GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,281
- 6,697
Kuna kitu kikubwa naona mungu anafanya makosa kwa sasa, nikisoma maandiko mbalimbali nagundua kuwa Mungu alikuwa anawaleta mitume na manabii kwa awamu.
Si hivyo tu, alikuwa anawaleta kwa uchache tena kwa maeneo maalumu hususani yale korofi. Pia alikuwa anawaleta kwa dalili na hoja zilizo wazi, pia ikitokea zama moja kuwa na manabii au mitume wawili au zaidi kwa wakati mmoja basi walikuwa wanaheshimiana sana.
KOSA, ni hawa manabii aliowaleta leo sijui kwanini amewabadilisha hivi;
1. Wanahubiri zaidi kutafuta na kumiliki mali kuliko ufalme wa Mbinguni.
2. Anawaleta wengi kwa pamoja halafu wengi wanashukia mijini, mfano Dar es salaam pekee si ajabu kukuta manabii au mitume mpaka 10.
3.Mitume na manabii anaowaleta kipindi hiki hawapendani yaani ukiwasikiliza kimtindo utajua wanapondana tu.
4. Huduma za maombi kwa hawa manabii wa sasa ni za kulipia.
5. Wengi ni matajiri wakubwa sana sio kama enzi zile za kina Ayubu, Yusufu Abraham/Ibrahim n.k.
Yako mengi wakuu..