter, that joined from cells, organs, system to an organism, n hadi sasa kuna bacteria wanasurvive kwenye mazingira magumu sana, na hawa ndio wanasayansi hutumia kuprove kwamba tumetokea huko, its a huge topic, huwezi iondoa tu alafu utudanganyie watoto wetu eti kwamba Mungu alitufinyanga akatupulizia pumzi and we became so, you'll be dumbing our kids.
 
MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,750
2,000
Hii HUMAN EVOLUTION badala ua kufutwa ni muhimu sana ifundishwe kwa vitendo namna hii
ndio maana tunasema wafundishwe wakiwa na uwezo wa kuhoji hata huyo sokwe katoka wapi.
maana hata wanaoamini hivyo hawaelewani wenyewe kwa wenyewe...
 
MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,750
2,000
Tatzo ww hukuelewa kiundani hatukutona na nyani wala hatukuwa nyani
Nyani walikuwepo na sisi tulikuwepo ila tulikuwa tunafanana na nyani baadae ndyo tukaanza kuchange Mdogo mdgo lakn hatukuwa nyani ila tulikuwa kama nyani
hapo hapo kwenye kufananana na nyani hata kama haukuwa nyani(maana Mimi naamini Orgin ya Mwanadamu ni UUMBAJI)
ndiko kwenye utata wenyewe.
Najua kabla ya kuwa kama nyani(Homo sapiens) tulikuwa Samaki kabisa kwa mujibu wa imani hiyo ya Evolution...
Ila ukifundisha wanadamu walitokana na SAMAKI ndio isingeeleweka kabisa
CeXDuN9.png

ourfacefish2man.jpg
 
Chachata

Senior Member
Apr 29, 2011
195
250
Dhana nyingi za elimu ya kizungu ni za kufikirika, hazina ukweli. Nimesikia jana BBC kuwa uturuki wamefuta ufundishwaji wa dhana ya human evolution shulen. Hilo si jambo jema kwa Africa hasa Tanzania na Africa mashariki yote mana dhana hiyo huambatana utalii wetu huko Oldvai Gorge . Wazungu wameona hii dhana haiwafavi na wakaona waiondoe,mi naona hata kama ya uongo ibaki tu tuendelee kupata watalii tupige hela
 
365

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
1,369
2,000
Dhana ya evolution ni nzuri na angalau inatoa mwanga kifikiri zaidi..ila dini hapana,kusema tulifinyangwa si kweli.
 
mwalomtata

Member
Nov 12, 2015
16
45
Hbrn za asubuhi. ULIYEETA HII HABARI NAKUPONGEZA MNO!
Me naona wangufuta kbsaaa hii story eti binadamu alianza kama nyani!....ndo imefanya wazungu kutudharau hadi leo na kutuona waafrika kama bdo tunafanana na nyani...na pia, imetufanya waafrika kutokujua our real identity! Kwamba chanzo chetu ni wapi,....sasa hawa jamaa wadhungu wanasema tulitokana na nyani, na kwa vile waafrika tusivopenda kufanya research zaaidi, tumeishia hapo!....
 
Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,872
2,000
Evolution.jpg

8676_Human_Evolution.jpg

Japo wanasayansi wachache wanabisha, lakini ni Ukweli usiofichika kwamba Elimu Dhana ya Uibukaji Ina utata mwingi kuliko Ukweli...
Pia ina Maswali mengi yaliyo wazi kuliko majibu...
Kila mtu anapofundishwa shule ya msingi na sekondari, Hushtuka anaposikia kwa Lugha Nyepesi kuwa Mwanadamu alitokana na Nyani/Sokwe/au mnyama wa jamii hiyo.
Tena hii ni kurahisisha tu watoto na vijana wangechanganyikiwa kabisa kama wangeanzia kuambia Huyo sokwe alipotokea.
594dbceac46188ed678b4616.jpg

Huyu mzee anaitwa Darwin ndiye muenezaji mkuu na anachukuliwa kama ni Muasisi wa mthana hii ya uibukaji...

DUNIANI kuna kitu kinaitwa INDOCTRINATION
Hii ni hali ya Kufundisha na kulazimisha kitu kwa njia ya Imani bila kuacha mwanya wa kuhoji na kujiridhisha kisayansi.
Hii hutumika sana na sisi watu wa Imani katika kukukubali vitu kama uwepo wa Miujiza,Uweza wa Mungu, na Masomo mbali mbali ya kidini.

Zoezi hili hufanana 100% na kinachofanyika mashuleni kuwaaminisha watoto na Vijana mwanadamu Kaibuka tena bila nyama za kushiba ambazo kwa uwezo wake kiakili hangeweza kufahamu.
Kufundisha Huku hakuna tofauti na Kumfundisha Mtoto Shuleni kuwa Mwanadamu aliumbwa na Mungu bila kuwa na maelezo ya kushiba.

NINI KIFANYIKA NA WEWE KARIBU KWA MAWAZO YAKO....
Kwa kutambua hilo ingekuwa ni vizuri kama
1:Kama kufutwa ikishindikana basi Nadharia zote mbili MTU KAIBUKA KUTOKA KWA SOKWE na MTU KAUMBWA NA MUNGU zifundishwe kwa uzito sawa ila kama mawazo mawili kinzani.

2:Yote mawili yatolewe kabisa na yaanze kufundishwa mtu akiwa tayari amejitambua na uwezo mkubwa wa kuhoji na kujifunza.

DONDOO ZA ZIADA
Kwa kutambua utata uliojificha katika Dhana hii, Kuanzia mwaka 2019 nchini uturuki dhana hii inafutwa rasmi katika vitabu vya historia na Baiolijia. Mwanafunzi atajifunza haya akiwa Chuo na uwezo mkubwa wa kuhoji na kutafakari vitu tata ya kisayansi na uvumbuzi.
Hata mi nimesikia mipango ya Uturuki. Mimi ni nakuunga mkono moja kwa moja ushauri wako kuwa tuyafundishe masuala haya kwenye watu wenye uwezo wa kuchambua mambo hasa kuanza A-Level.
Mimi ni mkristo, hata hivyo kwa mtazamo wangu theory ya evolution ni bora zaidi kuliko ile ya uumbaji (creation). Ukiikataa theory ya evolution, kataa pia kutoweka kwa dinosaurs, kubali kuwa mapiramidi ya Misri yalijengwa na waarabu.
Sasa swali, kama ukifuatilia mtiririko wa uzao wa mwanadamu tangu Adamu hadi Yesu Kristo ni miaka 2000 na tangu Yesu Kristo ni miaka 2017 na jumla ni miaka 4017. Je unakubali kuwa mwanadamu wa kwanza aliishi miaka 4000 iliyopita pekee? Wale Red Indians walifikaje Amerika ndani ya muda huo mfupi wakaenea kote? Wahindi weusi (Dravidian na Pre-Dravidian) nchini India na Sri Lanka walitoka wapi? Wale Aborigines wa Australia na Visiwa vya Pacific walitokea wapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom