Tetesi za ndani zinaonyesha misemo ya chini chini kuhusu idara hii nyeti ya serikali, hasa baada ya jaribio la kumuua kwa kumchinja engineer mmoja aliekuwa amelazwa Hospitali ya Muhimbili kutofanikiwa.
Mtazamo uliopo ni kwamba matukio mengi ya ukatili wa kupita kiasi yanayofanywa na Wasiojulikana yanaonekana kufanywa na watu wanaotoka upande wa pili wa nchi wa uongozi wa nchi, hali ambayo inaonekana kama kunakuwa na element za chuki binafsi dhidi ya wahanga wanaotoka upande mwingine wa nchi.
Na minong'ono inaendelea kuwa mara nyingine wafanyakazi wa idara hii nyeti ya serikali wanaotoka upande wa pili wa nchi ni kama wanaji-organize na kufanya kazi kivyao bila maagizo ya kiofisi, kama vile kujichukulia hatua wao wenyewe kwa kulinda maslahi ya mtu wa juu wanaemuona kuwa mtu wao.
Kuna ishara kwamba baadhi ya wafanyakazi wa idara hii nyeti wanaotoka upande mwingine wa nchi wameanza kuonyesha dalili za kutokubaliana na mambo yanayofanywa na wale wanaotoka upande mwingine wa nchi, na kuona kuwa wanapita kiasi katika yale wanayoona ni majukumu yao ya kazi. Kuna minong'ono kati ya baadhi yao kwamba wanaofanyiwa hivi ni wenzetu!
Kuna mmoja wao amekumbusha kwamba mpasuko wa namna hii ulikuwapo pia wakati wa awamu ya pili, na kukumbusha kwamba watu wa upande wa pili walihusika pia katika kumchinja injinia mwingine pale UDSM wakati wa mgomo uliopelekea UDSM kufungwa kwa mwaka mzima. Kauli ya "hawa jamaa kuchinja mtu ni kawaida yao na wanaona ni jambo dogo tu" ilisikika.
Inaonekana mambo yote haya ni sehemu ya jedwali kubwa ambalo limetia ndani baadhi ya wanene wa serikali kuamua kujitoa kwenye unene wao kutokana na mambo ambayo yamekuwa yakiendelea nchini, ikiwa ni namna ya wonyesho kwamba hawakubaliani na wanayofanyiwa watu wa upande wa pili wa nchi na staili ya uongozi wa nchi kwa ujumla.
View attachment 3392545
Ona pia:
Kwanini siku hizi Idara ya Usalama wa Taifa ya Kisiwa maarufu cha 'Puerto Rico' Watendaji wake WANACHUKIANA mno na kuna MPASUKO mkubwa sana?