Kuna uhusiano gani kati ya mafuta ya zaituni na majini?

kingkimbe

Senior Member
Jul 11, 2017
109
45
Wakuu habari Za wakati huu kama kichwa kinavyosema nataka kutambua uhusiano Kati ya mafuta ya zaituni na majini
Mana nimesikia haya mafuta yanaweza kutoa majini mwilini na yanaweza kutoa uchawi licha ya kazi yake ninayo ijua mimi ya kulainisha ngozi na kuifanya iwe mzuri.
NAWASILISHA MADA ASANTE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna kitu (uhusiano) hapo ndugu.

Kuna msemo wanasema, 'ukinuia jambo linaweza kutokea' so tunda la zaituni limekuwepo kabla ya jina hilo zaituni kutumiwa na wanadamu.

Kuna wale wenye imani na majini, hao ndiyo watakupa ulongo wa matumizi kwenye mahusiano.
 
Waulize mapasta mana huyatumia wakidai ni mafuta ya upako. Mana ake mahusiano yapo ndo mana mapasta hutumia hiyo advantage kwa wasiojua ukweli wake
 
Mafuta ya mizeituni yana nguvu kubwa kiasili......

Na hufanya kazi kutegemeana na manunuzi ya mtumiaji.

Ukiyatukia kama dawa unapona kabisa cha msingi ni imani yako (manuiz)

Nina ushahidi mmoja alipona TB na ilikuwa ishamla sana......na amepona haraka isivyo kawaida.
Kila mara anaenda checkup......ma Dr wanauliza unatumia dawa hizi hizi zetu? Au una tiba mbadala?
Jamaa anawaambia ni vidonge vyenu tu....

Mwishoni alipona kabisa....


Hata majini yanaondoka ila manuizi yako ndo yanayapa amri ya kufanya kazi
 
Mafuta ya Zeitun.ni mafuta yenye historia ya miaka zaidi ya 2000.ni mafuta matakatifu kwa wana wa Israel na wakatolic.ndo mafuta aliyopakwa Daudi na ndo wanayopakwaga wakatoliki wanaopata sacrament ya kipaimara ,au mpako mtakatifu kwa wagonjwa wanaokaribia kufariki..majini sawa wanaweza tumia lakini sio yale yaliotoka kanisani...hawa mapasta wengine wanatumia mafuta ya alizeti wanauzia watu wakidai ni mafuta yenye upako wakati sio kweli😁😁
 
Mke wangu aliugua ugonjwa usioeleweka kama miezi miwili iliyopita,basi mama mkwe akashauri nimpeleke kwenye maombi kanisa la Safina lilipo jijini Arusha,ile tunafika geti la kuingilia kanisani kuna jamaa amesimama hapo na mafuta kwenye pembe(sina uhakika kama ni la ng'ombe)akatupaka kwenye paji la uso,kisha unaingia kanisani,sikuelewa kabisa hicho kitu nikaulizia watu nikaambiwa mafuta ya mzeituni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilijua ni mazuri tu kwa afya sababu hayana cholesterol kumbe yanafukuza mpaka majini, ndio maana aghali kumbe

renegade
 
Mke wangu aliugua ugonjwa usioeleweka kama miezi miwili iliyopita,basi mama mkwe akashauri nimpeleke kwenye maombi kanisa la Safina lilipo jijini Arusha,ile tunafika geti la kuingilia kanisani kuna jamaa amesimama hapo na mafuta kwenye pembe(sina uhakika kama ni la ng'ombe)akatupaka kwenye paji la uso,kisha unaingia kanisani,sikuelewa kabisa hicho kitu nikaulizia watu nikaambiwa mafuta ya mzeituni.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahyo hadi makanisani yanatumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom