Kuna tatizo la msingi B.O.T.

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,946
3,685
Nilienda B.O.T kwa ajili ya kupata salary slip niweze kukopa Bank.Nilikuwa na utambulisho kutoka kwa Mwajiri wangu ukionyesha kwamba salary slip zangu zinapelekwa Bukoba kimakosa badala ya kituo changu halisi ambacho kipo DSM.Baada ya kumwona mhusika mmojawapo alinishauri nirudi baada ya siku mbili maana mtambo wa kutoa salary slip mojamoja umeharibika na utatengemaa ndani ya siku hizo Mbili.Baada ya siku mbili nilifika tena Ofisi ile na niliyemkuta pale akaniambia Mtambo wa kutolea salary slips mojamoja uliharibika siku nyingi na hana jinsi ya kunisaidia.
Kwa sababu ya mpishano wa maelezo kati ya hawa maafisa wawili niliomba kuonana na 'incharge'wao.Waliniitia bwana mmoja ambaye kwanza nilimtilia shaka maana alikuwa ananuka pombe na ndio kwanza saa nne asubuhi.Yeye alinijibu bila kuuma maneno kwamba wanachokifanya pale ni Msaada tu na hawaoni sababu ya kunipa hiyo salary slip.Niliondoka nikiwa nimenyong'onyea maana ndio nilikuwa naitegemea kwa ajili ya mkopo ili nimlipie mwanangu karo ya shule.Cha kusikitisha zaidi mwenzangu aliyekuwa na matatizo kama yangu yeye alifanikiwa kuipata ya kwake.
Ninachohoji hapa ni kwa nini B.O.T wafanye kazi kwa MSAADA badala ya misingi ya kazi?Hawaoni kwamba msaada huo ni mwanya kwa wapenda rushwa na wafanyakazi wasio waadilifu?.Sasa kama pako hivyo Benki kuu,ni Taasisi gani ya serikali ipo salama?
 
Back
Top Bottom