Kuna uhusiano gani wa lugha ya kiarabu na majini?

Kwenye maandishi ya waislamu utakuta wakieleza kwamba majini sio tu kwamba wana majina ya kizungu bali kuna hadi majini wenye imani ya ukristo na wengine hawana dini kabisa.
Yawezekana ukawa sawa but maelezo yako yapo too general cause huweki hata jina moja la hao majini kama ulivyo sikia au kusoma, mi nimetaja majina kama jinni mwajuma, maimuna, makata, mahaba nk. weka na wewe majina hayo ya kizungu tujifunze Zaidi.
 
Yawezekana ukawa sawa but maelezo yako yapo too general cause huweki hata jina moja la hao majini kama ulivyo sikia au kusoma, mi nimetaja majina kama jinni mwajuma, maimuna, makata, mahaba nk. weka na wewe majina hayo ya kizungu tujifunze Zaidi.
Sasa mkuu mbona unachekesha tena ina maana majina ya kizungu huyajui hadi nianze kutaja? Na hata nikitaja itabadili nini kama hukubali nilichoeleza? mfano nikitaja jini John au Smith ndio itathibitisha maelezo yangu ni kweli? Halafu vitu vyengine ni vya ajabu kwamba tunabishana et majini hawatumii majina ya kizungu kwani majina ya kizungu yana nini hadi majini wasitumie? Hivi kuna muarabu anaitwa Makata,mahaba au Mwajuma? Nenda huko Arabuni kama utakuta hayo majina.
 
Kutokana na maandiko yako, kwanza elewa kuwa Kiarabu hakiandikwi kutoka juu kwenda chini. Huandikwa kutoka kulia kwenda kushoto.

Pili, jee, unajuwa kuwa hata Kiswahili kilikuwa kinaandikwa na irabu (herufi) za Kiarabu?

Tatu, unakiona Kiswahili tunavyoandika hapa? Jee, hizi ni irabu za lugha ipi? Maana hizi hizi hutumika kuandika lugha nyingine nyingi duniani.

Unaweza kutumia irabu za Kiarabu kuandika lugha zingine na haimaanishi kuwa umeandika Kiarabu.

Ungeweka kilichoandikwa tunaojuwa Kiarabu tungekusaidia kukujuza kama hicho ni Kiarabu au la na kama ni Kiarabu maana yake nini.

Inawezekana kuwa anaandika Kigogo? Kihehe? Kiswahili?

Who knows?
Dahh, fox uko poa sana
 
imekuaje hadi nikajiuliza hilo swali?

story yenyewe iko hivi.

nina rafiki yangu wa kike,siku za hivi karibuni yapata kama mwezi sasa,mara kwa mara na humtokea baada ya kutoka kusali tu,anajikuta anandika vitu ambavyo hata yeye havijui.anakuja kushtuka tu ameandika.hiyo hali haikutushtua na tuliona kawaida tu

kilichotushtua ni hiki

alianza kuandika kwa kukoroga koroga kama ambavyo watoto wa awali huwa wanafanya wakipewa daftari na peni bila kufundishwa chochote.kisha akaanza kuimprove kidogo kidogo na ikafikia hatua anaandika kitu furan kinachoeleweka ambacho hatujui ni nini na ni lugha gani.

kwa kifupi kapitia hatua zote za mtu ambaye anajifunza kuandika lakini hata yeye binafsi hajui.ila anaandika mtindo kama kikolea au kichina kwa kwenda chini,tumejaribu kugoogle lugha mbali mbali hatukupata hata lugha moja ya mtindo huo

mashaka yakaanza
baada ya hiyo hali tukaanza kupata mashaka kua inawezekana kuna namna kiroho,pengine ni lugha ya kiMungu au ni mapepo.

tukaona tuwashirikishe watu wa Mungu(nazungumzia waokovu).siku ya ijumaa ikabid aende kwenye jumuiya na akawasimulia kila kitu.
baada ya kuonesha hilo daftar analoandika mama wa kwanza tu ambaye ndio mkuu wa jumuiya akashtuka ,akasema hiki si kiarabu lugha ya mashetani au majini.kisha akamwambia chukua namba ya simu badae utanipigia.lakini mpaka saizi hatujampigia maana bado tunamaswali mengi juu ya kauli yake.

swali liko hivi.
Ni kwanini ?hasa wakristo huwa wanahusisha lugha ya kiarabu na mambo ya kishirikina,majini,mapepo nk.
ikitokea sehemu yoyote ambayo inautata frani hivi kukawa na lugha ya kiarabu basi wazo la kwanza ni mapepo.

hiki kitu nmekisikia mara nyingi na nlijua ni kwa watu ambao hawajui.mambo ya Mungu sasa kilichonishangaza hadi myu wa Mungu nae yumo kwenye huo mkumbo.

mwenye ufahamu tafadhali tubadirishane uzoefu.

Angalizo,mimi ni mkristo na naamini katika Mungu,pia naheshimi dini zote duniani.kama.ninavyoheshimu dini yangu.mada kama hizi huwa hazichelewi kuhama lakini mimi sipo hapa kukashifu dini ya mtu yeyote.nipo hapa kupata ufafanuzi.na pia kama kutakua na mtu ambaye anaweza kunisaidia kuhusu tatizo la huyo dada nitamshukuru sana.

kama kuna sehem patahitaji kueleweshana nipo hapa,

natanguliza shukran
Unataka ukweli au ndugu yako apone nenda kwa mchungaji katunzi eagt city center mtoni mtongani kanisa lipo kwenye njia reli linapita juu kwa aziz ally mtoni au kituo stand ya shamba au kwa mama mgaya hapo atapona bure kabisa ibada kila siku nenda pale niamini ninachokwambia atapona kwa maombi pale bure kabisa nauli yako tu .
 
Mtoa post angeuliza
hivi.
Kuna Uhusiano gani Kati ya Majini na Uislamu ?
cc Tz mbongo,
Mtoa post kaeleza vizuri na kauliza swali vizuri tu lenye kuhusu kuhusishwa kiarabu na majini na ushirikina,sasa suala la uislamu na majini ni mada nyengine kabisa.

Lakini naweza kusema labda hichi kinachoonekana kama mahusiano kati ya uislamu na majini kwamba ni waislamu kuwa na elimu ya hao viumbe majini,sasa wabongo tuna mitizamo yetu kuhusu hao majini na kibaya ni kudhani hadi sehemu zengine nako wana mitizamo kama hiyo.
 
Back
Top Bottom