Kuna tatizo, mungu anaanza kukosea sasa

Kuna tatizo, mungu anaanza kukosea sasa

umemkosea mungu sana kusema amekosea hata kama angekuumba mdomo uko tumboni bado hukupaswa kusema hivo hyo pumzi unayotoa ndo inayokupa hicho kiburi cha kuandika hayo maneno
 
Comments za wengi humu zinaonesha hili suala la tofauti ya kuandika Mungu kwa herufi kubwa na mungu kwa herufi bado linatatiza kwenye uhalisia,na ndiyo maana watu wamemshambulia mleta mada bila kujari hilo suala la herufi ndogo wala kubwa.

Ila sijaelewa mleta mada angeweza vp kufikisha ujumbe wake huu kwa kuongea na si kwa maandishi kama hivi.
 
Wewe ndo umekosea.
Aliyekwambia kuwa hao nì manabii/mitume ni nani?
Vitabu vyao ni vipi?

Hao ni matapeli tu wa mjini.
 
MUNGU HAKOSEI NA HAJAWAHI KUKOSEA. YOTE ALIYOYAUMBA NA KUYAFANYA NI MEMA NA YENYE KUPENDEZA

Hao watu mnaowaita manabii au mitume sijui kitu gani hawajatumwa na Mungu. Msimsingizie Mungu mambo ambayo hajayafanaya hiyo ni KUFURU NA LAANA KUU
 
Kuna kitu kikubwa naona mungu anafanya makosa kwa sasa, nikisoma maandiko mbalimbali nagundua kuwa Mungu alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa awamu.

Si hivyo tu, alikuwa anawaleta kwa uchache tena kwa maeneo maalumu hususani yale korofi. Pia alikuwa anawaleta kwa dalili na hoja zilizo wazi, pia ikitokea zama moja kuwa na manabii au mitume wawili au zaidi kwa wakati mmoja basi walikuwa wanaheshimiana sana.

KOSA, ni hawa manabii aliowaleta leo sijui kwanini amewabadilisha hivi;

1. Wanahubiri zaidi kutafuta na kumiliki mali kuliko ufalme wa Mbinguni.

2. Anawaleta wengi kwa pamoja halafu wengi wanashukia mijini, mfano Dar es salaam pekee si ajabu kukuta manabii au mitume mpaka 10.

3.Mitume na manabii anaowaleta kipindi hiki hawapendani yaani ukiwasikiliza kimtindo utajua wanapondana tu.

4. Huduma za maombi kwa hawa manabii wa sasa ni za kulipia.

5. Wengi ni matajiri wakubwa sana sio kama enzi zile za kina Ayubu, Yusufu Abraham/Ibrahim n.k.

Yako mengi wakuu..
Tena hao Manabii hata huko Dar wamechagua maeneo ya wenye pesa ndo wamejazana. Huwezi kuwakuta kwa wingi maeneo ya Mbagala,Temeke,Gongo la Mboto bali utawakuta Mbezi Beach,Kimara,Tegeta na kwingineko kwenye hela ktk Wilaya za Kinondoni na Ubungo
 
Kuna kitu kikubwa naona mungu anafanya makosa kwa sasa, nikisoma maandiko mbalimbali nagundua kuwa Mungu alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa awamu.

Si hivyo tu, alikuwa anawaleta kwa uchache tena kwa maeneo maalumu hususani yale korofi. Pia alikuwa anawaleta kwa dalili na hoja zilizo wazi, pia ikitokea zama moja kuwa na manabii au mitume wawili au zaidi kwa wakati mmoja basi walikuwa wanaheshimiana sana.

KOSA, ni hawa manabii aliowaleta leo sijui kwanini amewabadilisha hivi;

1. Wanahubiri zaidi kutafuta na kumiliki mali kuliko ufalme wa Mbinguni.

2. Anawaleta wengi kwa pamoja halafu wengi wanashukia mijini, mfano Dar es salaam pekee si ajabu kukuta manabii au mitume mpaka 10.

3.Mitume na manabii anaowaleta kipindi hiki hawapendani yaani ukiwasikiliza kimtindo utajua wanapondana tu.

4. Huduma za maombi kwa hawa manabii wa sasa ni za kulipia.

5. Wengi ni matajiri wakubwa sana sio kama enzi zile za kina Ayubu, Yusufu Abraham/Ibrahim n.k.

Yako mengi wakuu..
Kweli hujielewi unaujua utajiri aliokuwa nao Ayubu au Musa wewe hebu soma Biblia utajua watu matajili walikuwa akinanani
 
MUNGU, kuna mambo hawezi;
Kukosea, kumuonea mtu, kusema uongo,n.k.
Hawa manabii na mitume wa kisasa naona hawakuletwa na Mungu wa Ibrahim,Ayubu,Yusufu,n.k.
Wanakupa neno la mungu Wao na wanakutoza Pesa. Wengine baada neno unapewa Tiba mbadala.
 
Mungu hadhihakiwi. Kwenye biblia maandiko yalitabiri kuwa manabii wa uwongo na wa ukweli watakuwepo. Alishaonya...
.
Hakuna manabii wa ukweli ila kuna nabii wa ukweli kila zama.
.
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
 
nathani kuna sehemu umekuta watu fulani walioghafilika wakijadili haya mambo ya ajabu nawe bila kufikiri na kuchanganya na zako umekuja moja moja hapa. mtume Paulo kupitia Roho Mtakatifu alituambia "kama mtu akijiita basi anayo dhawabu yake lakini kama nimeitwa na Mungu basi nimeaminiwa uwakili" kwa hiyo kwanza inaonesha bado wewe ni chekechekea kabisa kulisoma neno la Mungu alie hai umezoea magazeti kama jina lako lilivyo ndo unakutana na watu wa staili kama yako ya mawazo mfu unafikiri ndio ukweli. unaweza kuwa na uwezo wa ku- critisize saana lakini nataka kukuambia kuna "kweli" ndio neno na wewe umeikosa rudi ukasome uilewe na hivyo unavyosema mungu wako uliemwandika alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa vipindi tofauti sijui hali sjui nini kwani ndivyo mlivyokaa na huyo mungu akakupa hayo majibu ya swali lako au ni mawazo yako unayaandika hapa? usitutanie na Mungu kuwa anakosea labda huyo mungu wako katubu ukasamehewe kwa Jina la Yesu upate ondoleo la dhambi
 
Kuna kitu kikubwa naona mungu anafanya makosa kwa sasa, nikisoma maandiko mbalimbali nagundua kuwa Mungu alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa awamu.

Si hivyo tu, alikuwa anawaleta kwa uchache tena kwa maeneo maalumu hususani yale korofi. Pia alikuwa anawaleta kwa dalili na hoja zilizo wazi, pia ikitokea zama moja kuwa na manabii au mitume wawili au zaidi kwa wakati mmoja basi walikuwa wanaheshimiana sana.

ulipswa umshukuru Mungu kwa kutimiza yake yaliyotabiriwa ...alishatabiri kuwa watatokea watu wa hivyo..sasa kukosea kwake kuko wapi hapo?
 
Nabii Ngwajima yeye gharama yake ni mkeo...muulize mbasha
 
Wewe mleta uzi nadhani una tatizo KU-U-BWA kifikira. Unathubutu kusema Mungu kakosea? Unasema wanaokosea ni watu lakini hapo hapo unasema ni Mungu kawaleta. Una akili timamu kweli? Nani amekwambia ni Mungu amewatuma kufanya huo uovu wanaofanya? Yaani unataka kusema wauaji na wachawi wametumwa na Mungu kufanya uovu wao kwa hiyo Mungu ndiye amekosea kuwaleta duniani? Kwa hiyo Mungu akuue wewe sasa hivi kwa sababu unatenda dhambi (maana hakuna binadamu ambaye hatendi dhambi)?
 
Wengine wanavunja ndoa kwa kufanya mapenzi na wake wa wafuasi wao.
 
Back
Top Bottom