Kuna ubaya Rais wa sasa kujiunga na CHADEMA?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,090
2,000
Tunakoelekea mambo yatakuwa moto kama Rais ataamua kusimamia yale anayoyaamini kuwa ni sahihi kwa taifa. habari za mitandao huko zinasema kuwa ziko harakati za kumkwamisha katika utekelezaji wake wa majukumu ya kila siku. Na ugumu zaidi ataupata kwenye chama chake CCM ambapo wanadai kuwa mwanamama hataweza kuhimili mikiki mikiki ya siasa za bongo kama Rais, na zaidi kama mwenyekiti wa chama.

Taifa linaisubiri kwa hamu hotuba yake ya kesho (22/04/2021) hapo Bungeni Dodoma. Hakika itakuwa ni kama ile hotuba ya Rev MLK - I have a dream. Kuanzia hapo ndio taifa litajua ni upi mwelekeo sahihi wa taifa hili kwa kipindi cha miaka minne iliyobakia. Mama kasema kuwa yeye na hayati ni kitu kimoja lakini kiuhalisia si kweli. Ni kauli za kisiasa tu zile. Yeye ni Samia. Mtazamo wake na wa hayati hauwezi kuwa sawa hata kwa asilimia 70. Hizo 30 ndizo wadau wanazisikilizia, na ndizo zenye kila kitu ambacho watanzania pengine wanataka.

Sasa katika kuenenda huko ndipo yanatokea mambo kadha ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kumkwamisha Rais katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku, hasa wale wanazi wa chama tawala. Ukizingatia pia keshagusia suala la urais ifikapo 2025 ni wazi anajua kuna figisu nyingi zinaendelea huku chini. Jambo la heri ni kwamba, na sisi tumesikia ni kuwa CDF yuko nae.

Jambo lingine la kupendeza ni kwamba CHADEMA kwa wingi wao wameonyesha nia ya wazi ya kumkubali Rais wa sasa katika kutekeleza majukumu yake. Hii ni fursa njema sana kwa pande zote mbili (CDM na Rais). Pia tumesikia katika hotuba ya M'kiti Mbowe kuwa wameshamuandikia Rais barua ya kuhitaji kuonana nae ili kuona kwa pamoja tunasonga vipi mbele kama taifa hasa baada ya kipindi cha mpito cha miaka minne nyuma.

Maandishi haya yananirudisha nyuma kidogo kwa aliyekuwa Rais wa Malawi (Joyce Banda 2012 - 2014) baada ya kifo cha aliyekuwa Rais (Mutharika). Joyce aliingia madarakani kama alivyoingia Samia. Alikutana na hali ngumu ya kiuchumi hadi kuibuka kwa kashfa maarufu iliyoitwa Cash gate. Ulikuwa ni upigaji wa maana ulliofanyika kwenye serikali ambayo yeye alikuwa ni Makamu wa Rais. Hata alipokuwa akijitetea kwa wananchi baada ya kipindi cha urais kuisha, wakati wa kampeni, alikuwa akijitetea kuwa aliibua ufisadi wa kutisha Malawi. Wapinzani walidai kuwa ufisadi wote huo ulifanyika wakati yeye akiwa ni makamu wa Rais, na pengine alifaidika nao, hivyo mwisho hata uchaguzi alishindwa.

Hivyo Rais ana machaguo mawili; kuhakikisha hii ari mpya waliyo nayo watanzania inadumu hasa katika awamu yake hii na baada, au kudemka midundo ya wanazi wa chama chake.

Rais anayo backup ya kutosha toka kwa watanzania bila kujali vyama. Hata kama ndani ya chama chake kutatokea mizengwe, hana haja ya kuunda chama kingine. CDM ipo na ninaamini itampokea ikiona inafaa. Kadhalika Rais anao uwezo wa kubakia ndani ya chama chake akakubaliana na matakwa ya wanazi na hatimaye muda wake ukiisha, aidha urais ubakie huko CCM lakini kwa m-ccm mwingine, au urais uhamie upinzani, hasa tukichukulia mfano wa Malawi.

Yote kwa yote tunamwombea Rais ulinzi kwa Mungu na ulinzi toka taasisi imara na zenye uadilifu. Afanye kazi zake kwa weledi akishirikisha washauri wake pamoja na mawazo ya watanzania pale anapoona inafaa.
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,334
2,000
Sawa wacha tuicheze ngoma mwisho tuone nani fundi, tuingie uwanjani.
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,435
2,000
ccm NI CHAMA imara sana kama hufahamu, hizi figisu hazijaanza leo, labda ulikuwa hujazaliwa kuna kipindi kuliibuka kundi la G55 ndani ya ccm lakini lilieleweshwa na wakongwe likajiona halikujua kitu juu ya tunu ya muungano, hiyo ilikuwa chini ya baba wa taifa.

Mchakato wa katiba ulikuwa mtihani mwingine lakini ccm iliibukA KIDEDEA, bila hata kuwepo mwalimu na baba wa taifa. Mtihani unaojaribu kuuleta hautafua dafu mwaka 2025.

Inafahamika na ni utamaduni wa chama cha mapinduzi kuwa rais aliyeko madARAKANI na mwenyekiti wa chama ndiye na ndiye. Usipoteze muda wako,
 

Jamalm335

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
2,534
2,000
Tatizo hasa lililopo ni mfumo dume uliotujaa watu weusi. Kama makamo wa raisi wa Magufuli angekuwa ni mwanaume leo hii tusingekuwa tunasikia mambo ya kuwa ataweza ama atashindwa.

Tumpe huyu mama nafasi kwa kuangalia mbali zaidi ya jinsia yake. Anaweza kuja kutustaajabisha kwa mazuri mengi atayokuja kufanya endapo tu ataangaliwa kama Raisi wa Tanzania na sio Raisi mwanamke wa Tanzania.
 

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,090
2,000
Tatizo hasa lililopo ni mfumo dume uliotujaa watu weusi. Kama makamo wa raisi wa Magufuli angekuwa ni mwanaume leo hii tusingekuwa tunasikia mambo ya kuwa ataweza ama atashindwa...
Sure, alituambia wakati fulani yeye ndiye Rais katika maumbile ya mwanamke
 

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
928
1,000
Mbowe aliangushwa na konyagi alafu akasingizia amepigwa na wasiojulikana ,mliwahi kumchukulia hatua gani hapo chagadema??
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,539
2,000
Rais akijiunga CHADEMA hapo hapo urais wake unakoma inabidi uchaguzi mpya ufanyike agombee urais kama mwanachama wa CHADEMA.

CHADEMA wengine nyie acheni tamaa ya fisi kutegemea mkono wa mtu uanguke aule, tengenezeni viongozi wenu, pateni ushindi kivyenu.

Hamjajifunza kwa Shibuda, Lowassa na Sumaye tu?
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,435
2,000
Hili la kuhamia upinzani linaweza kufanyika pale ambapo muda wake wa miaka minne umekwisha
Ukihama ccm ndiyo mwisho wako, mama analijua hilo wala hatahangaika kuhamia chadema wakati anajua uimara wa ccm ambayo wewe unasema ni dhaifu. Marehemu I dd Simba aliwahi kusema; usimuone mlevi anapepesuka ukadhani amelewa" hiyo ndiyo ccm
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,520
2,000
Mama Samia alinikosha sana alivyoenda Nairobi kipindi kile kumjulia hali majeruhi Tundu Lissu pamoja na vitisho vilivyokuwepo kipindi kile. Alionesha utu na uungwana wa hali ya juu sana japo kuna kauli yake alikuja kuboronga kipindi cha kampeni ila inavumilika. Ubinadamu ni kitu cha msingi binadamu yeyote kamili anastahili kuwa nacho; kinyume cha hapo ni uhayawani.
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,435
2,000
Chadema hamtajifunza toka 1992 tabia ni zilezile kwa watu wale wale, yaani toka mzee Samuel Malecela akiwa kiongozi hadi leo amestaafu chadema bado tabia zilezile na hamjaijua ccm ambayo ndiyo mshindani wenu. Mnafeli wapi lakini???
 

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,090
2,000
Rais akijiunga CHADEMA hapo hapo urais wake unakoma inabidi uchaguzi mpya ufanyike agombee urais kama mwanachama wa CHADEMA.

CHADEMA wengine nyie acheni tamaa ya fisi kutegemea mkono wa mtu uanguke aule, tengenezeni viongozi wenu, pateni ushindi kivyenu.

Hamjajifunza kwa Shibuda, Lowassa na Sumaye tu?
Mkuu, huyu wa sasa ni mwanamama. Ni mwanaharakati pia. Haitazuia kitu nafasi ya mwisho ya majaribio akipewa mwanamke

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom