Kuna ukweli gani kuwa serikali ya kikwete ilianza kupwaya tangu Lowassa alipoondoka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna ukweli gani kuwa serikali ya kikwete ilianza kupwaya tangu Lowassa alipoondoka?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gosbertgoodluck, Apr 26, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Jana tukiwa katika mapumziko ya Jtatu ya Pasaka tulikuwa na mjadala kuhusu mabaya na mazuri ya Edward Lowassa. Kulikuwa na makundi mawili. Kundi la kwanza lilikuwa na msimamo kwamba hakuna lolote na maana alilofanya EL katika nchi hii zaidi ya kuifilisi. Kundi la pili lilimwelezea EL kama miongoni mwa viongozi ambao wapo tayari kusimamia maamuzi yao kwa manufaa ya wananchi. Kundi hilo lilitaja kwa uchache Mradi Mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria, ujenzi wa shule za sekondari za Kata na Sakata la City Water kama miongoni mwa mambo aliyoyasiamamia kwa ukamilifu kwa manufaa ya wananchi.

  Kundi linalomfagilia EL lilifikia hatua ya kusema eti kuwepo kwake kwenye serikali ya kikwete angalau kulileta heshima fulani mbele ya wananchi na kwamba tangu alipoondoka kufuatia sakata la Richmond serikali ya kikwete iliyumba na ikapwaya kiasi cha kuonekana haifai mbele ya wananchi. Je, kuna ukweli kiasi gani kuhusu hoja hii?
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  wewe upo kwenye kundi gani kati ya hayo?
  Lowasa ameyafanya aliyoyafanya,na watanzania wameyaona,lakini suala la richmond limeharibu kila kitu,siku zote mtu hutegemea kitu kizuri toka kwa mtu so akiharibu lazima watu watasema sana,maana kuharibu si katika makubalianoo,kwa Lowasa no matter alifanya nini,lakin kwa kua aliafanya madudu na kwa wadhifa aliokua nao hakustahili na hastahili tena kurejea kwenye uongoz wa juu,hata ubunge aliopewa ni kwa sababu ya ujinga wa wapiga kura,si umeona ya MRAMBA????
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wote EL, BM, RA, na AC walistahili kula nyasi pamoja na si hata ubunge huu waliopewa except BM!
   
 4. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,022
  Likes Received: 8,504
  Trophy Points: 280
  Imepwaya wapi?tangu aondoke hatujashuhudia tena kashifa kubwa ya ufisadi meaning watu wameogopa kuchota mafwedha ,yeah alikua mchapakazi lakini ndo ivo deal lilibumburuka vilevile ujue richmond scandal sio wizi literary ni suala la ten persent ama jamaa alikua na interest zake kwenye deal
   
 5. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ninalazimika kukubaliana na kundi hili. Kweli Lowasa ni mchapakazi lakini mwizi. Unafuu wake ni kwa vile anaandaa mazingira ya kuzalisha ili aweze kuponea hapo. Wengine wanakula hata ule mfupa! Kabla ya kashfa za Richmonduli, kulikuwepo na ahueni fulani, uliweza kuona serikali inawajibika, inafuatilia kero za watu, na mfano mzuri ni ule wa City Water. Baada ya kuondoka, mwangalieni Mh Dkt wetu! Hana hata msimamo, hujui anasimamia nini, hana mkakati, akijaribu hiki, kesho anabadilisha. Ninapata hisia kwamba EL alikuwa kichwa, akielekeza gurudumu liende wapi. Sidhani kama angekuwa amebaki serikalini, wakati wa kunadi wana CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu, angemruhusu (nasemaaa angemruhusu!) JK kuwashika mkono na kuwanadi wale waliokuwa wanatuhumiwa ufisadi!!

  Lingine ambalo nimeliona (na sio nina-condone la hasha) EL amejaribu sana kuwekeza humu ndani TZ, karibu kila mahali Dar, Arusha, Manyara, Moshi, Morogoro, Dodoma kuna biashara zake. Hii ni tofuati na wengine hasa wenzetu waasia ambao wamepeleka nje. Haina maana kwamba EL SI FISADI, NI FISADI kwa kila namna, lakini pengine katika mafisadi ana nafuu kidogo....hivi wapo mafisadi wangapi TZ! Nahisi wako zaidi ya 200 (yaani idadi ya mikoa na ya wilaya na idadi ya mawaziri, kila moja ikiwa na walau mmoja, mara nyingi kiongozi mkuu, halafu ondoa shaka kama 30%)!
   
 6. n

  ndimuchumvi Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kiongozi wa nchi ni lazima awe msafi na mwadilifu.hata kama anafanyakazi kama katapila na akakosa uadilifu hawezi kuwa mzuri.kuondoka kwake ilikuwa ahueni na sidhani kama kuna impact yoyote.hatujengi uongozi kwa kutegemea watu tu bali mfumo ambao hauwezi kufa mtu akiondoka.bado hata kama angekuwepo bado serikali engepwaya kama ilivyo sasa
   
 7. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Nakubali bila kupindisha mameno kuwa kuondoka kwa Lowassa imekuwa kama serikali iko uchi, kwa maneno mengine Lowassa alikuwa anaficha udhaifu wa serikali kwa utendaji wake
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mi ninaweza kuweka hivi, EL kweli alikuwa ni mzugaji so aliweza kuifanya serikali ya Jk inazuga hasa.... sasa baada ya huyu mzugaji kuondoka hii serikali imekosa mzugaji hivyo inaonekana inapwaya sababu marazote hivi viserikali vyetu vinafanya kazi kwa kutuzuga ndio maana bado hata baada ya miaka 50 ni kanchi kasichoeleweka.

  Pia ni kweli EL ni mtu mwenye kaliba ya uongozi ila ambaye alishaamua kuitelekeza kaliba hiyo zaidi ya miongo kadhaa iliyopita na Mwl Nyerere aliliona hilo.

  Mwaka 2008, nilikutana na mdau mmoja alikuwa anatoa stori kuwa EL alikuwa hawezi kupitisha "uwekezaji" wowote katika nchi bila kukatiwa chake.
  Sasa huyo hatuwezi kumuita ni mtu tena eti ni "afadhali"....

  Katika mjadala wa Tz tunayoitamani, EL ni TAKATAKA tu.​
   
 9. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ivi ukiiba sh laki tano kwamtu alafu baadae anakuja(hajui kama wewe ndiyo umemwibia) anasema naomba unikopeshe elfu ishirini lakini wewe ukampa laki moja si atakuona mwema sana,lakini akigundua kwamba wewe ndiye uliye muibia laki zake tano je unafikiri iyo laki moja yako uliyompa kwake itakua na maana tena,hivi ndivy lowasa alivyofanya.
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nahisi hata hiyo shule ya kata hukifika wewe maana hiyo reasoning yako ni ya mtu ambaye amekurupuka kutoka machungania. Hiyo City water unayozungumzia maamuzi yake aylichukuliwa Lowassa akiwa ni waziri wa maji na ni yeye aliyehusika na mkataba huo ambao baadae aliufanyia usanii wa kujifanya kuuvunja. Kilichotokea baada ya hapo ni serikali kuingia gharama kubwa za kuendesha kesi ambayo gharama za mawakili pekee zilikuwa ni zaidi ya dola 11 milioni alizopewa Mkono. Hizo shule za kata unazozitaja zilikuwa ni mkakati wa serikali na maamuzi ya baraza la mawaziri chini ya JK. Hakuna wakati wowote ambao yeye ametatua kero za watu zaidi ya kukaripia na kudhalilisha wakuu wa wilaya (Mongela na Madaha ni mifano michache) kwa nia ya kuonyesha anajali. This was purely a populist approach ambayo haikuzaa matunda yoyote.

  Inashangaza mtu ana-justify uwekezaji wa proceeds of crime ndani ya nchi kama namna ya kum-vindicate mtu aliyeiingiza nchi hii katika umaskini mkubwa. Tunalolikosa kutoka katika uongozi wake toka kuondoka kwake ni kutokuwepo kwa kashfa mpya inayotishia kuchota mabilioni ya shilingi kutoka hazina. Watu wanadhani uchapa kazi ni kupiga makelele, kukemea na kuonekana kwenye TV kila siku. This is an adolescent reasoning ambayo haizingatii kwa kiasi gani huyu mtu amefeli katika kuzingatia maadili. Kwa taarifa yako sifa mama ya mtumishi wa umaa ni maadili yake kwanza kwa sababu uchapa kazi hujitokeza baadae. Na nchi yoyote yenye ustawi popte duniani ni ile ambayo haifanyii mzaha suala la maadili. Ni hapa tu Tanzania (tena kwas wajinga wachache) wanaoshangilia wahujumu uchumi na kuwaona mashujaa. Hata swahiba yake Shinawatra (aliyekuwa ampe dili la mvua ya kutengeneza) aliondolewa madarakani na kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa ufisadi wake. Sasa ni vizuri ukawaambia hao mnaobishana nao kijiweni wkenu(maana hamna kazi za kufanya) kuelewa kwamba hatukubali viongozi walio bize kuchota maji na hapo hapo wako bize kutoboa mtungi wanaotekea maji halafu tuwaone ni mashujaa. Watafute watu wa kuwadanganya, siyo watanzania wenye uchungu na nchi na rasilimali zao. Kwani hawa majambazi wanaoua watu wasio na hatia si wamewekeza humu humu nchini na bado tunawalaani na kuomba wawekwe jela. Nashangaa mnamchekea huyu anayefanya ujambazi kwa kutumia makaratasi. Utumwa huu mtauacha lini?
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umempa shule ya uhakika sana huyu jamaa anayezeeka akishangilia kaburi la wanae na wajukuu zake!
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tena ni takataka ya sumu kali ambayo haitufai hata kidogo. Hawa ndiyo wanatufanya tupate majibu ya hovyo toka kwa watoto wetu mara zote tukiwauliza wangependa kuwa nani wakiwa wakubwa, wao wanasema wangetaka kuwa mafisadi!
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nenda basi ukamuarifu kwamba watu wanamtetea upate ngawira zako. Hata hivyo yeye mwenyewe kwa akili zake anajua wazi kwamba hatakiwi na ndiyo maana hathubutu hata kutembelea maeneo kama kariakoo, au hata mitaani arusha.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mbopo,
  Wameondoa kile kitufe cha thanks, ningekuwekea hata mara tano. You nailed it!
   
 15. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Katika kujibu hoja (kichwa cha habari):

  Kundi la kwanza halijajibu swali. Wao walikuwa wanajibu swali lisemalo. Je kuna lolote la maana lilifanywa na EL?

  Kundi la pili lilitamani kujibu swali lakini limeshinda kabisa kuthibitisha hoja. Kwanza wange tupa maana ya 'Serikali kupwaya', kisha watuambie ni lini hasa Serikali ilianza kupwaya? ni nini kilisababisha kupwaya? Kuwepo kwake kungesaidiaje au kutokuwepo kwake kulisababisha ukosefu wa nini katika utekelezaji wa shughuli za Serikali katika Wizara, Idara, Taasisi za Serikali, Mikoa, Halmashauri, Wilaya n.k mfano katika Katika hali ya Chakula, Afya, Elimu, Nishati, Maji, Miundombinu, Makazi, Demokrasia & Uhuru wa Wananchi n.k.

  Awe amefanya mabaya au mazuri huko nyuma, natoa tena angalizo kuwa ukizunguka Wilayani, Mikoani, Idarani, Wizarani, Kwenye Vyuo vyetu, Kwenye Mashirika ya Serikali na yasiyo ya Serikali, ndani ya CCM na nje ya CCM! utapata watu wengi wa namna ya EL na pia utapata Watu wengi zaidi wenye sifa nzuri zaidi kuliko EL kielimu, kiutendaji na hata kimaadili. Sasa swali kwa nini tunapenda kuzunguka hapo hapo, kama vile Tz ina mtu wa aina hiyo mmoja pekee???????


  NI wakati muafaka sasa kufungua macho yetu na kuwatafuta hao watu wengine wengi zaidi kama tuko makini kuijenga nchi yetu.
   
 16. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tangu aondoke zimechotwa nyingi kuliko zilizochotwa akiwepo, hujui zile pesa za economic stimulus package zaidi ya trillion moja zimetumika kifisadi na sasa ndio kwanza zinaanza kufumuka
   
Loading...