Kuna siri gani ya mume kutangulia kufa?

Kuna siri gani ya mume kutangulia kufa?

Kifo ni siri ya Mungu,japo utapata majibu mengi tu hapa ila uhai wa Binadamu mpaka kufa kwake hupangwa na Mungu,

Hao uliowataja ni watu maarufu tu ndio maana tumewajua,swali lako lingependeza zaidi kama tungeweka orodha ya watanzania wote wajane ambao wamefiwa na waume zao.
aweke orodha ya watanzania wote wajane ili iweje, unataka kuwafufua.
hiyo ya kupangwa na Mungu siyo kweli ,ila anajua mwanzo wetu na mwisho wetu pia
 
aweke orodha ya watanzania wote wajane ili iweje, unataka kuwafufua.
hiyo ya kupangwa na Mungu siyo kweli ,ila anajua mwanzo wetu na mwisho wetu pia
Mbona unakua mjinga kiasi hicho? ni wapi nimemwambia mleta mada aweke orodha ya wajane wote?

Nimeandika hivi swali lako lingependeza zaidi kama tungeweka orodha ya watanzania wote wajane ambao wamefiwa na waume zao elewa neno tungeweka,

Hivi unazijua hata kanuni za kufanya research au unaropoka tu?

Unataka mpaka kubishana na imani yangu kua kifo hakipangwi na Mungu? kama unapingana hilo na mimi inakuweje wewe unaamini kua Mungu anajua mwanzo wetu na mwisho wetu? kwahiyo kifo cha Binadamu hupangwa na nani?
 
Miaka ya sasa na tunapoelekea hakutakuwa na msemo wa tutakufa na kuzikana kwa wapendanao.
 
Wanabodi napenda kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kutulinda na kutufikisha siku ya leo.

Pili nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli Laigwanan Edward Ngoyayi Lowasa kilichotokea tarehe 10/02/2024.Pia nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha ghafla cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga wakili msomi Imani Madega ambaye naye amefariki tarehe moja na Lowasa.Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Baada ya kupokea taarifa za misiba hii mikubwa kwa taifa letu, binafsi nikawa nawaza kuhusu namna ambavyo wanaume ndio mara nyingi wanatangulia na kuwaacha wake zao. Nikajaribu kupitia orodha ya watu maarufu waliofariki na kuacha wake zao ikawa ni ndefu mno kwa kifupi naomba nitoe japo kwa uchache:-

1.Abeid Amani Karume(Mkewe yupo hadi leo)
2.Edward Moringe Sokoine
3. Aboud Jumbe Mwinyi
4. Mwalimu Nyerere
5. Ben Mkapa
6. JP Magufuli
7. Dr. Omary Ally Juma
8. Maalim Seif Sharifu Hamad
9. Bernard Camillius Membe
10.Kapten John Komba
11. Moses Nnauye
12. Jomo Kenyatta
Listi ni ndefu sana.Sina maana kwamba wanawake ndio watangulie ila kwetu kama wanadamu na waja wa Mwenyezi Mungu tunajifunza nini?
Nawasilisha.
Kisayansi, mume mara nyingi ndio huwa na umri mkubwa kuliko mume, mume anapitia stress na hatari nyingi zinazozoofisha afya akipambana kulisha mke na watoto, mengine ni ajali tu za maisha.

hata hivyo, kifo sio ni kizuri kama unakoenda ni motoni, ila kama unaenda moja kwa moja kwenye shimo la kuzimu ni kitu hatari na cha kuogofya, mpe Yesu maisha yako ili ukifa ufe katika Bwana na ukiishi uishi katika Bwana. tafakri na uogope hilo.
 
Why do women live longer than men .
20240301_185319.jpg
20240301_185303.jpg
20240301_185256.jpg
20240301_185252.jpg
20240301_185248.jpg
20240301_185243.jpg
20240301_185222.jpg
20240301_185218.jpg
20240301_185213.jpg
 
Niataeleza Kwa upana wa uelewa wangu:-

1.Ki Baiyolojia.
-wanaume tunazalisha Hadi uzeeni yaani tunaendelea kuwa na hamu ya kufanya ngono Hadi uzeeni ndio maana tunaoa hadi wajukuu,lakini kina mama Wana menopause ambayo huwasaidia kutunza virutubisho vyao hadi Hadi ubibi kizee!!kadiri mwanaume anavyofanya ngono ndivyo anavyokaribia kifo,IPO Siri katika kutofanya ngono ndio maana watawa wengi au jamii nyingi za siri hujitenga na ngono !!

2.Kiuchumi.

-Bado Sana sekta ya uzalishaji inaaminika ni ya wanaume yaani shughuli au kazi zote za nguvu na risky tunafanya sisi wanaume kwahiyo ajali,ulemavu,kupata sumu zinazoathiri mapafu,moyo,figo n.k hii inasababisha lifespan ya mwanamme kuwa fupi!

3.kijamii

Majukumu makubwa kenye familia,ukoo na jamii kapewa mwanamme ndio mtatuzi was changamoto za mahitaji ya wote,huu msalaba wanawake wamewatubebesha sisi hasta kama uwezo wanao,Hilo huleta sonona kwasababu ni ngumu kutimiza mahitaji ya wazazi,familia Yako na wazazi was mke wako Kwa pamoja,Bado presha ya kutotimiza hayo inamuandama Kila siku!!

4.kisiasa

Bado sisi ndio tuna tazamiwa kupigania uongozi kufa na kupona na hio huleta maadui ndani na nje ya familia,kifo hakiepikiki Kwa style hiyo!!

5.Ulozi,maagano na laana

Kila mwanamme Hadi anafikisha miaka 50 ameshajaribu mengi Santa katika utafutaji,ulozi na uganga hadi maagano mabaya keshajaribu ambayo Yana matokeo.chanya au hasi huko mbeleni!!

Laana za watoto,wapenzi wazazi kutokana na kutotimiza matarajio Yao pia zinatuandama kila kukicha!

Kurogwa au kuchezewa shere pale unapopata unafuu.wa maisha pia hufanya maisha yetu kuwanmafupi!

Ukufuatilia sana kwenye ukoo au familia wanaume tuliofanikiwa ndio hufa mapema.sana.wakiacha mali ambazo.wakati mwingine hazidumu!

Ni kuwindwa na.kuwindana Hadi siku.unaenda!!Hilo nimeona sana!!

Wengine wanaweza ongezea!!
Hii nimeinukuu na kuipigia mstari kwa makapeni ya bluu kabisa.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Wanabodi napenda kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kutulinda na kutufikisha siku ya leo.

Pili nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli Laigwanan Edward Ngoyayi Lowasa kilichotokea tarehe 10/02/2024.Pia nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha ghafla cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga wakili msomi Imani Madega ambaye naye amefariki tarehe moja na Lowasa.Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Baada ya kupokea taarifa za misiba hii mikubwa kwa taifa letu, binafsi nikawa nawaza kuhusu namna ambavyo wanaume ndio mara nyingi wanatangulia na kuwaacha wake zao. Nikajaribu kupitia orodha ya watu maarufu waliofariki na kuacha wake zao ikawa ni ndefu mno kwa kifupi naomba nitoe japo kwa uchache:-

1.Abeid Amani Karume(Mkewe yupo hadi leo)
2.Edward Moringe Sokoine
3. Aboud Jumbe Mwinyi
4. Mwalimu Nyerere
5. Ben Mkapa
6. JP Magufuli
7. Dr. Omary Ally Juma
8. Maalim Seif Sharifu Hamad
9. Bernard Camillius Membe
10.Kapten John Komba
11. Moses Nnauye
12. Jomo Kenyatta
Listi ni ndefu sana.Sina maana kwamba wanawake ndio watangulie ila kwetu kama wanadamu na waja wa Mwenyezi Mungu tunajifunza nini?
Nawasilisha.

Ni kukataa mapema na ku behave well.

Wengine wanarogwa, life style anayoongea Prof Janabi,
Wanaume wengi hawafanyi physical activities ambazo ni mbadala wa mazoezi unlike women.

Kataa kurogwa.
Usikae kizembe , jizoeshe kutembea na kufanya physical activities,
Usibebe mambo kifuani, yaseme , kuwa tayari kuachana kwa faida ya afya yako
 
Fanya utafiti huu, mwanaume na mwanamke wanaolingana umri na afya, wafunge kula uangalie nani atachoka zaidi, anaefifia zaidi ndie atakaetangulia kufutika katika uso wa dunia. Hapo utajua ni kwa nini wanaume wanatangulia kufa.
 
Back
Top Bottom