Kuna ugomvi wa chini chini India dhidi ya Tanzania?

Kuna ugomvi wa chini chini India dhidi ya Tanzania?

Ingawa wahindi wanadharau lakini kwenye serikali hii Kuna mengine wanawafanyia kwa uonevu, mtu kapewa tenda ya kushona sare za jesho, unamwambia muhujumu uchumi, aliyekula pesa za escrow wanajulikana anakamatwa singa singa peke yake
Kwa hiyo inawezekana ndugu na jamaa waliokuwa wananunua na ku export mazao haya wakafanya mgomo baridi?
Unajua nimeliwazia sana hili mpaka kuandika haya.
Lakini pia hata kama ni hivyo kwanini sisi wenyewe tusipeleke zinakohitajika kama walivyokuwa wanapeleka wao.
Maana sidhani kama ni serikali ya India ndio imekaa bidhaa zetu
 
Nani alikwambia hayon i mazao ya biashara.. ilisha shauriwa eti yaliwe na wanafunzi mashuleni pia na sisi wananchi tuyatumie kama mboga,tutengeneze bagia,vibama n.k
 
Wenzetu wana umoja sana, sababu kubwa ni yule mhindi aliyepimwa mkojo...kwa hiyo wakulima wataisoma namba kwa kigujarati🙂🙂🙂😉
 
Kwa hiyo inawezekana ndugu na jamaa waliokuwa wananunua na ku export mazao haya wakafanya mgomo baridi?
Unajua nimeliwazia sana hili mpaka kuandika haya.
Lakini pia hata kama ni hivyo kwanini sisi wenyewe tusipeleke zinakohitajika kama walivyokuwa wanapeleka wao.
Maana sidhani kama ni serikali ya India ndio imekaa bidhaa zetu

Hatuwezi kupeleka wenyewe maana kule wanauza kwa kujuana na kama wamepanga wahindi wote kutokununua bidhaa zako basi tegemea hasara, yaani walipoacha kununua tz maana yake wametafuta sehemu nyingine wananunua sasa
 
Kweli tumekwama, kama ni hivyo ni bora kutafuta nchi zingine wanazohitaji kwani zipo nyingi tu
 
Kwa hiyo inawezekana ndugu na jamaa waliokuwa wananunua na ku export mazao haya wakafanya mgomo baridi?
Unajua nimeliwazia sana hili mpaka kuandika haya.
Lakini pia hata kama ni hivyo kwanini sisi wenyewe tusipeleke zinakohitajika kama walivyokuwa wanapeleka wao.
Maana sidhani kama ni serikali ya India ndio imekaa bidhaa zetu

Mbona tuwavivu wa kosoma na kujua ukweli. Nimewawekea links zinazowaonyesha, shida sio walanguzi bali hali ya zao la mbaazi nimbaya hata kwa wakulima wa huko India.

Sasa ikiwa bei ya hilo zao iko chini india, tulitegemea wanunuzi waje wanunue kwetu kwa bei ya mwaka juzi, walipe kodi zetu na wazisafirishe , na kumbe zao hilo ni bei rahisi kwao.

Mbona tunatafuta kuegesha lawama pasipo stahiki. Hakuna mfanyi biashara atakaye wacha shillingi moja yenye faida kwake. Manji akigoma Rajesh atafanya.

Rudia jibu langu kwa Zitto NA soma links utafaidika
 
Pia tungejaribu kuangalia kuanguka kwa mazao kama Nazi, kahawa na pamba enzi zile nini kilisababisha ndo iwe kama literature review zetu then sasa tutajua why now mazao haya. Unajua enzi zile sisi tulikua ndo wauzaji wakubwa wa bidhaa nlizotaja mpk zikapelekea baadhi ya nchi ikiwemo uarabuni kugombea kututawala lakini baada ya miaka kadhaa mbele zimekua sio kitu so yaezekana sababu iliyoiangusha bidhaa zile ndo the same zinayoitenda bidhaa hizi

Mkuu funguka zaidi kuhusu hizo sababu nasi tupate kujua tafadhali na kuchanganua zaidi
 
Ukitaka kujua hali ya mbaazi au tatizo kwani India wamesitishakununua mbaazi njee ya nchi, soma kwenye links hizi, NA uache unafiki NA kufuata uchochezi wa kisiasa::

1) Tur dal to get 50% cheaper as state keen on clearing stock - Times of India

2) mbaazi zaozea shambani Mozambique: Unsold pigeon peas at risk of rotting in Cabo Delgado

3) https://www.producer.com/2017/11/india-slaps-duty-on-peas-wheat/

Zitto ni mwansiasa nilie na mategemeo naye, lakini kwenye hilo ametuhadaa sana na anajua sababu ya India kusitisha kununua zao hili na ni uongo kuwa kuna tatizo la kisiasa. Swali jee anawatumikia marafiki zake NA sponsor wake akina Manji na wafanybiashara wa zao hili??????!!!
 
Inawezekana wanawalinda wakulima wa ndani.juzijuzi marekani wamepiga pini export za aluminium foil kutoka china ili kulinda uzalishaji wa ndani
 
Mbona tuwavivu wa kosoma na kujua ukweli. Nimewawekea links zinazowaonyesha, shida sio walanguzi bali hali ya zao la mbaazi nimbaya hata kwa wakulima wa huko India.

Sasa ikiwa bei ya hilo zao iko chini india, tulitegemea wanunuzi waje wanunue kwetu kwa bei ya mwaka juzi, walipe kodi zetu na wazisafirishe , na kumbe zao hilo ni bei rahisi kwao.

Mbona tunatafuta kuegesha lawama pasipo stahiki. Hakuna mfanyi biashara atakaye wacha shillingi moja yenye faida kwake. Manji akigoma Rajesh atafanya.

Rudia jibu langu kwa Zitto NA soma links utafaidika
Sio uvivu wa kusoma mkuu link hizi umeweka baada ya mjadala kupamba moto.
Na kila mchangiaji anawaza lake na wengine huchangia au kujibu hoja
Kwa hiyo usishangae ukaona mtu anachangia mpira katika uzi huu
Anyway ngoja nizipitie hizo link
 
Mbona tuwavivu wa kosoma na kujua ukweli. Nimewawekea links zinazowaonyesha, shida sio walanguzi bali hali ya zao la mbaazi nimbaya hata kwa wakulima wa huko India.

Sasa ikiwa bei ya hilo zao iko chini india, tulitegemea wanunuzi waje wanunue kwetu kwa bei ya mwaka juzi, walipe kodi zetu na wazisafirishe , na kumbe zao hilo ni bei rahisi kwao.

Mbona tunatafuta kuegesha lawama pasipo stahiki. Hakuna mfanyi biashara atakaye wacha shillingi moja yenye faida kwake. Manji akigoma Rajesh atafanya.

Rudia jibu langu kwa Zitto NA soma links utafaidika
Siyo uvivu bali wana JF wengi ni kama mabehewa..wewe andika uzi wa kizushi basi kama watatokea wachangia wakaaonyesha kwa vielelezo ya kuwa siyo kweli asilimia 99 ya wachangiaji watakaofuta wa reply post yako ya mwanzo kwa na mara nyingi hawasomi zawachangiaji wengine na wataanza kutoa povu kulingana na info za original post.
Zito ziyo kama hajui bali ni mpotoshaji anafanya hivyo kwenye facebook kwani yeye anafuta kick ya popularity si unaona hivi sasa anatafuta kick kwa kutembelea miradi hana hata idea nayo na hajasaidi chochote lakini wanajimilikisha wao. na kila siku katika post zake huwa anatapatapa..Usipoteze muda kuwafahamisha hawaoni hao ijapokuwa macho wanayo na viziwi ijapokuwa wana masikio kwao hivyo viungo ni mapambo tu na haviwasaidii kwenye hisia
 
Walikuwa wana export India mazao hayo wengi ni watanzania wenye asili ya India A kina Manji n.a. export trading co. Wote wamechanganyikiwa n.a. kikimbiza mitaji baada ya jamaa yetu kutwa kucha ni vitisho tu wameogopa sasa
 
Rais amelala usingizi wa nusu kaputi kuhusu shida halisi za watanzania, na akikurupuka kutoka usingizini basi ni kufukuza watendaji wake, kununua na kuwaangamiza wapinzani na mwisho kuvamia bandarini na kujidai kukamata cargo zilizoagizwa na taasisi za serikali.

Mawaziri nao wamekuwa kama kuku wa kienyeji, kutwa kuzurura ovyo na kudokoa dokoa (kutatua shida ndogo ndogo za mwananchi mmoja mmoja na hapo hapo kuwaadhibu watumishi wa umma) na mwisho wanawika kama kuku (Wanaropoka matamko yasiyokuwa na kichwa wala mkia ili kutafuta kick).

Serikali imepoteza mwelekeo.
Taifa limepoteza mwelekeo.
Nchi inazidi kuangamia kwa kasi.
Link Mwinyi: Nchi sasa inakwenda kama Gari bovu

Vyuma vimekaza, wazalendo wanaomba grisi ili walainishe uchumi unaokuwa kwa kasi kwenye makaratasi.

Link Waziri Mpango aiomba Benki ya Dunia mkopo wa Dola 150 milioni za Marekani ili kuchochea ukuaji wa uchumi

Link2. Muda wa kudanganya na kutafuta "kick" sasa umefika kikomo, umebaki muda wa kuumbuka
 
Mkirindi sawa mbaazi zilikua chini na hayo mazao mengine nayo? usidhani links ni majibu tosha kwa maumivu ya sisi wakulima.
 
Ni commerce ya kidato cha pili haihitaji degree
Supply ikiwa kubwa demand inakua ndogo na bei inashuka
Dawa yake ni rahisi sana kujiunga kwenye ushirika tu.
India walitusumbua sana kwenye korosho,tukabadili mfumo wa uuzaji sasa watu wanapata faida.
Zitto usitake kudanganya watu wasio na ufahamu hakuna tatizo kati nchi mbili hizi ni biashara tu,mtu hawezi kununua mazao kwa bei ya juu kukufurahisha wewe ili muimarishe uhusiano,wakati ana mzigo wa kutosha kwenye hifadhi yake
 
Muheshimiwa zito usipotoshe umma hii imetokana na mabadiliko ya sheria zao za kuingiza mazao Kwa ajili ya kuwalinda wakulima wao kabla hujaandika vitu kama hivi fanya uchunguzi kwanza kuliko kuropoka na kuleta matatizo ya kidiplomasia na hii sio kwa Tanzania tu bali ni kwa nchi zote zinazoingiza mazao hayo india ushahidi ni hii sehemu ya gazette la serikali ya india
1daadb0e79498dfa90c3304bc0cd5162.jpg
b6516d05a20837835b050301f83df511.jpg
 
Na kuhusu dengu serikali ya india imeongeza import duties from 25% to 60% ambayo inaleta juma ya kodi zote kufikia 66% hivyo hakuna faida Kwa mnunuzi kununua kwa bei ya zamani hivyo ni lazima wawabane wakulima wauze kwa bei ya chini au waache kununua. Tatizo hapa ni kushindwa kuwa na soko mbadala la mazao yetu ya pulses vilevile serikali kutokujizatiti kufanya biletaral agreement na nchi wanunuzi wakubwa wa pulses. Bei ya Dengu itaendelea kushuka kutokana na hilo reference nenda www. Globalpulseconfedaration.com
 
Back
Top Bottom