Nasa imepokea ujumbe toka angani

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Kampuni ya Nasa inayojihusisha na masuala mbalimbali ya utafiti na safari za Anga(spaces) imepokea signal Toka kwenye chombo kilichoruka umbali mrefu.

View attachment 2824594

Jaribio Hilo la Nasa la Deep space Optical Communication (DSOC) kupitia chombo Cha Pysche liliweza kuwakilisha kiwango kikubwa Cha mafanikio kupitia teknolijia ya mawasiliano Angani.

Ni jaribio la Kwanza kufanikiwa kwa chombo kuweza kurudisha ujumbe Toka umbali mrefu wa miles milioni 10 ni zaidi ya mara 40 umbali Toka duniani mpaka mwezini ambapo mawasiliano yalifanyika kupitia radio signal ambayo imetuma na kupokea ujumbe Toka kwenye Antenna kubwa iliyopo duniani.

NasaSpace%20%E2%80%93%201.jpg


Waliongezea kwa kusema kwa sasa upelekaji wa data kiwango chake ni kidogo mno Yani ni mdogo mdogo hivyo ni ngumu au haiwezekan kutuma file kubwa kama vile picha na video zenye ubora.

Pia Nasa kupitia DSOC walisema teknolijia hii inaweza kuboresha viwango vya data kwa zaidi ya mara 100 lengo ni watu kuweza kufanya mawasiliano na watu wengine wakiwa mbali na Dunia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom