Kuna siri gani ya mume kutangulia kufa?

Kuna siri gani ya mume kutangulia kufa?

Imejengeka nadharia kwamba mkioana mwanaume ndiye atatangulia kufa. Ndio maana kuna dhana ya ujane na wajane wana taasisi zao kusaidiwa na kujisaidia. Ina maana wanaume ndio wanakufa zaidi kuliko wanawake
Ujane na taasisi za kusaidia wajane pia inachangiwa na mfumo dume tulionao. Wanawake wengi wanajikuta wakidhulumiwa mara waume wao wanapofariki na mila nyingi zilikuwa hazitoi haki ya urithi kwa wajane.
 
Wanabodi napenda kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kutulinda na kutufikisha siku ya leo.Pili nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli Laigwanan Edward Ngoyayi Lowasa kilichotokea tarehe 10/02/2024.Pia nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha ghafla cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga wakili msomi Imani Madega ambaye naye amefariki tarehe moja na Lowasa.Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.Baada ya kupokea taarifa za misiba hii mikubwa kwa taifa letu,binafsi nikawa nawaza kuhusu namna ambavyo wanaume ndio mara nyingi wanatangulia na kuwaacha wake zao.Nikajaribu kupitia orodha ya watu maarufu waliofariki na kuacha wake zao ikawa ni ndefu mno kwa kifupi naomba nitoe japo kwa uchache:-
1.Abeid Amani Karume(Mkewe yupo hadi leo)
2.Edward Moringe Sokoine
3. Aboud Jumbe Mwinyi
4. Mwalimu Nyerere
5. Ben Mkapa
6. JP Magufuli
7. Dr. Omary Ally Juma
8. Maalim Seif Sharifu Hamad
9. Bernard Camillius Membe
10.Kapten John Komba
11. Moses Nnauye
12. Jomo Kenyatta
Listi ni ndefu sana.Sina maana kwamba wanawake ndio watangulie ila kwetu kama wanadamu na waja wa Mwenyezi Mungu tunajifunza nini?
Nawasilisha.
Imeandikwa mke atarithi mali za mumewe, hakuna sehemu inayosema mume atarithi mali za mkewe hata hivyo unaweza kukwepa kutangulia kufa kwa kuamua kuacha kuoa.
 
Mwanaume hana uwezo mkubwa wa kuhimili na kustahimili ugumu wa maisha kama mwanamke.

Hata watu wakishinda njaa siku 7, mwanaume atawahi kufa.

Mwanamke anaweza akalia na sumu kwenye fahamu ikaisha ila siyo mwanaume.

Wanaume bado ndiyo wenye kufanya kazi hatarishi.

Ninasisitiza kazi hatarishi

Hata kwenye mapenzi mwanaume ndiye anamwaga uji uji na mwanamke anaunywa na kusema asante baby.

Lakini bado kuna watu watasema Wanawake wa Kichagga wanaua waume zao.
 
Niataeleza Kwa upana wa uelewa wangu:-

1.Ki Baiyolojia.
-wanaume tunazalisha Hadi uzeeni yaani tunaendelea kuwa na hamu ya kufanya ngono Hadi uzeeni ndio maana tunaoa hadi wajukuu,lakini kina mama Wana menopause ambayo huwasaidia kutunza virutubisho vyao hadi Hadi ubibi kizee!!kadiri mwanaume anavyofanya ngono ndivyo anavyokaribia kifo,IPO Siri katika kutofanya ngono ndio maana watawa wengi au jamii nyingi za siri hujitenga na ngono !!

2.Kiuchumi.

-Bado Sana sekta ya uzalishaji inaaminika ni ya wanaume yaani shughuli au kazi zote za nguvu na risky tunafanya sisi wanaume kwahiyo ajali,ulemavu,kupata sumu zinazoathiri mapafu,moyo,figo n.k hii inasababisha lifespan ya mwanamme kuwa fupi!

3.kijamii

Majukumu makubwa kenye familia,ukoo na jamii kapewa mwanamme ndio mtatuzi was changamoto za mahitaji ya wote,huu msalaba wanawake wamewatubebesha sisi hasta kama uwezo wanao,Hilo huleta sonona kwasababu ni ngumu kutimiza mahitaji ya wazazi,familia Yako na wazazi was mke wako Kwa pamoja,Bado presha ya kutotimiza hayo inamuandama Kila siku!!

4.kisiasa

Bado sisi ndio tuna tazamiwa kupigania uongozi kufa na kupona na hio huleta maadui ndani na nje ya familia,kifo hakiepikiki Kwa style hiyo!!

5.Ulozi,maagano na laana

Kila mwanamme Hadi anafikisha miaka 50 ameshajaribu mengi Santa katika utafutaji,ulozi na uganga hadi maagano mabaya keshajaribu ambayo Yana matokeo.chanya au hasi huko mbeleni!!

Laana za watoto,wapenzi wazazi kutokana na kutotimiza matarajio Yao pia zinatuandama kila kukicha!

Kurogwa au kuchezewa shere pale unapopata unafuu.wa maisha pia hufanya maisha yetu kuwanmafupi!

Ukufuatilia sana kwenye ukoo au familia wanaume tuliofanikiwa ndio hufa mapema.sana.wakiacha mali ambazo.wakati mwingine hazidumu!

Ni kuwindwa na.kuwindana Hadi siku.unaenda!!Hilo nimeona sana!!


Wengine wanaweza ongezea!!
 
Back
Top Bottom