Kuna tatizo Chadema hilo lazima tukubali

Kuna tatizo Chadema hilo lazima tukubali

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,470
Reaction score
13,621
Sijawahi kuipenda CCM toka nimepata uelewa wa vitu. Mwanzoni kabisa nilikua naipenda CUF, ila katika miaka ya 2005-2010 siasa za Zitto pamoja na Dk. Slaa zilinivutia sana eventually nikajikuta nasupport CHADEMA. Miaka kadhaa ikapita Zitto akafukuzwa chama kwa maneno mengi sana kama in sellout na ilikua in kipindi kama hiki kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015.

Katika utetezi wake ndugu Zitto alidai matatizo yote ndani ya CHADEMA yalianza baada ya yeye kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya chama ila hakuambulia alichotegemea akapata label ya kua anatumika. Na leo tena same case imetokea kwa Mzee Sumaye baada ya kuonyesha azma ileile, naye figisu zikaanza. Na laiti angekua kijana mwenye nguvu pia angeshtumiwa/atashutumiwa kutumiwa na serikali.

GuDume ana Uzi wake humu ndani akiuliza wapinzani wa Tanzania wanataka nini? Na mimi nakazia kwa kua very specific CHADEMA mnataka nini?
 
Kumekuwa na tetesi za muda mrefu ambazo zninatokana na wanachama wa CHADEMA wanaonesha nia ya kugombea uongozi taifa kwa ngazi ya uenyekiti madhara yanayo watokea na figisu zinazo watokea zipo zimeweza kudhibitishwa na kudhibitika ipo mifano kadhaa ya wazi ya baadhi ya wanasiasa hao wamefukuzwa au kuhama chama kwa tuhuma nzito zinazo wafanya wahame au waokufukuzwa katika mazingira pia na matukio mengine mengi hatarishi ambayo yamekuwa yakiwatokea na kuyahushishwa matukio hayo na nia zao za kuonesha nia ya kugombea kiti cha uenyekiti taifa kilinachokaliwa na Mhe. Mbowe kwa zaidi ya miaka 15 sasa

Pia kutokana na kasheshe hii ya ngazi ya mwenyekiti taifa ndani ya CHADEMA kuwa ni ngumu kuipata na nafasi ambayo haigusiki kwa zaidi ya miaka hiyo pia katika mkutano wake aliekuwa mwenyekiti wa CHADEMA ngazi ya kanda, kanda ya Pwani na waziri mkuu mstafu wa jamhuri wa muungano wa Tanzania amewaeleza na kuwathibitishia waandishi wa habari jinsi na namna amabavyo amefikwa na kadhia hizo ambazo hata walio tangulia na kupitia hayo wali wahi kueleza ndiyo yale yale Mhe. SUMAYE amekithibitisha mbele ya waandishi wa habari. Mbali na SUMAYE pia wapo wanachama wamejitokeza na kutoa malalamiko yao akiwemo KUBENEA, KOMU na MWAMBE hii ndyo hali iliyo ndani ya chama kinacho jinasibu kuwa cha Demokrasia .

Ofisi ya msajili wa vyama nchini atuambie kanuni na masharti gani ambayo yanakiukwa na vyama vya siasa ktk mfumo wa kujiiendesha na kama zipo kanuni zinazokiukwa ni hatua gani? zistahili kuchukuliwa dhidi ya vyama hivyo kwani malalamiko haya hayaja anza kusikika leo baada ya Mhe. Sumaye huu ni mwendelezo tu matukio ya aina hii kuendelea kutokea ambayo bila shaka mwelekeo wake siyo mzuri kwa usitawi na ukuwaji wa demokrasia nchini.
 
John Heche kapokea Kijiti cha Sumaye kama Sumaye alivyopokea cha Zitto kama Zitto alivyopokea cha Chacha Wangwe

Mie naunga mkono juhudi za Feeeman Mbowe

Mbowe mjanja sana , kimya cha Lissu kilimvuruga akajikuta kamtega awanie U Makamu mwenyekiti ili yeye abaki kwenye ‘ardhi yenye rutuba ‘
 
huku ni kupakaza

mr zero kashindwa uchaguzi wa kanda huo wa ngazi ya Taifa angewaniaje bila kupita ngazi ya kanda.?

au mie sielewi..

MNYONGE mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Naomba kujuzwa namna kiti cha uwenyekiti CCM kinavyowaniwa? ukianzia pale kwenye form za kuomba uwenyekiti huo, mchujo wa wagombea kupitia kamati za chama, upigwaji wa kura na hatimaye mshindi kutangazwa...

Hawa wa vyama vya upinzani kujifunza toka chama tawala ni jambo jema.
 
Tatizo hakuna mkaskazini aliyeandaliwa kumrithi Mbowe....... ndiposa wanafikiria ubishani ukizidi itabidi Halima Mdee avae viatu vya Mbowe!
Hii hoja ya Ukaskazini huenda ikawa ina mashiko ila Sumaye mbona yeye mbona ni wa Kaskazini, au sio mkaskazini enough?
 
John Heche kapokea Kijiti cha Sumaye kama Sumaye alivyopokea cha Zitto kama Zitto alivyopokea cha Chacha Wangwe

Mie naunga mkono juhudi za Feeeman Mbowe

Mbowe mjanja sana , kimya cha Lissu kilimvuruga akajikuta kamtega awanie U Makamu mwenyekiti ili yeye abaki kwenye ‘ardhi yenye rutuba ‘
huyu mtu ni noma aise yuko vizur ngoja aendlee kula ruzuku
 
Sumaye Kaja Chadema Juzi halafu awe mwenyekiti wa Taifa ni aibu.

Huyu Komu, Kubenea, na Mwambe wasipohamia CCM kabla ya 2020 Njoo hapa nidai 100,000
Afadhali basi angekuwa na hoja za ushawishi kama Tundu Lissu
 
Back
Top Bottom