Kwa wale wajuzi wa lugha yetu tofauti ya maneno hayo ni nini hasa?
Michango ya wadau
Michango ya wadau
Hayati ni neno la kiarabu likimaanisha uhai, kwa hiyo mtu aliyekufa na kuacha Legacy yaani bado kuna vitu alifanya kwa manufaa ya jamii au dunia na bado vinaishi huyu ndiye huitwa hayati kwa maana kafa lakini bado anaishi kutokana na legacy aliyoiacha wala siyo lazima kuwa maarufu au tajiri.
Hata Masikini anaweza kuacha Legacy, kwa mfano anaweza kusema ana eneo lake ligeuzwe kujengwa shule au hospitali au kisima au msikiti au kanisa na ikafanyika hivyo huyu ni hayati maana kaacha legacy kile alichokuwa akimiliki pamoja na umasikini wake bado kinaishi na kinainufaisha jamii aliyoiacha.
Mwingine anaweza kufundisha ujuzi vijana na wale vijana wakanufaika na ule ujuzi na ukanufaisha jamii, kwa hiyo elimu yake aliyoitoa bado inaishi na inainufaisha jamii huyu naye ni hayati.
Lakini ukifa na kashfa kibao za ufisadi wa mali, ufisadi wa mapenzi au dhulma au uchawi yaani kifo chako kikaleta nafuu kwa jamii, basi wewe ni marehemu tu huwezi kupewa heshma ya kuitwa hayati.
Kwa hiyo kila mtu ajitathmini kama yeye akifa ataitwa Hayati au Marehemu?
Mimi nijuavyo maneno yote mawili marehemu na hayati hutumika kwa kutangulizwa kabla ya kutaja jina la mtu aliyekwisha kufariki.
Lakini tofauti yake ni kwamba neno marehemu linatumika bila kujali kama aliyefariki amefariki leo muda mfupi uliopita, wiki iliyopita, miaka kumi, miaka hamsini au zaidi iliyopita wakati hayati linatumika pale mtu anaezungumziwa habari zake alikuwa ni mtu maarufu katika jamii tena anakuwa alifariki muda mrefu kidogo uliopita pengine miaka kadhaa nyuma mfano hayati Mwalimu Nyerere, hayati Shaaban Robert na wengineo. Pengine ndiyo maana mleta mada umekuwa ukisikia akina "hayati" wachache tofauti na marehemu kwa sababu wengi tunakufa bila umaarufu wowote au kuacha legacy yoyote nyuma yetu.
Sijawahi kusikia mtu aliyefariki mfano leo asubuhi au jana akatanguliziwa jina la hayati.