Kiukweli mtoa mada kakosea sana kumkosoa mungu ila wewe nawe unazidi kuwachanganya wenzako maana mitume na manabii wote wa sasa wanaamini katika yesu kuwa ni mungu sasa wewe unawaambia warudi Kwa yesu naomba kujua yesu wako wangapi?
Nitafafanua kidogo
1. mungu aliyeandikwa ni mmoja wa miungu . Angeandika Mungu ningeelewa. angalia herufi ya kwanza M= Mungu wa kweli lakini m ndogo ni miungu. ndivyo biblia husema.
2. Biblia inasema kuwa nyakati za kurudi kwa yesu basi watatikea manabii wengi wa uwongo wakitumia jina la yesu kufanya miujiza. lakini tunaaswa kuwa makini na kuomba sana. Hivyo hao manabii wanaimaba yesu lakini sio wakweli
mafungu ya biblia - agano la kale na manabii wa uwongo
1 Wafalme 22:22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo
Yeremia 23:25 Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto.
Yeremia 14:14 Ndipo Bwana akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao.
Yeremia 23:26 Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe?
Yeremia 27:15 Kwa maana mimi sikuwatuma, asema Bwana, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria.
Ezekieli 22:28 Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiona ubatili, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo Bwana hakusema neno.
agano jipya - biblia yasema
Mathayo 7:15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mathayo 24:11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
Mathayo 24:24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Marko 13:22 kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.
Luka 6:26 Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.
2 Petro 2:1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
1 Yohana 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
NAWASILISHA Nafikiri sasa umeelewa mkuu habari na utendaji kazi - hivyo kuepuka na kuomba sana tuwakimbie!!