Una uhakika gan kam yeye ndo kawaleta hao?Kuna kitu kikubwa naona mungu anafanya makosa kwa sasa, nikisoma maandiko mbalimbali nagundua kuwa Mungu alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa awamu.
Si hivyo tu, alikuwa anawaleta kwa uchache tena kwa maeneo maalumu hususani yale korofi. Pia alikuwa anawaleta kwa dalili na hoja zilizo wazi, pia ikitokea zama moja kuwa na manabii au mitume wawili au zaidi kwa wakati mmoja basi walikuwa wanaheshimiana sana.
KOSA, ni hawa manabii aliowaleta leo sijui kwanini amewabadilisha hivi;
1. Wanahubiri zaidi kutafuta na kumiliki mali kuliko ufalme wa Mbinguni.
2. Anawaleta wengi kwa pamoja halafu wengi wanashukia mijini, mfano Dar es salaam pekee si ajabu kukuta manabii au mitume mpaka 10.
3.Mitume na manabii anaowaleta kipindi hiki hawapendani yaani ukiwasikiliza kimtindo utajua wanapondana tu.
4. Huduma za maombi kwa hawa manabii wa sasa ni za kulipia.
5. Wengi ni matajiri wakubwa sana sio kama enzi zile za kina Ayubu, Yusufu Abraham/Ibrahim n.k.
Yako mengi wakuu..
well said mkuu...umeniwakilisha vyemaWewe jamma una Laana! Yani ulefikia hatua ya kumkosoa Muumba wa Mbingu kama hauna la kusema si ukae kimya kwani lazma uwanzishe Uzi
Hapo Dar hakuna Mtume wala Nabii hao wote ni Waongo matapeli wa mjini siku moja aliojiwa mtu mmoja anaedai kuwa yeye ni Mtume na kituo cha TBC akiwa kavaa suti na Cheni Shingoni sasa kweli Mtume / Nabii anaweza kuvaa Cheni shingoni?
Bila shaka hawa ndio walinganizi wanao waita watu kuingia Motoni ?
Hawa Wanaojiita Mitume/Manabii ni watu waovu sana kuliko hata walevi wa Kilabuni...!
Mzee wa kurekebisha saf sanaa jwel w n great thinkerMtoa Mada ana akili sana unatakiwa utulie uweze kumuelewa Angalia hizi sentesi.
kuna kitu kikubwa naona mungu anafanya makosa kwa sasa
nikisoma maandikombalimbali nagundua kuwa Mungu alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa
awamu
Mtoa mada anazungumzia pande mbili tofauti mungu ambaye anakosea na Mungu ambaye aliwaleta
manabii enzi hizo.
ACHENI KUCHEZA NA MUNGU NYIE TENA TUBUNI SASA!!!!!!!!!kweli mungu kuna sehemu amekosea, tena amekosea sana!!
Mkuu hujamuelewa mleta mada. Msome vizuri tu utamuelewa, wala hamzungumzii Mungu huyu aliyetuumba mimi na wewe.ACHENI KUCHEZA NA MUNGU NYIE TENA TUBUNI SASA!!!!!!!!!
Unataka kutuambia Hawa wote tunaowasikia matapeli?Kuna kitu kikubwa naona mungu anafanya makosa kwa sasa, nikisoma maandiko mbalimbali nagundua kuwa Mungu alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa awamu.