Mlimani health center
JF-Expert Member
- Nov 25, 2021
- 600
- 1,526
Miaka michache iliyopita kulikuwa na dada mmoja ambaye nilikuwa namfahamu kwa mbali. Alikuwa mfanyabiashara.
Kwenye mitandao ya kijamii alikuwa anaonekana kuishi maisha ambayo wengi walikuwa wanayatamani. Mara vacation, hoteli za kifahari, simu za gharama, shopping za kila mara. Ukiangalia picha zake, ungeamini hana tatizo lolote la maisha.
Wengi wetu tulikuwa tunasema, "Huyu maisha yake yamekaa." Kila mtu alikuwa na tafsiri yake kuhusu chanzo cha mafanikio yake.
Lakini siku moja zikaja taarifa za kusikitisha kuwa amefariki akiwa anapatiwa matibabu.
Baada ya msiba ndipo baadhi yetu tulipopata nafasi ya kufika nyumbani kwao. Kilichotukuta kilitufundisha somo ambalo sitalisahau. Nyumba ilikuwa ya kawaida sana, mazingira yalionyesha familia inaishi maisha ya kawaida yenye changamoto nyingi.
Hata maandalizi ya msiba yalikuwa ya uwezo wa kawaida wa familia—tofauti kabisa na picha ya maisha ya kifahari aliyokuwa akiionyesha mitandaoni.
Ndipo nikagundua kuwa mara nyingi tunavutiwa na kile tunachokiona kwenye mitandao, bila kujua uhalisia wa maisha ya mtu.
Somo langu si la kumhukumu marehemu wala familia yake. Ni kutukumbusha sisi tulio hai kwamba tusiishi kwa ajili ya kuonekana. Usiingie kwenye madeni au kujitesa ili watu waseme una maisha mazuri. Mitandao inaonyesha sehemu ndogo tu ya maisha ya mtu, si hadithi yake yote.
Ishi maisha yanayokupa amani, si maisha yanayowavutia watu. Mwonekano unaweza kudanganya, lakini uhalisia hujitokeza siku zote.