Kuna tatizo Chadema hilo lazima tukubali

Kuna chadema wapinzani wa kweli na chadema maslahi. Hawa maslahi Wana nguvu Sana kwenye Mambo ya ndani ya chama. Ni kundi hatari ukigusa madaraka na maslahi yao.

Chadema wapinzani wa kweli hawa hawapo kimaslahi. wanachotaka kuona Ni chama kinakua na nguvu lakini kinaendeshwa vizuri katika misingi ya UWAZI, haki na katiba kwa kila mwanachama.
 
Ningependa sana kuona demokrasia inashamiri ndani ya CHADEMA. Ningependa kuona watu wenye uwezo, imani thabiti na wenye upeo mkubwa na mbinu mpya tofauti tofauti wanapokezana uongozi kwenye ngazi zote ndani ya CHADEMA.

Lakini nia isiwe kupokezana tu. Yaani mtu yeyote hata kama hana uwezo au imani yake kwa chama ni ya mashaka mashaka, anapewa uongpzi kwa vile tu mnataka mabadiliko ya uongozi.

Mbowe katika ngazi ya Taifa, atengeneze viongozi wanaoaminika. Wenyeviti wa kanda watengeneze viongozi wanaoaminika. Hiyo iwe ni kwa ngazi zote.

Uongozi mpya huleta hamasa mpya na hamu ya watu kutaka kuona uongpzi mpya unaleta nini kipya. Uongozi mpya unaweza kuleta fikra mpya, mawazo mapya na mbinu mpya. Ushauri wangu ni kuwa Lisu ambaye anategemea kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa apewe uhuru mkubwa na Mbowe afanye kazi kama kiongozi mlezi wa Chama. Na ukifika muda fulani, hata kabla ya muda wake kwisha, anaweza kuiachia nafasi yake kwa Tundu Lisu. Hapa naongelea CHADEMA ambayo inastahili kutoa funzo kwa CCM.

CCM haina demokrasia hata ndogo kabisa kwenye uongozi wa Kitaifa. Mwenyekiti wa CCM wa Taifa anapewa tu umwenyekiti. Hakuna kugombea hakuna upigaji kura. Halafu huyo ambaye amepewa tu uongozi anawateua viongozi wakuu. Huu ni udikteta wa hali ya juu. CCM hawana yeyote wa kumfundisha demokrasia kwa sababu wao wenyewe hawana. Huwezi kumpa mtu mwingine kitu ambacho huna. CCM wanachokifanya ni maigizo ya kiujanjaujanja.
 
Hii hoja ya Ukaskazini huenda ikawa ina mashiko ila Sumaye mbona yeye mbona ni wa Kaskazini, au sio mkaskazini enough?
Kaskazini ina mikoa mingi kama Tanga,Kilimanjaro,Arusha,Manyara

So sema KASKAZINI UCHAGANI(KLM) NDO WAMILIKI WA CHADEMA.
Sumaye anatokea Arusha
 
Ngoja wapambe wa mbowe waje wakushambulie hadi u log off Jf

Unamfahamu tindo Salary Slip n.k ?
Naomba tuwe wakweli, yaani Sumaye utoke CCM (kama kweli ulitoka kwa kuwa hukurudisha kadi yako ya CCM) miaka minne (4) and then ukabidhiwe uenyekiti wa CHADEMA!! Nenda kajaribu hata TLP au CUF uone utakavyotimuliwa na mzee wa Kiraracha ama Professor wa CUF. Kuna 'wafia chama' ambao wamepoteza mali, hadhi hata kufungwa, wewe hujawahi kushuhudia bomu la machozi upewe uenyekiti wa chama!!! Nenda CCM uonyeshe tu dalili za kuutaka uenyekiti wa CCM Kitaifa kama hutajuta kuzaliwa. Kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM walishindwa kukuamini sembuse uenyekiti wa chama!! Nakushauri ustaafu siasa, usipende kuanzisha mitafaruku 'Feki'.
 
Afadhali basi angekuwa na hoja za ushawishi kama Tundu Lissu
Tundu Ana hoja gani Yule..mbona mweupe Sana..akili yake kwanza bado haijakomaa..nadhan sababu ya umri..kazi yake ni kutetea tumbo lake tu
 
Naomba tuwe wakweli, yaani Sumaye utoke CCM (kama kweli ulitoka kwa kuwa hukurudisha kadi yako ya CCM) miaka minne (4) and then ukabidhiwe uenyekiti wa CHADEMA!! Nenda kajaribu hata TLP au CUF uone utakavyotimuliwa na mzee wa Kiraracha ama Professor wa CUF. Kuna 'wafia chama' ambao wamepoteza mali, hadhi hata kufungwa, wewe hujawahi kushuhudia bomu la machozi upewe uenyekiti wa chama!!! Nenda CCM uonyeshe tu dalili za kuutaka uenyekiti wa CCM Kitaifa kama hutajuta kuzaliwa. Kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM walishindwa kukuamini sembuse uenyekiti wa chama!! Nakushauri ustaafu siasa, usipende kuanzisha mitafaruku 'Feki'.
Ilikuwaje Sasa mbona Lowasaa alifika na ku overtake akachukua nafasi ya kugombea urais, mkataka mumsukumie Ikulu hivyohivyo...hahahah
 
Biashara ya mtu haiingiliwi hovyo hovyo,
Hiyo nafasi ya mwenyekiti ni Mali yake binafsi hivyo si rahisi kukiacha kiti kizembe.
Ole wake awaye yeyote atakayejaribu kukitamani kiti hicho.
 
Sijawahi kuipenda CCM toka nimepata uelewa wa vitu. Mwanzoni kabisa nilikua naipenda CUF, ila katika miaka ya 2005-2010 siasa za Zitto pamoja na Dk. Slaa zilinivutia sana eventually nikajikuta nasupport CHADEMA. Miaka kadhaa ikapita Zitto akafukuzwa chama kwa maneno mengi sana kama in sellout na ilikua in kipindi kama hiki kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015.

Katika utetezi wake ndugu Zitto alidai matatizo yote ndani ya CHADEMA yalianza baada ya yeye kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya chama ila hakuambulia alichotegemea akapata label ya kua anatumika. Na leo tena same case imetokea kwa Mzee Sumaye baada ya kuonyesha azma ileile, naye figisu zikaanza. Na laiti angekua kijana mwenye nguvu pia angeshtumiwa/atashutumiwa kutumiwa na serikali.

GuDume ana Uzi wake humu ndani akiuliza wapinzani wa Tanzania wanataka nini? Na mimi nakazia kwa kua very specific CHADEMA mnataka nini?
Sema kuna tatizo Tanzania.Ni wapi na kwa Katiba ipi inazuia mtu kumpinga Rais/Mwenyekiti ktk uchaguzi wowote kama siyo Tanzania pekee?
Kwa CHADEMA tatizo,KWA CCM NI UTAMADUNI! Kweli kuku tu ndiye hunya!
 
Songela Nkese!
 
Sumaye Kaja Chadema Juzi halafu awe mwenyekiti wa Taifa ni aibu.

Huyu Komu, Kubenea, na Mwambe wasipohamia CCM kabla ya 2020 Njoo hapa nidai 100,000
Ila lowasa kuwa Rais ni sawa, kumbuka na yeye alikuwa mgeni
Dr Bashir Ally katokea CUF mbaka kuwa katibu mkuu ccm ajabu nn?
 
Naomba tuwe wakweli, yaani Sumaye utoke CCM (kama kweli ulitoka kwa kuwa hukurudisha kadi yako ya CCM) miaka minne (4) and then ukabidhiwe uenyekiti wa CHADEMA!! Nenda kajaribu hata TLP au CUF uone utakavyotimuliwa na mzee wa Kiraracha ama Professor wa CUF. Kuna 'wafia chama' ambao wamepoteza mali, hadhi hata kufungwa, wewe hujawahi kushuhudia bomu la machozi upewe uenyekiti wa chama!!! Nenda CCM uonyeshe tu dalili za kuutaka uenyekiti wa CCM Kitaifa kama hutajuta kuzaliwa. Kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM walishindwa kukuamini sembuse uenyekiti wa chama!! Nakushauri ustaafu siasa, usipende kuanzisha mitafaruku 'Feki'.
Lowassa alitoka CCM miaka mingapi??
 
Hao Lapdogs wanaotetea kila ujinga labda waendelee kuwa misukule milele otherwise wataondoka siku watayojitambua na ku-violate interest za Sultan.

Yupo wapi Dr Slaa si alikuwa loyal kwa Mbowe miaka yote!
 
Naomba tuwe wakweli, yaani Sumaye utoke CCM (kama kweli ulitoka kwa kuwa hukurudisha kadi yako ya CCM) miaka minne (4) and then ukabidhiwe uenyekiti wa CHADEMA!! Nenda kajaribu hata TLP au CUF uone utakavyotimuliwa na mzee wa Kiraracha ama Professor wa CUF. Kuna 'wafia chama' ambao wamepoteza mali, hadhi hata kufungwa, wewe hujawahi kushuhudia bomu la machozi upewe uenyekiti wa chama!!! Nenda CCM uonyeshe tu dalili za kuutaka uenyekiti wa CCM Kitaifa kama hutajuta kuzaliwa. Kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM walishindwa kukuamini sembuse uenyekiti wa chama!! Nakushauri ustaafu siasa, usipende kuanzisha mitafaruku 'Feki'.
Mbona lowassa siku 3 tu mkampa dhamana ya kuwa Rais kama angeshinda

Au uenyekiti chadema ni mkubwa kuliko nafas ya urais wa nchi?
 
Uimara wa Mbowe ndio uimara wa CDM..

Mbowe shikilia hapo hapo kwa manufaa ya upinzani wa Tanzania na uhai wa CDM..

Uenyekiti CDM hauhitaji watu legelege, watu njaa njaa, wasaka fursa na maslahi bali unahitaji watu wenye dhamira ya dhati katika kupigania maslahi ya upinzani na Tanzania..

Wahamiaji wote waliotoka CCM na ule upepo wa Lowasa ni wasaka fursa na maslahi, wahamaji wote waliotoka CDM kwenda CCM na wengine kukacha siasa eti kwa kuwa Slaa aliwekwa pembeni nao walikuwa wasaka fursa na wasaka maslahi..

Nauona upinzani unakwenda kuimarika chini ya CDM na ACT kupitia MBOWE, ZZK, SEIF, JUSA nk..
 
Mkuu ukiangalia kwa jicho la kawaida unaweza kuona kama wanaonewa lkn ukweli ni kwamba kuwa kiongozi wa chama cha upizani ni zaidi ya kuwa kiongozi.
I stand to be corrected
Sijawahi kuipenda CCM toka nimepata uelewa wa vitu. Mwanzoni kabisa nilikua naipenda CUF, ila katika miaka ya 2005-2010 siasa za Zitto pamoja na Dk. Slaa zilinivutia sana eventually nikajikuta nasupport CHADEMA. Miaka kadhaa ikapita Zitto akafukuzwa chama kwa maneno mengi sana kama in sellout na ilikua in kipindi kama hiki kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015.

Katika utetezi wake ndugu Zitto alidai matatizo yote ndani ya CHADEMA yalianza baada ya yeye kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya chama ila hakuambulia alichotegemea akapata label ya kua anatumika. Na leo tena same case imetokea kwa Mzee Sumaye baada ya kuonyesha azma ileile, naye figisu zikaanza. Na laiti angekua kijana mwenye nguvu pia angeshtumiwa/atashutumiwa kutumiwa na serikali.

GuDume ana Uzi wake humu ndani akiuliza wapinzani wa Tanzania wanataka nini? Na mimi nakazia kwa kua very specific CHADEMA mnataka nini?
 
Sumaye Kaja Chadema Juzi halafu awe mwenyekiti wa Taifa ni aibu.

Huyu Komu, Kubenea, na Mwambe wasipohamia CCM kabla ya 2020 Njoo hapa nidai 100,000
Vilevile hawajakatwa kama kule ng'ambo kwa wenzetu,wanashindwa kura hatoshi,na wengine bado wapo kwenye kinyang'anyilo cha taifa mbowe anasema kama wapo wengine wachukue form
 
Back
Top Bottom