Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

Vijana wa bongu ujuaji
Mnapinga hata tu. Hata hoja kidogo hamna

Tunaifa la hovyo sana
Hivi katika hii mada ulivyo isoma hujajiuliza chochote kuhusu ukweli wa mada husika au umependa stori na picha ?

Mimi nilivyo soma hii mada cha kwanza nilianza kuhoji au kujiuliza juu ya picha ukiangalia kwa umakini hizo picha ni picha bunifu hakuja picha hata moja ambayo ni halisi.

Kingine kuhusu vipimo na utoaji wa majina na maelezo ya jambo husika,maelezo yanaonyesha ya kuwa wahusika hawana maarifa sahihi juu ya anga na vilivyomo. Swali la msingi nililo jiuliza ni kuwa wametumia mchakato gani kujia ukubwa wa hilo jiwe ?

Nani wa kwanza kutambua uwepo wa jiwe hilo na ilikuwa lini na alijuaje kuhusu jiwe hilo ?
 
Mwana kulitafuta,mwana kulipata! Bado Corona walioichokonoa uko China haijatuacha!!
 
Ukisoma comments za humu na ukaambiwa Hawa ni watu wazima wenye makende yaliyokomaa unaweza ukachoka Aisee,
Hivi wabongo aliyewafundisha ujuaji ni nani?
Watu wapo field wanapiga kazi watu Kama nyie kutoka huko Nanjilinji na namtumbo mmeshika simu za android kupinga project za wanaume wa kazi et AAA uongo,chai,haiwezekani,
bla bla za Mungu wenu sijui kufuru,wanamjaribu Mungu,Mungu Ndie atakaye tulinda,huo ni mpango wa ibilisi sijui hawatafanikiwa!
Daaaaaaa inasikitisha Sana!

Maujinga tu yapo vichwani mwenu Tena wengine ni members ambao hua naona angalau kidogo akili zenu zinachaji kumbe likija swala la kisayansi lakugusa dini zenu mnajulikana Kwa ujuha wenu
Shwain!

Elimu! Elimu!Elimu!
 
Umeongea point shida yetu hatuko huru kimawazo kwasababu tunatetea vile tulivyoaminishwa kuwa ndivyo vilivyo na tunapinga vile ambavyo vipo nje ya kile tunavyovifahamu au tulivyoaminishwa ni kama tuko programmed naamini ukweli wa kila jambo upo ndani yetu haya ya nje ni kama milunzi mingi usipojitambua itakupoteza.
 
walokole utawajua tu
 
Tunawasiwasi na matokeo ya hizo tafiti zenu za ki sayansi, maana lolote lile linawezekana,unaweza pata matokeo chanya au matokeo hasi! Na hiyo ndiyo maana ya tafiti unajaribu kitu usichokijua matokeo yake yatakuwaje!!
 
Umeandika kwa kutumia maarifa yepi? Dini? Uraia? Uchumi? Au uwezo wako tu wa kufikiri? Kz kifuatacho utaanza kusema hata zile satellites wanazituma Mars siyo kweli.. Nijuavyo hii project ya kujifunza ku-diverge miamba mikubwa imeanza miaka mingi--- sasahivi wapo kwa testing the implementation..
Na siku nilipojua kuwa ndugu wanamonitor kila asteroid angani kupitia deep space network zao za Spain, Australia na Carlifornia, na wanapeana shifts kama intern Doctor hospitalini, siku ile ndo nikajifuta macho na kujiuliza what role am i playing hapa duniani?
Acha sisi tuendelee kubeza ila ukweli ni kwamba people are very serious!
 
Nimekukubali mzee.. Ukweli ni kwamba watu wapo serious na haya maisha, na hii dunia yetu.
 
Hili ni dili la kuchota matrillion kwa kutishiana vitu ambavyo havipo, hapa nchi zote tutachangishwa pesa kwa madai wanarusha makombora ya kulipiga hilo jiwe, kumbe wanarusha sattelite zao tu, na mchango tunalipishwa
Lini ulishalipishwa pesa!? Tuna pesa za kuwalipa NASA kweli!!?? Wakati mwingine ni vema tukawa wasomaji na watazamaji tu.
 
Wabongo sisi kwa kuwa hakuna tunachokijua,basi tumebaki kupinga tu.wenzetu wako busy kuilinda dunia.
 
Bado watu wengi wanaamini kwamba dunia ni flat, yaani kama uwanja wa mpira - na ngumu kuamini kuna eti sayari nyingi zinazunguka jua bila kugongana miaka mabillion kwa mabillion. Wachache wameanza kuamini ni duara baada ya kuona kwenye TV watu wa Asia ama marekani wanashangilia mwaka mpya ili hali sisi bado tumelala ama mchana kweupe.

Hii sayansi ya unajimu kwa mtu asiyeelewa ni kama unamwelezea uchawi.

Kwangu mie habari hii n i njema na nasubiri na sisi Watanzania ni lini tutarusha satellite yetu kwenye anga za mbali kufanya security ya dunia nikingali hai.
 
Nimegundua Wabongo wengi ni watu wapumbavu na wajinga wajinga sana ndio maana ni maskini nadhani hatuna elimu stahiki na tumekua brainwashed na imani wakati imani yenyewe inasema tutumia maarifa ku solve problem

Huwezi kaa tu ukatengemes imani itakuponya kama hujitumi kwa maarifa ulionayo ebu tujifunze jamani tupate elimu ya vitu tuache kusema wazungu ni waongo wakati wanafanikiwa kupitia maarifa yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…