Dart: Mpango wa kulishambulia jiwe kubwa la Dimorphos linalokaribia kugonga dunia kuanza

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Chombo cha anga za mbali kiko tayari kuanza safari yake na kupima teknolojia ambayo siku moja inaweza kuhitajika kutambua mwamba unaozunguka uzio wa jua.

Safari hiyo ya NASA itatathimini pendekezo la muda mrefu la kumaliza mwamba huo ulioko katika anga za mbali unaoelekea kwenye dunia.

Chombo hiki cha anga za mbali kitaanguka kwenye kitu kinachoitwa Dimorphos kuangalia ni kwa kiasi gani kasi na njia yake inaweza kuharibiwa.

Kama kifusi cha cosmic chenye urefu wa mita mia moja kitagongana na sayari yetu, inaweza kusababisha maafa makubwa.

Hili ni jaribio la kwanza la kuzuwia mwamba huu unaozunguka dunia kwa melengo ya kujifunza jinsi ya kuilinda dunia, ingawa aina hii ya mwamba unaolengwa wakati huu sio tisho.

"Dart itakuwa ikibadili kipindi cha uzio(obiti) ya Dimorphos kwa kiasi kidogo.

Na hilo kusema kweli ndio tu linalohitajika katika tukio ambapo mwamba utagundulika kabla ya muda ,"anasema Kelly Fast, kutoka ofisi ya uratibu wa ulinzi wa sayari ya Nasa.

Infographic
Miamba inayozunguka jua ni mabaki yanayosalia katika ujenzi wa mfumo wa jua, huku mingi ikiwa haina tisho lolote la hatari kwa sayari yetu. Lakini wakati njia ya mwamba inapoziba njia inayozingira jua inapita ile ya dunia ili vitu viwili viweze kupita kwa wakati mmoja, na hivyo mgongano wa vitu hivi viwili unaweza kutokea.

Safari ya chombo hicho -Dart inayogarimu dola milioni 325 (£240m) italenga miamba miwili ambayo uzio wake unakaribiana - inayofahamika kama binary. Mwamba mkubwa zaidi kati ya miamba hiyo miwili, unaitwa Didymos , ukiwa na ukubwa wa karibu mita780 , huku mdogo zaidi ukiitwa Dimarphos-wenye upana wa mita milioni - Dimorphos - una upana wa mita 160.

Ukubwa wa Dimorphos unaweza kulipuka kwa kiwango cha nguvu sawa na bomu la nyuklia mara nyingi, na kusababisha maafa katika eneo linalokaliwa na watu wengi na kuwajeruhi makumi ya maelfu ya watu.

Miamba hii inayozingira dunia, mithili ya sayari ndogo(Asteroids) yenye milimita za ujazo 300 na mikubwa zaidi inaweza kusababisha uharibifu mkubwa katika sayari, huku miamba mikubwa zaidi ya kilomita 1 inaweza kusababisha athari kote duniani..

Halafu kitazuwia binary kitakapokaribia umbali wa katika eneo la maili milioni 6.7 za dunia Septemba 2022.

Dart kitapasua na kuingia ndani ya Dimorphos kwa kasi ya karibu mita 15,000 kwa saa (6.6 kilomita kwa sekunde). Hii inatarajiwa kubadili kasi ya mwamba huo kwa kasi ya milimita moja kwa sekunde-na matokeo yake kuharibu uzio wake unaozingira Didymos.

Chombo cha anga za mbali chanasa sauti za miamba ya sayari ya Mars
Ni mabadiliko madogo sana, lakini inaweza kutosha tu kugonga kitu kinachoenda kugongana na dunia.

Infographic
Kuna miamba mingine mingi midogo inayozingira jua kuliko mikubwa na kwa hiyo kuwa na uwezekano wa tisho ambalo tumewahi kukabiliana nalo -kama tutawahi kukabiliana nalo-huenda litakuwa ni kutoka kwa mwamba wenye ukubwa wa aina hii ,"amesema Tom Statler, mwanasayansi anayesimamia safari hii katika Nasa.

Dart kinabeba kamera inayoitwa Draco ambayo itatoa picha za miamba yote inayozingira jua na kusaidia chombo kujiendeleza katika mwelekeo sahihi ili kugongana na Dimorphos.

Takriban siku 10 kabla ya Dart kugonga shabaha yake, chombo cha anga za mbali cha Marekani kitatuma setilaiti ndogo, iliyotengenezwa Italia inayoitwa LiciaCube. Setilaiti hiyo ndogo itatuma duniani picha za tukio, kuondolewa kwa kifusi na shimo lililotokea kutokana na athari ya tukio hilo.

Chombo hicho kina maabara asilia muafaka kwa ajili ya kipimo cha aina hiyo. Kugongwa kw ana chombo hicho kutabadili uzio wa Dimorphos uliopo karibu na Didymos kwa takriban 1%, badiliko ambalo linaweza kugunduliwa kwa darubini ya ardhini kwa wiki au miezi kadhaa.

Hatahivyo, iwapo Dart kingejigonga katika mwamba wa wenyewe, muda wake wa uzio unaozunguka Jua ungebadilika kwa karibu 0.000006%, jambo ambalo lingechukua miaka mingi kulipima.

Mwamba wa binary ni mdogo sana kiasi kwamba hata kwa darubini zenye uwezo mkubwa wa kuvuta picha

BBC
 
Chombo cha anga za mbali kiko tayari kuanza safari yake na kupima teknolojia ambayo siku moja inaweza kuhitajika kutambua mwamba unaozunguka uzio wa jua.

Safari hiyo ya NASA itatathimini pendekezo la muda mrefu la kumaliza mwamba huo ulioko katika anga za mbali unaoelekea kwenye dunia.
Asante sana kwa Elimu
 
Nilivyoona Dart nikajua ni ile yetu Dar Rapid Trans nikakimbilia kuona advancement yetu kumbe ni wenyewe🤣😂
 
Sisi wakaazi wa dunia tumeshirikishwa!? Likisambaratisha kokoto huku si tutakufa kizembe?hao NASA nani kawaruhusu?
 
Back
Top Bottom