Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,639
- 729,583
Kuna hiki kitu tabia hulka au mazoea, ni kitu tunachokuwa nacho na kamwe hakiepukiki kinakuwa ndani mwetu na kuna wakati ni kama utambulisho wetu na hiki kitu huwa nawe mpaka mwisho wa maisha yako na huja kuleta athari hata kwenye mazishi yako.
Mifano hii michache
1. Kama ulikuwa mvivu goigoi na mtu wa kuchelewa kila mahali hata msiba wako utakuwa hivyo hivyo..kutakuwa na uchelewaji mwingi kwenye chochote bila sababu .
2. Kama ulikuwa mchafu na mtu usiye na mipangilio katika maisha yako hata msiba wako utakuwa shaghala baghala mpaka kwenye misosi .
3. Kama ulikuwa mwizi kibaka jambazi nk hata msiba wako utaandamwa na hayo matukio, lazima kati ya ndugu au waombolezaji baadhi walizwe.
4. Kuna watu mambo yao yalikuwa na mpangilio na kujali muda hawa huwa hivyo hivyo mpaka mwisho wao
Hakuna anayependa kuacha jina baya baada ya kufa hakuna anayependa kusemwa vibaya kila mtu hupenda kusemwa na kunenewa mazuri na sifa kemkem.
Bado uko hai una nafasi ya kurekebisha mienendo yako kuanzia mahusiano yako na watu mpaka mambo yako binafsi ili Usiwe kikwazo na kuacha simulizi mbaya baada ya kutwaliwa kutoka maisha haya.