Kuna ubaya Rais wa sasa kujiunga na CHADEMA?

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,642
2,000
Kwani unadhani anaanisha. Alikuwa anaota. Ok. Ukienda Ndani zaidi. Wanaandika such nonsense kwa malengo ya kujifariji na kutaka kueleza kuwa mwendazake hawakumuunga mkono Sasa ndo huyu Ni zaidi ya yule. Sio mbaya kujifariji.
Tatizo la siasa zetu zinazunguka watu badala ya sera. Halafu kuna watu majununi humu hata huwezi kujua wapi wako serious wapi wanatania.

Sasa huyu running mate wa yule, mabaya yote ya yule aliyajua na kayakalia kimya, ndiyo wanamtaka?
 

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,103
2,000
Mnashangaza Mbowe, Mnyika, Lissu ua Mwalimu hawana maana tena. Wewe unaonekana mzoefu wa kutamani waume wa wenzio?
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,056
2,000
Ungetoa maoni yako tu kwa jinsi unavyoyaona mambo yanavyokwenda bila hata kuiingiza CHADEMA katika mambo ya maCCM...

Kuihusisha CHADEMA na Rais Samia Suluhu Hassani, inaonesha wazi kuwa huijui katiba ya JMT. Unalowaza haliwezekani kikatiba...


Kama Rais Samia S. Hassan hakubaliani na mambo yalivyo huko CCM na anataka aendelee kuwa Rais Wa nchi hii na kutekeleza ajenda zake bila usumbufu, basi ana options zifuatazo pekee;

1. Kuvunja bunge na twende ktk uchaguzi mwingine, au;

2. Afanye a total & a complete OVER HAULING ya cabinet na serikali yote kwa ujumla bila kuvunja bunge, na au;

3. Ahakikishe anavunja nguvu za makundi pingamizi yote dhidi ya mipango yake. Na eneo hatari kwake ni BUNGE...

Hakuna shaka yoyote kuwa Spika Job Ndugai ndiye opposition force kubwa dhidi ya ajenda za Rais Samia S. Hassani...

Akiachwa hivi hivi bila kitu kufanyika, technically, anaweza kulitumia bunge vilivyo kukwamisha na kuvuruga ajenda za Rais Samia..!!

Atakapogundua kuwa anahujumiwa na Bunge kisha akaamua kuchukua hatua (labda kwa kulivunja hili bunge), itakuwa a little bit too late kwa political damage itakayokuwa imetokea...!!

All in all, Mimi nadhani, upo mpango wa Mungu wa kufanya "a complete political power shifting" ya utawala wa nchi hii kutoka CCM kwenda chama kingine cha siasa...

Moja ya ishara kubwa ni kifo cha huyu Bwana John Pombe. Hakikuja katika namna ya kawaida. Kimekuja amidst malalamiko makubwa ya wananchi kunyanyaswa na kunyimwa haki zao...

Then, ndani ya wiki mbili au tatu hivi mtu anapotea na kisha anarudi akiwa mfu ndani ya jeneza. Ilikuwa ni maajabu sana sana sana..!!!

Kisha, all of the sudden, nchi inachukuliwa na kutawaliwa na mwanamke..!!

I believe tuko kwenye "transition period". Na mama Samia S. Hassan asipokuwa makini, hata yeye ANAWEZA ASIFIKE 2025...

Scramble & struggle for political powers haijawahi kuacha nchi na baadhi ya watu salama hata wale tunaodhani wanaweza kuwa salama zaidi kuliko sisi..!!

Let the political change takes its course no matter how...

Na mama Samia Suluhu Hassan has been assigned these responsibilities by the Almighty God to facilitate these changes whether akiwa anajua ama hata pale atakapokuwa hajui...!!

That's how God, The Almighty does his things to save his people...
 

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,096
2,000
Nakupa thanks japo umenipinga kisha ukarudi kule kule. Sikutaka kutumia Samia na badala yake nikatumia Rais. Ukinisoma vyema utaona nazungumzia pale ambapo awamu ya tano inaisha, yaani miaka minne iliyokuwa ya JPM. Sasa wakati wa kuanza kampeni ndipo hayo mambo yanatokea ukichanganya na yale uliyoweka hapo
 

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,096
2,000
Kweli we nchi kavu. Ukaota. Ukaamka. Ukaota kabla ya kuamka ukaandika. Hakuna chama cha upinzani kinachoweza kumuuunga mkono Rais wa chama tawala. Labda moyoni Lakini sio hadharani. Hiyo itamaanisha kuwa wamejitoa upinzani. Ndo mana wewe mkuu endelea kuota.
Kwenye siasa kila kitu kinawezekana. Wewe ulidhania ingefika siku nchi nzima ikatwaliwa na ccm?
 

Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,563
2,000
Kuanzia leo hadi mwisho wa mwezi huu ndio tutawajua.

Kelele zote kumbe mbaka saizi hujui unacho ngojea.
Kaa endelea kungoja pekeako wenye akili wanajua ccm wanafanyaga nini.
Hata Yusufu aliota na akadhihakiwa, sembuse mimi?

Sio wewetu nawenzako pia wana ndoto matope kama izo.

Mngekuwa mnaota kuhusu ruzuku na michango yenu inavyoliwa na DJ ningekuona unandoto.

Ufipa Ofisi kama banda la bata na pesa kwa mabilioni mnalipwa zinaenda kwenye Mbege milimani nyie mnakazana kuota mipango ya Ccm, nyumbu ni nyumbutu.
 

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,096
2,000
Kelele zote kumbe mbaka saizi hujui unacho ngojea.
Kaa endelea kungoja pekeako wenye akili wanajua ccm wanafanyaga nini.


Sio wewetu nawenzako pia wana ndoto matope kama izo.

Mngekuwa mnaota kuhusu ruzuku na michango yenu inavyoliwa na DJ ningekuona unandoto.

Ufipa Ofisi kama banda la bata na pesa kwa mabilioni mnalipwa zinaenda kwenye Mbege milimani nyie mnakazana kuota mipango ya Ccm, nyumbu ni nyumbutu.
Endelea kutapika mkuu. Yaelekea bado tumbo lako lina uchafu wa kutosha. Tutadeki usiwe na shaka
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,488
2,000
Na ugumu zaidi ataupata kwenye chama chake CCM ambapo wanadai kuwa mwanamama hataweza kuhimili mikiki mikiki ya siasa za bongo kama Rais, na zaidi kama mwenyekiti wa chama.
This time ikitokea tena watu wakaanza kufanya upumbavu wa namna hii, kwa hakika watakuwa wanalipigia Jeshi, na si kwamba watakuwa wanalibip, hapana. Watakuwa wanalipigia Jeshi na safari hii litaipokea simu hiyo. Tuache kuendelea kufanya ujinga kwenye mambo ya msingi yanayohusu nchi
 

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,096
2,000
This time ikitokea tena watu wakaanza kufanya upumbavu wa namna hii, kwa hakika watakuwa wanalipigia Jeshi, na si kwamba watakuwa wanalibip, hapana. Watakuwa wanalipigia Jeshi na safari hii litaipokea simu hiyo. Tuache kuendelea kufanya ujinga kwenye mambo ya msingi yanayohusu nchi
Kwa awamu hii ya mama anything is possible maana kuna watu watataka kujaribu misuli yao kisa ni mwanamama
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,488
2,000
Kwa awamu hii ya mama anything is possible maana kuna watu watataka kujaribu misuli yao kisa ni mwanamama
Mama tayari alishaonya kuhusu pilika pilika za 2025 kwamba watu waache; wenye akili timamu na wenye kusikia nadhani watakuwa walimsikia na kumwelewa
 

LGF

JF-Expert Member
Dec 6, 2020
339
250
Poor CHADEMA, kijasho kinawatoka. Sasa wanajaribu kila stori kujiliwaza, sawa na mzamaji Ziwa Tanganyika anakumbatia muwa umuokoe. Eti wana mass following? Wapi? Bagonza ni mmoja tu wala hatoshi hata ukiingiza kina Salungi na tundulissu majuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom